CHADEMA yagomea mazungumzo na CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yagomea mazungumzo na CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 8, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,711
  Trophy Points: 280
  CHADEMA yagomea mazungumzo na CCM
  • Polisi waua Mkenya, ‘waharibu mimba’ ya mtu

  na Ramadhani Siwayombe


  [​IMG] KATIKA kujibu hoja ya Waziri wa Mambo ya Ndani Shamsi Vuai Nahodha aliyetaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Mapinduzi (CCM) vikae kuzungumza namna ya kumaliza mfarakano ulioleta maafa jijini Arusha, CHADEMA kimekataa pendekezo hilo kwa maelezo kuwa CCM na serikali yake ni katili na ya kihuni.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana, katika hospitali ya Mount Meru alikokwenda kuwajulia hali majeruhi wa vurugu hizo, akiwamo mchumba wake Josephine, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilibrod Slaa alisema: ”Hatuwezi kukaa meza moja na serikali ya kihuni. Tumepigwa, tumedhalilishwa huku tukiwa na vibali vyote halali vya kuturuhusu kufanya mkutano na maandamano, halafu haohao wanasema tukae meza moja kujadili nini?”
  Alisema pendekezo la Waziri Nahodha limechelewa na kwamba chama hicho kwa hivi sasa hakiwezi tena kukaa meza moja na CCM kujadili mvutano uliojitokeza kwani wakati serikali ilipoungana na CCM kuhujumu uchaguzi wa meya ilikuwa inajua matokeo yake.
  Alisema pendekezo la mazungumzo sasa hivi ni ghiliba ya serikali kuhujumu harakati za mabadiliko ya Watanzania wakiongozwa na CHADEMA.
  Alisema kitendo cha serikali kushambulia, kupiga na kuua waandamanaji badala ya kuwalinda ni uhuni usioweza kuvumiliwa; na kwamba CHADEMA haiwezi ’kununuliwa’ kwa mazungumzo ya mezani.
  Akizungumzia mchakato mzima wa kufanya mkutano na maandamano, alisema mchakato huo ulianzia mwaka jana ambapo yeye kama katibu aliwasiliana hadi na Msajili wa Vyama kuhusu suala hilo, tena kwa maandishi.
  Alisema kuwa Desemba 22 mwaka jana alimuandikia barua Msajili John Tendwa kumjulisha suala hilo na yeye akaahidi kulifanyia kazi kwa kuwasiliana na mkuu wa jeshi la polisi na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Mkuchika ili kuona uwezekano wa kuitishwa uchaguzi mpya katika maeneo yaliyokumbwa na matatizo.
  Januari 3 mwaka huu Msajili aliwasiliana naye kwa simu kutaka kujua makubaliano ya awali, akaahidi kuwa kabla ya Januari 4 angekutanisha pande zote kujadiliana suala hilo.
  Jioni ya Januari 3 Tendwa alimpigia (Dk. Slaa) simu na kumwambia kuwa waendelee na taratibu zote za maandamano pamoja na mkutano wa hadhara na akashauri katika mkutano huo wazungumze kiistaarabu na wasitoe kashfa kwa yeyote ili chama kiendelee kupata heshima kwa jamii.
  Kwa mujibu wa Dk. Slaa akiwa njiani kuelekea Arusha Januari 4, Tendwa tena akampigia na kumuuliza alikuwa wapi na alipomjibu kuwa yuko njiani kuelekea Arusha akamuuliza kama walikuwa tayari kuahirisha mkutano endapo waziri wa TAMISEMI angetangaza kurudiwa kwa chaguzi zote za mameya katika maeneo yaliyokumbwa na vurugu. Dk Slaa akamjibu kuwa ni vigumu kuahirisha mkutano kwa kuwa umeishaandaliwa kwa gharama kubwa.
  ”Baada ya kuwasiliana na kuelezana hayo nilimtania kidogo Tendwa nikamuuliza kwa kuwa alikuwa nyumbani Same ’niambie wapi ntakuta mahindi yangu ya kuchoma ili nikifika Arusha nikayachome nile’ kwa kuwa huwa mara nyingine nataniana naye,” alisema Slaa.
  Alisema kuwa simu za Tendwa hazikuishia hapo na baadaye siku hiyo hiyo saa 12 jioni alinipigia na barua kadhalika alituma.
  “Na mimi bahati nzuri nikafahamishwa na watumishi ofisini kuwa imeishafika, na hivyo Tendwa tena, akaniambia anawasiliana na Mkuchika kujua kama ameishatoa tangazo la kufanyika kwa chaguzi,” alisema.
  Katika hilo Slaa alisema kutokana na hayo yote aliyoyafuata kitaratibu kufanikisha mkutano huo na barua ya mkuu wa polisi wilaya (OCD) kuruhusu kibali cha maandamano na mkutano na kuambulia kupigwa sasa, hawaoni sababu za kukutana na serikali ya aina hiyo kujadiliana nayo.
