CHADEMA yahusishwa na hali ya Tanzania kutotawalika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yahusishwa na hali ya Tanzania kutotawalika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nickname, Jan 19, 2011.

 1. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Tanzania sasa mambo yanakwenda kombo viongozi wanahaha kunusuru na wengine nahisi wanajuta kwanini walichaguliwa kuwa viongozi.Kuna masuala mengi yanayowaumiza vichwa mara DOWANS,madai ya Katiba mpya,Mauaji ya raia wasioa na hatia Arusha na Mbeya,Umeya wa Arusha,migomo ya vyuo vikuu,migomo ya wafanyakazi na mambo mengi kadha wa kadha.

  Wanajaribu kusuluhisha na wengine wameshasema wazi kuwa CHADEMA wanahusika na hali hiyo inayojitokeza.Yaani kila viongozi wakikwama kusuluhisha migogoro utawasikia waropokaji na wanazi wa chama tawala kuwa CHADEMA ndio wanahusika.Jamani hii ni kweli?

  My Take : Mimi naona kuwa viongozi waliochaguliwa kuongoza nchi hii kazi imewashinda na wanatafuta mchawi.Walianza na Samuel Sitta wakaja kwa Tido Mhando na sasa baada ya maji kuwafika shingoni kila kitu wanawasingizia CHADEMA.Kama CCM na serikali yake wangeifanyia mema nchi hii na wananchi wake leo hii nchi hii kusingekuwa na shida zote hizi
   
 2. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Hivi mtu kama anadai mshahara wake, chama cha siasa kinahusikaje? Ingekuwa labda wanadai serikali ijiuzulu, kidogo tungetafuta mchawi ambaye lazima angekuwa na maslahi kisiasa
   
 3. a

  arasululu Senior Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mshaara wa dhambi ni mauti! usipoziba ufa utajenga ukuta! ukifanya mapenzi bila kinga mimba itakuumbua! CCM waliyafanya yote hayo sasa ndo saa ya kuumbuka na MUNGU anaanza kujibu maombi ya watanzania wametutes muda mrefu wakitufanya wajinga sasa tumeamka na hii ni trela movie iko kwa njia!! TUSHIRIKIANE KUITEKETEZA CCM NA SERIKALI YAKE DOWANS(DAWANS)  Mungu ibariki tanzania
   
 4. w

  wari2 Member

  #4
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  na tutegemea mambo mengi kuendelea kufichuka
   
 5. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Unapoongoza watu wenye uwezo kuliko wewe hayo ndo madhara yake. Mbinu zote za kufanya usanii zimeshindikana na hamna kiongozi anayemtania mtu akacheka. watu woote wana makunyazi na wamepoteza hisia za vicheko hadi hapo suluhisho la umeme, maji, barabara, kushuka kwa bei ya mafuta na gesi n.k litakapopatikana. Hivi ulishamchekesha mtu mwenye njaa ukaona ? Sasa viongozi wanapoona very clear kwamba nyuso za watanzania zina makunyanzi kusubiria umeme na huku wakijua haiwezekani kuwapatia huku matatizo mengine yanaibuka kama Dowans, migomo Vyuoni n.k ujue watafanya yale ya Mbaazi akikosa maua kusingizia jua
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Nadhani ni kupambana na adui ambaye hawamjui. Tatizo limeanzia kwenye uongozi wa juu wa nchi hii, maisha magumu, gharama za umeme juu, maji vyuoni hakuna, ruzuku kwa wanafunzi vyuoni mgogoro, na mengine mengi sasa cdm imehusikaje?
   
 7. B

  Batale JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,070
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Mimi naona tunakoelekea mengi yataibuka na hatimaye taifa kuangamia kabisa kutokana na viongozi wetu kukosa ujasiri wa japo kufukuzana na kukemeana. siasa imezidi ukweli imekuwa kuteteana tu hata penye upumbavu, angalia polisi kuwa na ushabiki na chama tawala na kuona mauaji ni sawa na baadaye wanatoa video ya kuchonga wakisema ndivyo hali ilikuwa, wanasahau kuwa sehemu kubwa yao(polisi) wanaishi na jamii ileile wanayoiua je siku ikiwafukuza wataenea kwenye nyumba zao(kambi)? au wananchi wakitangaza vita ya chini kwa chini na polisi watapona huko uraiani?, ajabu bado wanahitaji ulinzi shirikishi hii ni aibu.
   
