CHADEMA yaibwaga CCM Arumeru Mashariki; CCM Yakubali kushindwa (Zaidi ya kura 6,000)

well.. tangu jana mmeona nikiripoti lolote toka ARumeru? don't doubt it. Kama ulikuwa na mpango wa kwenda kusherehekea you have my permission.

watu hawakujuwi na hawajuwi kama hawakujuwi.

kuna mtu alisema utashuka thamani kwa 99% nikamwambia shhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh!
 
Kwakweli leo hata kazini nimeamua kutokwena kazini watanisamehe kwa leo acha nisherekehe ushindi
A%20S-omg.gif
happy PEOPLEZZZZ.
 
Mkuu amenipa moyo wa kwenda kulima lile shamba langu arumeru kwa kweli..
 
Arumeru hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Hongera sana CDM,
Hongera sana Nasari,
Hongera Sana Dr. Slaa ( Dokta wa ukweli),
Hongera sana Mbowe
Hongera sana Zitto Kabwe,
Hongera sana Nyerere MB
Hongera sana wabunge wote wa chadema,
Hongera sana wapiganaji wa CDM
Hongera sana wana Arumeru kwa kuutaa ufisadi
Mwendo mdundo mwaka 2015 Mungu yuko pamoja nasi
 
Subirini sasa propaganda za ccm. "Sisi tumekubaliana na matokeo ya uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki. Tunaonyesha ukomavu na uvumilivu wa kisiasa kama taasisi. Hiyo ndo gharama ya demokrasia. Tunavisihi vyama vingine kuiga ustaarabu huo usio na maandamano ambayo kimsingi hayana tija kwa maendeleo ya Taifa". (wanakuwa wamemsahau livingstone, shortly).
 
Kilichoniudhi mimi ni kuwa tunaifanya demokrasia kuwa ngumu kweli; hadi damu, polisi, mabomu n.k it is silly.. ingeweza kuwa rahisi kweli kabla watu hawajaenda kulala kila kitu kimemalizika. Inakuwa kana kwamba tunaanza kufanya uchaguzi leo!! That really upset me.

Nami pia uwa napata shida sana hivi atufiki sehemu mfumo ukakubaliana na reality, haya mambo ya kusema tunaishi kama juzi na si kama leo,wafike sehemu mfumo watambue si lazima wawaone CCM kuwa wanahaki milki ya kusimamia ujenzi wa Taifa letu,wote tu Watanzania na CDM kama Watanzania nao CCM ni Watanzania,hivyo nao wanastahiki fursa hiyo hiyo kama ambavyo CCM wamekuwa nayo siku zote mara baada ya kuipokea mwaka 1977.Na watu wenye nafasi ya kusimamia haki ya CDM ama haki ya CCM ni mfumo huo huo ambao unaweza kusimamia CDM kuongoza Nchi yetu kama wanavyo simamia CCM wakituongoza.

Ombi langu ni tufike sehemu walio kwenye mfumo watenganishe nguvu za mfumo na vyama vya siasa,nguvu za mfumo zisimamie TAIFA kama Nchi na si kusimamia matakwa ya chama au vyama vya siasa na utashi w kisiasa kugandamiza haki ya vyama vinginea au wananchi wengine. Vyama viwe ni vyombo vya kuonyeshea dira na kusimamia maendeleo ya Taifa,chini ya ulinzi na macho yenye kanuni za mfumo kwa niaba ya Taifa,vyama vije na wagombea wao wapite lakini mfumo utabaki kuwa ule ule kwa maslahi ya Taifa na vizazi vyake.

Binafsi sitaki kuamini kwa wanamfumo kuna watu ambao bado wanaamini hali ya kisiasa ya Tanzania,bado ni ile ile ya fikra za mwenyekiti zidumu na chama kidumu.Mimi ni kijana wa kizazi kipya ambae naona kama vijana wengine wanavyo ona,tulipofika kama Taifa kwa njia za chama kilicho tawala kwa miaka hamsini [50] tunaitaji mabadiliko hata kwa hali ya kawaida binadamu yoyote kisaikolojia akiishi na kitu kwa muda mlefu ukinai na kuona kuwa kitu hicho kwake ni mazoea na hivyo ili kuludisha matanio upya kwake ama kitu kile kitoke kije kipya ama kibadilishwe baaadhi ya vitu vilivyo ndani ya kitu husika ili kuondoa ule uchovu wa mazoea.

Ni hakika viongozi wetu wengi na baadhi ya wanamfumo ni kizazi cha uhuru,lakini wa haitoshi kusema wana halalisha mwenendo wa kuendesha maisha ya Watanzania kwa kuzingatia vigezo vya miaka ya watu wa fikra za uhuru.Taifa kama Taifa watu wanapokezana uongozi wa vyama na mfumo kama zilivyo mbio za vijiti.Nguvu ya mpokezi mmoja wa kijiti ndio mwanzo wa safari ya kumkabidhi mwingine ambae anakuja na nguvu mpya baada ya huyu aliyetangulia kuwa amechoka.Ubaya wa Taifa langu ni viongozi wa vyama na mfumo wamejiona na kujipa dhamana kuwa wenye maamuzi ya mstakabali wa Taifa kwa kuangalia enzi ya zama zao na sio kwa kupima kuongoza Nchi kwa njia ya ushirikishi wa kizazi kipya ambacho ndicho kinategemea kuishi zaidi ya kizazi cha watu wa uhuru kama ni kwa mapenzi ya Mungu.

