CHADEMA yagawanyika, Lissu kukutana na Samia haikuwa ajenda ya chama

5525

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
5,412
6,273
Habarini watu wa ukumbi huu..,

Vyanzo vya ndani vinasema hivyo, Tundu Lissu alikutana na Rais Samia kwa matakwa na maamuzi yake binafsi haikuwa ajenda ya chama wala hawakuwahi kukaa ata kwa dakika 5 kupeana mashauri juu ya kukutana na rais Brussels.,

Lakini vyanzo vilienda mbali zaidi baada ya mmoja katika viongozi wao wakuu na alisema "pamoja na kwamba hatukua na Lobbing yoyote yeye kukutana na rais lakini Tundu Lissu hakuwa mtu mwenye kuvumilia kwa kile walichoongea na rais, baada ya kuachana na mama tu alienda kuandika walichoongea na mama jambo ambalo tunahisi limepelekea Mwenyekiti Mbowe kwenye ile kesi mambo kubadilika na kuonekana Mbowe ana kesi ya kujibu Ameendelea kusema mmoja wa viongozi wa juu kwamba ''Sisi tulikuwa na matumaini makubwa Mhe. Mbowe angekuwa huru na kutoka lakini haikuwa hivyo tunahisi ni kutokana na kiongozi wetu huyu kupenda kubwabwaja kila kitu hadharani" Akajenga suali "Kuna tofauti gani alichofanya Zitto ambaye tunamuimta msaliti na alichofanya yeye Lissu"

Akaendelea kutolea mfano "Mbona maalim seif alipoenda kukutana na magufuli hakuna aliyejua nini waliongea lakini hata maalim seif alipoulizwa alijibu ni siri ya wao wawili, maalim seif akaenda mbali zaidi mpaka kule Chato lakini maalim hakuwahi kwenda kwenye media kutangaza nini na nini waliongea na mwendazake lakini matokeo yake baadae walikuja kuona Zanzibar inaingia kwenye serikali ya Umoja wa kitafa"

Baada ya kuvuja kwa walichoongea Lissu na Mama, Yasemekana ndio kilichopelekea Mama alipoulizwa kuhusu Mbowe akajibu hawezi kuingilia Mahakama, anasema jibu hili lilitokana kwa kukurupuka kwa Tundu Lissu kubwabwaja kwa yale ambayo waliongea na rais.

Chanzo kimeeleza kwamba walitegemea mwenzao huyu Tundu Lissu baada ya kukutana na mama basi angekutana na wenzake kupitia angalau Zoom na kuzipeleka hizi ajenda kwenye kikao chao cha ndani na kuona kama kuna tija yoyote kwenye chama lakini Tundu hakuwa akifanya hivyo alifanya maamuzi ya kuweka wazi kwa umma.

Lakini pia kiongozi huyu ameenda mbali zaidi kuhusu katiba na akasema kwenye mkutano wetu wa ndani tulifanya mjadala wa kudai katiba mpya na mapendekezo yaliyotoka walipendekeza kwamba huenda mama kwa jinsi wanavyomuona anaweza kuleta Katiba mpya baadae hivyo wakata waendelee kuvumialia badala yake Chadema wadai Tume huru ya Uchaguzi lakini ni Tundu Lissu aliepinga wazo hili 100% na kusema wakati ni sasa wa kudai katiba mpya ndipo Mbowe alipojaribu kudai katiba mpya na matokeo yake ndio akashikwa hadi leo na kubambikiziwa hayo makesi, anasema ni matokeo na maamuzi ya Tundu Lissu lakini na msigwa kwenye jambo hili.

Naomba kuwasilisha.
 
Asante kwa taarifa!!

Ingawa ilijulikana toka mwanzo CCM chjni ya Magufuli na Makamu kwa wakati ule,, walitoa ahadi kuu juu ya kuwamaliza wapinzani na wakafanikiwa!!

Suala la Mbowe Ni matekelezo ya ahadi ile ,, Sasa kuhusu Lissu kuelezea nini kliongeleka kinahusiana nini na maamuzi ya Jaji!!?