 8. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,506
  Likes Received: 2,749
  Trophy Points: 280

  Ukifanya mapenzi bila kinga ..... Ukimwi utakuua!!! Sasa CCM in ukimwi na kifo kiko njiani.
   
 9. C

  Campana JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Je, kauli za kulumbana viongozi wa dini - ni CDM?
  Je, mgawo wa umeme na maji - ni CDM?
  Je, Taifa Stars kugaragazwa Misi - ni CDM?
  Je, kuadimika kwa gesi - ni CDM?
   
 10. tracy

  tracy JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  there is still more to know than what meets the eye!..kuna vitu vingi bado havijalipuka na naona viongozi wamekaa mkao wa kuanza mbio za 1000meters!..hii ndo TZ mpya!
   
 11. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  mi numeshasema humu kuwa lazima namna ifanyike ili tuondokane na utawala huu mbovu!!!! hatuwezi kuwa na mtu mwenye upeo mdogo kiasi hiki... lazima namna ifanyike hapa vinginrvyo tutalia sana bado parefu jamani hadi 2015?!!!
   
 12. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hapo Mvumbuzi umevumbua.

   
 13. Freestyler

  Freestyler Senior Member

  #13
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Lol..watasema alishasema nchi haitatawalika!..
   
 14. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Ukame unaolikumba taifa kwa sasa ni Chadema.
  Kushindwa kesi na kutakiwa kuilipa Dowans ni Chadema.
  Mazingira mabovu UDOM ni Chadema.
  Wizi wa fedha za walimu UDOM in Chadema.

  Huu sasa ni wendawazimu, si ni bora tusiwe na viongozi tujiendee kama kuku wa kienyeji. Huku ni kufilisika kifikra
   
 15. BigTime

  BigTime Member

  #15
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 17, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu MCHAWI wa CCM ni CCM wenyewe...wanaendesha hii inchi kama kimwaka 1947, hawataki kuelewa kuwa zama zile za uficho zimepitwa na wakati, mikataba feki na haramu inayoiangamiza taifa muda huu wanasingizia ni siri kwa ajili ya usalama wa taifa....!!!! Ha ha ha ha....serikali yetu inaendeshwa na wazee waliolala kimawazo na kimtizamo; ingawa ni hodari kwa vi-trip vya nje lakini hawajifunzi utandawazi na bado wanadhani TZ bado ni kisiwa kilichojitenga kwenye sayari ya kipekee huko angani, C'mon, watu wanajuwa nn kinaendelea...hapa ni KIKWETE kuvaa msuri na kuamua kucharaza bakora wote wanaohusika, na kiboko chake asichape huku anatabasamu; akifanya hivyo ndo nitamuona kweli ni rais kidume asiyehusika na uozo huu...

  Siku hz jinsi maisha yalivyo magumu, sitashangaa hata kidogo watu wakaingia mtaani kudai haki zao, kwani nchi zilizoingia kwenye machafuko walianza hivi hivi, watu wakichoka sana na serikali yao wataigeuka na hakuna atakayesalimika...watoto wa maskini waishio uwanja wa fisi, Tandika, Tandale, and like places watavamia majumba ya kifahari Oysterbay, Mbezi nk nk nk wakitaka wagawane kile Watanzania wenzao matajiri wanaown kwa wakati huo...na hiki ndo ninachokiona siku si nyingi kama huyu mheshimiwa asipoamua kumfunga paka kengele.
   
 16. BULLDOZZER

  BULLDOZZER Senior Member

  #16
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuanzia leo nchi ya tanzania haitatawaliki tena....................................( )
   
Loading...