Siasa mpaka sokoni? Big up kwa aliyeshinda
DAR, mnasikitisha duniani. Katika dunia hii ni majiji mawili tu, ndio bado yanakumbatia siasa za chama tawala, DAR na mdogo wakeTANGA. Hayo ndio majiji jinga dunia nzima. Kila kitu kipo dar, kashfa zote mnazisikia dar kwanza lakn mmekuwa wa mwisho kuzielewa.
Ndugu wanajf, jana kulikuwa na uchaguzi wa mwenyekiti wa soko la nguzo nane lililopo shy mjini. Uchaguzi huo uliwakutanisha uso kwa uso makada wa vyama viwili asimu nchini namaanisha CHADEMA na ccm. HASSAN BARUTI, Mwenyekiti wa BAVICHA wilaya ya shy mjini ambaye ni mfanyabiashara wa soko hilo alimkabili mwenyekiti aliyemaliza muda wake, ABDUL KIDODE, kada wa ccm, na mfanyabiashara mwenye bucha nyingi mjini hapa. Mwisho wa uchaguzi kamanda HASAN BARUTI alishinda kwa kupata kura 445 dhidi ya mpinzani wake mwanaccm, ABDUL KIDODE, aliyepata kura 120 tu. Nawasilisha.
Mwendo ni huo huo kuanzia grassrooot level. Hata ukitokea uchaguzi wa umoja wa wauza kuku, tunaweka mgombea na tunawabwaga wanamagamba.
Sasa mwenyekiti wa Soko au raisi wa DARUSO hivi ni vyeo vya kisiasa mpaka mchuano uwe kati ya vyama? Athari za kuingiza siasa kila mahali baadaye zitaleta matatizo makubwa sana katika ustawi wa umoja wa kitaifa. Sasa na mimi kama ni chama X nikitaka wafanya kazi nitafute wafuasi wa chama X?
kwako wewe ni hopeless, lakn kwetu ni hope. Kwako ni wastage of time, lakn kwetu ni progress. Hayo yote ni mapito kuelekea ukombozi wa kweli. Hatutarudi nyuma na badala yake tutasonga mbele kwani mwenyezi mungu yu pamoja nasi.Hopeless kabisa mlishindwa Urais wa Nchi leo mnajifariji ushindi wa sokoni! Tehetehethe wastage of time CDM!
Sasa mwenyekiti wa Soko au raisi wa DARUSO hivi ni vyeo vya kisiasa mpaka mchuano uwe kati ya vyama? Athari za kuingiza siasa kila mahali baadaye zitaleta matatizo makubwa sana katika ustawi wa umoja wa kitaifa. Sasa na mimi kama ni chama X nikitaka wafanya kazi nitafute wafuasi wa chama X?
hayo ya kweli kabisa, akija usalama wa taifa na ffu wanakuwa nae popote anapokwenda. Hukushinda na alitangazwa kwa diff ya kura 1.Bado ubunge,manake nasikia hata huyo mbunge aliyetangazwa hakanyagi shy town for fear of being assasnated,wadau wa shy ya kweli hayo?
We upo nchni gani Bwana?
Soma hiyo taarifa tena, anaona hujaielewa, au una maanisha wagombea hawakupaswa kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa?
CCM wanaweka siasa hadi kwenye vijiwe vya Bangi, huoni bendera za mashina ya CCM!
Sikutegemea viongozi wa sehemu za huduma za jamii washindanishwe kwa itikadi ya vyama vyao. Kama ni sokoni wangeangalia mfanya biashara miongoni mwao atakayetetea huduma za wafanyabiashara kama usafi sokoni, kupatikana kwa huduma nyinginezo kama maji na vyoo.