  Maaskofu walaani polisi, wamkataa meya Arusha
  Katika hatua nyingine, umoja wa maaskofu wa Kikristo Mkoa wa Arusha wametoa tamko kulaani ubabe na ukatili wa polisi kupiga na kuua waandamanaji.
  Akisoma tamko hilo la pamoja kwa niaba ya viongozi wenzake wanaounda umoja huo jana katika hoteli ya Korridor Spring, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, Josephat Lebulu, alisema Jeshi la Polisi ndilo chanzo cha ghasia na mauaji hayo na ndilo linapaswa kubeba lawama.
  Alisema machafuko hayo kwa kiasi kikubwa, yalisababishwa na polisi iliyotoa maamuzi mkanganyiko yaliyowachanganya wananchi.
  “Wao walitoa kibali cha kufanya mkutano na maandamano, halafu mara ghafla, dakika za mwisho, wanakataza maandamano; na kama hiyo haitoshi wanatumia nguvu kubwa kuwatawanya watu kwa mabomu na risasi. Kwa nini wanasababisha vurugu badala ya kuzuia?” alisema Askofu Lebulu.
  Askofu huyo alitamka wazi kuwa maaskofu hao, wakiwa sehemu ya wananchi, hawamtambui Meya Gaudensi Lyimo aliyechaguliwa kinyemela kwa kuwa hakupatikana kihalali; akasisitiza kuwa hawako tayari kufanya kazi naye.
  Alisema kuwa wao kama umoja wa viongozi wa dini mkoa wa Arusha wanaitaka serikali kuchukua tukio la Arusha kama jambo la kitaifa kwa kutoa maelezo ya kutosha na ya kuridhisha kwa Watanzania wote na jamii ya kimataifa ili kurejesha na kujenga upya imani ya wananchi kwa serikali yao.
  “Sisi tunataka haki itendeke na haki ionekane imetendeka. Uchaguzi haukuwa huru wala wa haki, maana hata vyombo vya habari vilituhabarisha kuwa wengine hawakupiga kura na wengine wasiokuwa wakazi wa Arusha walipiga kura. Hili jambo linatakiwa nalo lifanyiwe uchunguzi,” alisema Askofu Lebulu.
  Alisema njia pekee ya serikali kuifanya nchi iwe na amani na kuongozwa kidemokrasia, ni kwa serikali kutenda haki kwa kufanya uchaguzi mwingine ambao utakuwa huru na wa haki.
  Idadi ya waliokufa yaongezeka
  Wakati huo huo, idadi ya raia waliokufa katika vurugu hizo imeongezeka kutoka watatu hadi wanne, huku polisi wakibainika kumuua pia raia mmoja wa Kenya, aliyefariki katika Hospitali ya Mount Meru.
  Awali, polisi walikuwa wametangaza kifo cha raia aliyetambulika kwa jina la George Waitara, lakini baadaye imegundulika kuwa marehemu hakuwa Mtanzania na jina lake halisi si Waitara bali Paulo Njuguna Kaiyela.
  Njuguna amefahamika baada ya kupatikana kwa vitambulisho vyake ambapo kitambulisho chake kinamtambulisha kama raia wa Kenya kina namba 25066938 na sirio namba yake ni 218733089.
  Hadi jana kulikuwa na majeruhi 17 katika hospitali za Mount Meru na St. Theresa. Miongoni mwao, 11 walijeruhiwa kwa risasi na wawili miongoni mwao ndio waliotolewa vipande vya mabomu. Baadhi ya majeruhi bado wana risasi mwilini na wamelalamikia kuchelewa kutolewa risasi hizo.
  Kati ya majeruhi hao, yumo mwanamke mmoja aliyekuwa mjamzito, ambaye kutokana na kipigo alichopewa na polisi mimba yake imeharibika na kutoka.
  Majeruhi mwingine ambaye ni dereva wa Mbunge wa CHADEMA, Grace Kiwelu, amepoteza uwezo wa kuhisi, na pia miguu imekufa ngazi.
  Madaktari waliozungumza na gazeti hili, walisema kuwa wanaogopa kumpeleka hata kwenye chumba cha X-ray kwa sababu hali yake inaweza kuwa mbaya zaidi.
  Akizungumzia malalamiko ya majeruhi hao Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Mount Meru Salash Toure alisema majeruhi wameishapata huduma ya awali mpaka sasa.
  Alisema wale ambao bado wana risasi mwilini wamepatiwa dawa za kupunguza maumivu ili kusubiri uchunguzi zaidi juu ya risasi walizonazo mwilini kuona kama kuna uwezekano wa kuzitoa.
  Hata hivyo, bado hazijapatikana taarifa sahihi za waliojeruhiwa katika tukio hilo la Jumatano kufuatia kuwepo kwa majeruhi wengine wanaotibiwa katika hospitali binafsi za Seliani na AICC ambapo miongoni mwao ni askari polisi.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,711
  Trophy Points: 280
  Hivi suala la uwajibikaji hapa lipo wapi? Waziri Mambo ya Ndani, Mkuu wa Polisi na RPC Arusha ni vyema wakafukuzwa kazi..kwa kuanzia tu....................
   
