CHADEMA yaibuka kidedea uchaguzi wa mwenyekiti NGUZO NANE - Shinyanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yaibuka kidedea uchaguzi wa mwenyekiti NGUZO NANE - Shinyanga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jiwejeusi, Jul 7, 2011.

 1. Jiwejeusi

  Jiwejeusi JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu wanajf, jana kulikuwa na uchaguzi wa mwenyekiti wa soko la nguzo nane lililopo shy mjini. Uchaguzi huo uliwakutanisha uso kwa uso makada wa vyama viwili asimu nchini namaanisha CHADEMA na ccm. HASSAN BARUTI, Mwenyekiti wa BAVICHA wilaya ya shy mjini ambaye ni mfanyabiashara wa soko hilo alimkabili mwenyekiti aliyemaliza muda wake, ABDUL KIDODE, kada wa ccm, na mfanyabiashara mwenye bucha nyingi mjini hapa. Mwisho wa uchaguzi kamanda HASAN BARUTI alishinda kwa kupata kura 445 dhidi ya mpinzani wake mwanaccm, ABDUL KIDODE, aliyepata kura 120 tu. Nawasilisha.
   
 2. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hongera CDM
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hongera Chadema- Bavicha SHy moto ni ule ule hakuna kurudi nyuma
   
 4. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Mwendo mdundo CDM! Twanga Kotekote.
   
 5. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Sokoni nako itikadi zimeingia?
   
 6. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  ndugu yangu Vincent,, siasa ni popote tena hizi za kuing'oa ccm zinatakiwa zisambae kwa kasi ya ajabu. cha msingi zisitupeleke kwenye kubaguana wakati wa shughuli/huduma za kijamii kwamba wa cdm huku na ccm kule. ibaki kama ushabiki wa mpira vile ambao jukwaani mnakuwa pande tofauti game ikiisha mnakaa meza moja mnapiga kinywaji
   
 7. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hivi unagombea nafasi ktk uchaguzi wowote ngazi yeyote mahala popote tanzania iwe ungozi wa soko, jumuia ya wanafunzi, umoja wa makonda, wapiga debe, wabeba mizigo, muwakilishi chama cha wafanyakazi au wakinamama katika saccos, kisha unajinadi wewe ni kada wa ccm, au hata usiposema watu wakibaini kuwa uliwahi kujihusisha na ccm muda na mahala fulani, au ukipakaziwa na mpinzani wako hivyo, ujue umekwisha maraia wanahasira na ccm watakupiga chini mbaya, kama hamjui chukueni hiyo.
   
 8. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  cdm haina udini, shinyanga wanatudhihirishia hilo.
   
 9. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Sasa mwenyekiti wa Soko au raisi wa DARUSO hivi ni vyeo vya kisiasa mpaka mchuano uwe kati ya vyama? Athari za kuingiza siasa kila mahali baadaye zitaleta matatizo makubwa sana katika ustawi wa umoja wa kitaifa. Sasa na mimi kama ni chama X nikitaka wafanya kazi nitafute wafuasi wa chama X?
   
 10. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Umenifurahisha na ukweli wako mkuu mfereji maringo. Ni kweli kabisa, saizi ukisema wewe ni kada wa ccm basi ujue wewe ni kama mwizi, jambazi au mhuni unayeibia watu wazi wazi. Tuiepukeni CCM jamani. Hongera CDM kwa kushinda mkoani kwangu japo kuna changamoto nyingi zinawakabili wakazi wa Shy na soko lao, mjitahidi kuliweka soka katika hali ya kisasa!
   
 11. M

  Mr EWA JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 15, 2007
  Messages: 332
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Siasa mpaka sokoni? Big up kwa aliyeshinda
   
 12. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wa kulaumiwa ni CCM waliingiza na sasa wana siasa kila kona .Now wenzao wanawafuata huko huko .Hebu angalia kuanzia FAT sasa TFF , mashuleni , Mashirika ya Umma nk kote ni siasa .Leo unashangaa nini ?
   
 13. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hongera cdm 'tuirukeni ccm wametukosea heshima
   
 14. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Siasa kwenye mashirika ya umma zilikoma mwaka 1992. Kabla ya hapo kila shirika la umma lilikuwa na menyekiti wa tawi la chama sehemu ya kazi na alishiriki kwenye vikao vya uongozi....hii ilipelekea mashirika kukosa ufanisi na kufa. Tuepuke siasa kwenye sehemu za huduma kwa jamii kama masoko, hospitali, stand n.k. vinginevyo tutaanza kugawa maeneo ya nchi kwa kufuata itikadi ya vyama kama Afrika Kusini.
   
 15. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,717
  Likes Received: 1,627
  Trophy Points: 280
  sijui kwa nini hapa dar tumelala maana ndio kwenye wabishi wengi lakini kwa vitendo ni zero yenye masikio
   
 16. Jiwejeusi

  Jiwejeusi JF-Expert Member

  #16
  Jul 7, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu, nafikiri haupo tz na wala hujawahi kuishi tz. Kuna watu walinyimwa kaz kwa sabab, walibambikiziwa kodi na tra, walifukuzwa sehemu za biashara na hata kubomolewa vibanda vyao kwa sababu tu walisapoti upinzani. ccm mnaingiza siasa kila mahala. Kwa kuwa sasa mmezidiwa, ndio mnataka turudi nyuma. Kamwe hatutarudi, tutasonga mbele, hatutaogopa kwa sababu tunae mungu. Tutashinda
   
 17. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ziliisha kinadharia tu, lakini kiuhalisia bado zinadumu..ni kawaida kwa mfanyakazi wa umma kurudi kazini baada ya kushindwa kwenye kura za maoni za ubunge/udiwani kwa ticket ya chama cha magamba ila kwa wale wanaogombea kupitia upinzani, hilo huwa ni kosa ka kuachishwa kazi,fatilia utaona
   
 18. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kama kweli vile!!! Kama mambo ni hivyo basi Chama cha Magamba wanahitaji wajitambue upya. Kama ni ubatizo basi waende wa kuzamishwa au wa moto.
   
 19. Jiwejeusi

  Jiwejeusi JF-Expert Member

  #19
  Jul 7, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  DAR, mnasikitisha duniani. Katika dunia hii ni majiji mawili tu, ndio bado yanakumbatia siasa za chama tawala, DAR na mdogo wakeTANGA. Hayo ndio majiji jinga dunia nzima. Kila kitu kipo dar, kashfa zote mnazisikia dar kwanza lakn mmekuwa wa mwisho kuzielewa.
   
 20. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #20
  Jul 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mwendo ni huo huo kuanzia grassrooot level. Hata ukitokea uchaguzi wa umoja wa wauza kuku, tunaweka mgombea na tunawabwaga wanamagamba.
   
Loading...