Kama wamedhamilia kumnyeshea mvua ya kutosha ndugu Mbowe, Hata Rais Samia angekutana na Mungu live,, lazima Mbowe ale mvua ya kutosha
 
Lissu amekurupuka kweli aisee, kwenye haya maneno kuna logic sana Lissu kuna mambo anayabeba yeye mwenyewe binafsi akafanya ni agenda za chama, Mbowe ndio anaeteseka, Tundu ni kama vile amedandia treni kwa mbele itawacost sana Chadema
 
Hizo ngonjera zenu hazita wasaidia kitu hapo Lumumba. Lissu ni mtu mwenye Akili kubwa ndio maana mlihangaika na Risasi zenu Mungu akakataa.

Mlitaka asiseme kilicho jadiliwa ili muanze kuongopa uzushi kuwa eeh Lissu kanunuliwa, ooh kajipendekeza, ooh ameisaliti Chadema nyambafu.

Lissu kaweka hadharani kila kitu mnaanza kujinyea nyea tuu. Kwani Lissu ndiye aliye mkamata Mbowe na kumuweka ndani kwa kesi za michongo? Msimamo wa Chadema upo imara na hautatereka kuwapigia magoti watesi.
 
Kwamba hata kauri ya lema, katibu mkuu, hujasikia ulichoona ni kukurupuka na mada za ajabu, hapa sio facebook ,Kuna watu na akili zao, wafuatiliji wa Mambo,

Ukitoka hapa wajitapa hu undercover ,very shame
 
Hizo ngonjera zenu hazita wasaidia kitu hapo Lumumba. Lissu ni mtu mwenye Akili kubwa ndio maana mlihangaika na Risasi zenu Mungu akakataa.

Mlitaka asiseme kilicho jadiliwa ili muanze kuongopa uzushi kuwa eeh Lissu kanunuliwa, ooh kajipendekeza, ooh ameisaliti Chadema nyambafu.

Lissu kaweka hadharani kila kitu mnaanza kujinyea nyea tuu. Kwani Lissu ndiye aliye mkamata Mbowe na kumuweka ndani kwa kesi za michongo? Msimamo wa Chadema upo imara na hautatereka kuwapigia magoti watesi.
Mkuu ni wewe uliyeandika hivi?
Lissu amempigia mama magoti kule brussels wewe unaishi dunia ipi? embu cheki haka kapicha, angalia kwa makini jicho la tundu lissu lakini angalia kwa makini jicho la mama utagundua kitu
Tundu Lissu.jpg
 
Hivi kati ya Samia na Tundu Lisu nani bosi wa mwenziye ? I mean, yupi mwenye uwezo wa kukinukisha ziaidi klk mwingine kwa maana ni kama wanaogopana, kama unaweza kusoma body language utaona tu …
 
Lakini pia kiongozi huyu ameenda mbali zaidi kuhusu katiba na akasema kwenye mkutano wetu wa ndani tulifanya mjadala wa kudai katiba mpya na mapendekezo yaliyotoka walipendekeza kwamba huenda mama kwa jinsi wanavyomuona anaweza kuleta Katiba mpya baadae hivyo wakata waendelee kuvumialia badala yake Chadema wadai Tume huru ya Uchaguzi lakini ni Tundu Lissu aliepinga wazo hili 100% na kusema wakati ni sasa wa kudai katiba mpya ndipo Mbowe alipojaribu kudai katiba mpya na matokeo yake ndio akashikwa hadi leo na kubambikiziwa hayo makesi, anasema ni matokeo na maamuzi ya Tundu Lissu lakini na msigwa kwenye jambo hili.
Wa kijani mnajitahidi sana kubumba lakini haitawasaidia. CHADEMA ndio kuimarika na kung'ara. Kammuulize hata Ndugai huko mafichoni. Poleni
 
Ila watanzania mna roho mbaya. Yani Lissu kukutana na mama mmekasirika Sana.
 
Back
Top Bottom