 3. n

  niweze JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi CCM Wanataka Kusungumza Nini na Chadema? Meya wa Arusha Sio Discussion ni Aondoke na Kuhama Hio Nafasi, Alichaguliwa na Nani? Kikwete Aondoke Ikulu Kwani Alichaguliwa na Nani? Hakuna Majaridiliano Hapa na Kutaka Kugeuza Maneno Mnafikiri Hii Ndio Solution. Watanzania Hawawataki Tena Full Stop.
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,711
  Trophy Points: 280
  Kwa vipigo hivi kwa raia, Tanzania hakuna amani

  [​IMG]

  [​IMG] "MNYONGE mnyongeni haki yake mpeni" na "Usiache mbachao kwa msala upitao" ni semi zenye maana katika jamii.
  Waliotunga semi hizi za Kiswahili hakika hawakukosea.
  Nasema hawakukosea sababu ni semi zinazotumika kulingana na wakati na matukio yanayotokea katika jamii.
  Nikiwa kama mmoja wa wananchi wa kawaida katika nchi yetu ya Tanzania inayosifika kwa amani ndani na nje ya bara la Afrika si vibaya kama nikitumia mkono wangu kuandika kile kilichonisikitisha.
  Ninalotaka kulizungumzia hapa ni lile lililotokea Januari 5 mwaka huu mkoani Arusha.
  Kila mmoja anafahamu kuwa maandamano nikitendo cha kawaida kwa kila taasisi ama kundi la watu fulani kwa minajili ya kuhamasisha au kushinikiza utekelezaji wa jambo.
  Maandamano si dhambi na ndio maana ni moja kati ya taratibu zinazofuatwa kama njia mbadala ya wananchi ili kudai haki.
  Katika tukio lililotokea Arusha ambapo polisi walipambana vikali na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hadi kusababisha vifo vya watu watatu na wengine 16 kujeruliwa vibaya.
  Tukio hili limelitia doa taifa hili linalosifika kwa amani.
  Sasa amani ipi tunayojivunia Watanzania ikiwa jeshi tulilolikabidhi jukumu la kutulinda kutokana na wavamizi wa nchi linatugeuka na kutushambulia wananchi.
  Maandamano yaliyofanywa na CHADEMA hayakuwa maandamano ya kuvunja amani bali yalikuwa ni maandamano ya amani.
  Kwa mtazamo wangu polisi walitakiwa wasimamie maandamano hayo ili kuwalinda wafuasi wa chama hicho na kuangalia kama watafanya fujo, lakini si kuanza kuwapiga.
  Kitendo cha polisi kuzuia maandamano hayo kwa kutumia nguvu na silaha za moto walizo nazo, ni kitendo cha kinyama na uonevu.
  Ni dhahili kabisa jeshi linaendesha kazi zake kisiasa.
  Jeshi la polisi limeishaonyesha udhaifu mkubwa na kuifanya jamii kutokuwa na imani nalo tena, kwa kitendo cha kuvuruga amani ya wakazi wa Arusha na kutumia silaha zao kudhuru usalama wa raia.
  Polisi ni chombo kilichoaminiwa sana na raia kutokana na viapo walivyokula wafanyakazi wake (polisi).
  Kwa ujumla jamii haikutendewa haki kama raia, hatua iliyochukuliwa na polisi kuwapiga wananchi ni nzito kuliko kile walichokifanya.
  Kwa mujibu wa taarifa zilizoandikwa kwenye vyombo vya habari, polisi waliendelea na udhalilishaji kwa kuwapiga waandishi wa habari na kuwadhalilisha pamoja na kuwajeruhi vibaya.
  Pia waliharibu mali walizokuwa nazo waandishi wa habari kama vitendea kazi.
  Na hii si mara ya kwanza kwa polisi kufanya udhalilishaji kama huo, kwa vyovyote vile jeshi hili linajijengea uhusiano mbovu na wanahabari.
  Madaraka ya viongozi wa jeshi la polisi si kuamrisha majeshi dhidi ya wananchi bali kulinda haki za wananchi kama ni hivyo basi viongozi husika wa jeshi la polisi pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani Shamsi Vuai Nahodha wachukue hatua haraka iwezekanavyo ili kujisafisha katika uso wa taifa.
  Labda niwakumbushe polisi kuwa jukumu lao si kulinda maslahi ya watu wa aina fulani tu, kumbukeni na ninyi baada ya kuvua magwanda yenu mpo katika jamii hii hii mnayoilipua kwa mabomu ya machozi.
   
 5. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sasa CCM wanataka waongee nini na CDM wakati tatizo linaeleweka wazi ni uchaguzi haramu wa Meya, hapo hakuna cha mazungumzo, mazungumzo yafanyike baada ya uchaguzi kurudiwa. Ni kiasi cha serikali kutangaza uchaguzi urudiwe na wakishatangaza watuambie aliyevunja kanuni amechukuliwa hatua gani period. Huo ndio ustaarabu wa serikali zinazofanya kazi.
   
 6. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Haikubaliki serkali kuahidi meza ya mazungumzo badala ya kurekebisha makosa yaliyopelekea matatizo haya
   
 7. W

  We can JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wafukuzwe na nani? Mhhh!
   
 8. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Sio mbaya lipizo la damu ya wahanga hao ndo maziko ya CCM kaskazini.
   
 9. V

  Vancomycin Senior Member

  #9
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wazungumze nini wakati Makamba alishasema hawawezi kukaa meza moja na CDM baada ya ushauri wa Lowasa.Wasubiri wakati wanaandaliwa mashtaka ya kukiuka HAKI ZA BINADAMU.To hell you traitors.
   
 10. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Yaaani nawaonea sana huruma ccm hawana chao tena arusha....JK ndio ameua chama hiko alichokuwa anakigopa BWM kimemlalia JK....chama kimeishaa na ndio rais mwisho wa ccm....hakika kabisa....historia itaandikwa kuwa alitokea rais kiherehere akakumbatia watu wenye pesa....akatumia pesa nyingi sana kupata nafasi hiyo....akavurugaa kila msingi uliopoo na akaua chama na akavuruga amani....na kila kitu .......kiherehere chake kimeua nchi....uwezo mdogo na IQ ndogo..sana ila alilazimishia sana kuwa Pres hakujua anataka kulifanyia nn taifa. Yeye alitaka awe pres basii mengine yaende tuuu....kama hakuna pres siku ziende aandikwe historia...hakuna cha maana alichotaka kufanya ahazi lukuki zisizotekelezeka kwa muda mfupi na nchi changa kama hii na ufisadi alioukumbatia
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Jan 8, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Hicho ndicho tulichotegemea kusikia.
  Hakuna kukaa meza moja na Mafisadi, kujadili nini?
  Kwanza siku Nahodha anatoa tamko la kukaa Meza moja na CCM, siku hiyo hiyo Makamba naye alitoa tamko la kulaani CHADEMA.
  Sasa tunakalia nini?
   
 12. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #12
  Jan 8, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Wamefurahi kutupiga risasi na mabomu.. Waendelee kwanza ndipo sheria itakapochukua mkondo wake..

  Kama ni kukaa nao tuanzie kwenye urais kwanza ndipo tuendelee na mazungumzo..
   
 13. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #13
  Jan 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ni lini mawaziri wetu ataanza kuwajibika kwa uchafu unaofanywa na watu walio chini ya wizara zao??? Ama kweli waafrika akili zetu ni makamasi tu. Sasa chadema itakaaje meza moja na watumia makamasi badala ya ubongo!! Ni kupoteza muda tu.
   
 14. soine

  soine JF-Expert Member

  #14
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 391
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  Kiukweli inakera na kusikitisha kwa yaliyotokea Arusha. Je, serikali inayotaka mazungumzo na chadema inategemea lini kufanya mazungumzo na ndugu wa marehemu, walioachwa vilema, walioharibiwa na kupoteza mali zao juu ya fidia?
  Nafkr waafrika sio wajinga na akili zao hazijajaa kamasi kama mmoja wa wanaJF alivyosema kwani jirani zetu kenya wanafanya vema ktk siasa-kiongozi akfanya madudu anajiuzulu huku akiendelea kuchunguzwa. Labda angesema kuna viongozi malimbukeni walioshka madaraka na kuongoza watu kama familia zao.

  Mi nafkr Ocampo anene na hilo tukio la Arusha!
   
 15. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #15
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Kwa jinsi nilivyosoma hii habari, hakika sioni haja ya mazungumzo. na kumbe nimegundua serikali ilikuwa inaogopa mkutano huu kwa kuona utawaumbua, jamani democrasia ya kweli haiji kwa mbinu za kimafia za serikali ya ccm, tubadilke wakubwa. nashindwa kuendelea kwani machozi yananitoka kwa yanayotokea nchi hii
   
 16. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #16
  Jan 8, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  ''Nchi yangu Tanzania nakupenda kwa moyo wote'',nina hakika Kikwete hawezi kuuimba tena huu wimbo. Amepoteza muelekeo,amekosa dira na hafai kuwa kiongozi wa taifa huru la tanzania.Anasubiri siku ziende basi hakuna la ziada hana anachokifanya na amezungukwa na manunga yembe ambao hawawezi kumuambia mzee hii ni rangi ya njano siyo nyekundu kama ulivyosema.Wako kwaajili ya kumfurahisha wakati wanajua kwamba Rais wao ni bomu linalosubiria kulipuka. Tuzidi kuomba mungu ainusuru nchi yake na atunusuru watu wake!
   
 17. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #17
  Jan 8, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hakuna maana yoyote kuketi na wauwaji,ccm na serikali walipewa muda wa kutosha toka tarehe 21 dec wakapuuza leo hii baada ya mauaji ndo wanataka mazungumzo,they must be out of their mind,,,,ni saa ya ukombozi
   
 18. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #18
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ili mazungumzo yafanyike lazima pande zote katika tatizo zifahamu na kukiori kuwa kuna tatizo tena linalohitaji kushughulikiwa haraka.

  [​IMG]
  Nahodha amezungumza kama serikali na Makamba kama chama kinachohitajika kukaa meza moja na CHADEMA. Sasa kama katibu mkuu wa CCM ambae kimsingi ndie anaetakiwa kutoa muelekeo wa mazungumzo ya vyama hivi analaani CHADEMA, nani anatarajia kuna udhati wa mazungumzo hapo.

  GO to hell you booby CCM
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Jan 8, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hivi huyo meya anajisikiaje baada ya yote haya?
   
 20. GATS

  GATS JF-Expert Member

  #20
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 240
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Hayo mazungumzo wanayodai CCM ni danganya toto tu hakuna cha maana wanachoweza kufanya CCM zaidi ya kufanya ukandamizaji.
  Kumbukeni haki hutafutwa hata kwa kumwaga damu. Ila sasa ndio wanajimaliza kabisa. Maana wanazidi kuongeza msululu wa watu ambao hawatawapenda milele.
   
Loading...