Lawama za haya yote tulipofika ni watu wa mfumo ambao kwa nguvu ya maarifa na busara yao walipaswa kujua Taifa linajengwa na kuimalishwa na aina mpya ya nguvu zenye mawzo yanayoendana na nyakati,with all problem with Mzee Mwinyi kwangu uwa namkubali yule Mzee pamoja na kutofanikiwa kiuchumi lakini kwa busara nzuri yule Mzee anastahki na ndio maana watu hawana maneno nae,na hata alipopigwa kibao watanzania walimtetea tofauti na viongozi wengine.Moja ya kauri ambaz mimi uzipenda ambazo alipata kusema na kuonyesha kweli kwa vitendo kuwa anamaanisha hivyo ni hii ya KILA ZAMA NA VITABU VYAKE.

System should wake up and see what Mzee Mwinyi alipata kuaddress kila zama na vitabu vyake,yani kila kizazi kina namna yake ya kuishi,na hivyo basi watu walio kwenye mifumo wanapaswa kuliona hilo na kulifanyia kazi aijalishi walio kwenye CCM ndio walioshirki kuleta uhuru na kuwa ndio wanaojua dhaman ya Taifa,hapana ni vyema kusoma alama za nyakati na kutoka huko.Manake mfumo kuendelea kungangania kuwa CCM bado ni kiongozi mwema wa kuonyesha njia ya kizazi cha sasa chini ya miaka 45,kwa style ya wazee wale wale [Wasira,Mkapa,Lusinde na Mzee wa Matusi ya Aibu] ukweli haitawezekana na zaidi ni aibu na kuongeza chuki ambayo hata ambao hawakuwemo kwenye mkumbo huo wataingia kwenye mkumbo huo wa kusulubiwa pamoja na walengwa wa historia.

Mfumo ujisimamie binafsi ujitoe kwenye kutumikishwa,waachwe CCM wapambane na hali halisi.Kuendelea kumsimamia CCM, mfumo ambae ndiye mzazi, na CCM ndie mtoto ambae anaonekana kwa umri wa miaka hamsini [50] bado yuko nyumbani na anakula na kulala kwa hisani ya Baba yake ambae ni mfumo.Kwa picha hiyo Baba Mfumo na mazingira ambayo anamjengea mwanae huyo [CCM] eti kwa kuwa ni wa kwanza hakika anamvisha kilema na woga wa kujitegemea kuishi kama ambavyo watoto wengine wa Baba Mfumo kama CDM na CUF na wengineo wanajitegemea wenyewe hivyo kuzalisha ugoigoi na kuonekana mtoto wa Mama hata kama mzazi uenda alikuwa na nia njema kwa mwanae huyo lakini huruma ya aina hiyo inaponza toto na kuzua janga la toto kutoweza kumudu kuishi kulingana na hali halisi ya maishaya Watanzania.

Yaliyotokea Arumeru aungulumapo simba mcheza nani?
 
NIKIWA KAMA MWANA CCM KIPENZI.

hongera chadema, hongera joshua nassari, hongera wana arumeru, hongera ccm kwa kukubali matokeo, hongera sioi kwa kujaribu! Sasa mh. Mbunge mteule, joshua nassari, hudumia wananchi wako wa arumeru mashariki na watanzania wote bila kuweka mbele itikadi za kisiasa. Wapende pia sana wale waliokunyima kura hasa zile kata ambazo ccm imeshinda uwe karibu nao zaidi uwaondoe hofu yao. Demokrasia imeongea wana wa arumeru mashariki wameongea.


BUCHO WA JF
Safi sana BUCHO umeonyesha ukomavu!
 
:welcome: Mhe Joshua Karibu Mjengoni! aluta kontinyuuuuuuuuuuuuuuuu! Tugenge mising ya shindi mkuu 2015! Piiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiipooooooooooooooooooz! pawaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Hakika hii ni nguvu ya Umma. Wapambanaji tusirudi nyuma, Kuna baadhi ya maeneo yanahitaji nguvu kama mkoa wa kagera. Tunaomba msaada mkubwa wa hamasa hasa kwa viongozi wa kitaifa. Tunatarajia kufungua ofisi ya tarafa ya chama huko nshamba mwezi wa sita. wapambanaji jitokezeni kutupa support ili tukio hili liwe la kitaifa. Tuwasiliane kwa no. 0755925228, 0655925228 na 0786608230
 
hongera chadema sauti ya wengi saut ya mungu joshua nasari mungu akupe uwezo wa kufanya kazi kwa umakini ili kufanokisha maendeleo ya arumeru mashariki na taiga kwa ujumla mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom