CHADEMA yafungua kesi mahakama kuu kanda ya Mwanza dhidi ya polisi kuzuia Mikutano

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903


Kahama. Chadema kimesema leo kinatarajia kufungua kesi Mahakama Kuu kanda ya Mwanza dhidi ya Polisi, kupinga zuio la maandamano mikutano ya hadhara ya kisiasa.

Akizungumza mjini Kahama jana, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alisema mikutano ya hadhara ni haki ya kikatiba na hawatanyamaza inapozuiwa na mtu, au mamlaka yoyote.

“Tutapambana kwa njia na nguvu zote kulinda demokrasia nchini, hata kama itabidi kufia uwanjani. Ikibidi kwenda mahakamani kudai haki hiyo tutafanya hivyo.” alisema

Hata hivyo, Mbowe hakuwa tayari kuthibitisha taarifa za Chadema kufungua kesi jijini Mwanza, leo.

Mawakili wa Chadema akiwamo Peter Kibatala na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu walitarajiwa kuwasili Mwanza jana tayari kutoa ushauri wa kisheria na kufungua kesi.

=======

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, jana alifungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, kupinga amri ya polisi kuzuia mikutano ya vyama vya siasa nchini.
9.jpg

Kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2016, ilifunguliwa jana na kusimamiwa na mawakili watatu Gasper Mwanalyela, John Mallya na Paul Kipeja.

Licha ya kuwepo na ulinzi mkali wa jeshi la polisi uliowekwa katika barabara zote za kuelekea Mahakama Kuu, viongozi na wafuasi wa Chedema walifanikiwa kuvuka vizuizi hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka mahakamani jana jioni, Mbowe alisema sababu za kufunguliwa kwa kesi hiyo ni baada ya kuona demokrasia ya vyama vingi "inabakwa nchini."

Mbowe alisema watu wanne waliotajwa katika kesi hiyo ya madai ni Kamanda wa Polisi wilayani Geita, Kamanda wa Polisi wilayani Kahama, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa polisi (Makao Makuu) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Alisema wadaiwa hao wamefunguliwa kesi kutokana na kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa nchini, kwa kuchukua maamuzi ambayo hayaendani na demokrasia.

“Tunaiomba mahakama itangaze amri ya jeshi la polisi ya kuzuia mikutano ya vyama vya siasa ni batili, utekelezaji unaofanywa ni batili, polisi wapewe tangazo la kutowanyanyasa wapinzani na pia itoe amri ya vyama vya siasa kufanya mikutano yake na polisi wawe walinzi wa mikutano hiyo,” alisema Mbowe.

Alisema pamoja na polisi kuwabana hawataondoka jijini Mwanza, na wataongezeka zaidi mpaka kieleweke.

Alisema upo mkakati wa makusudi kuhakikisha Chadema inafutika katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kutokana na baadhi ya viongozi wake kutekwa na kunyanyaswa na polisi.

Mkutano huo na waandishi wa habari ulihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Saidi Issa Mohamed, Dk. Vincent Mashinji (Katibu Mkuu), Salum Mwalimu (Naibu Katibu Zanzibar), Halima Mdee (Mwenyekiti Bawacha) na Pastrobass Katambi (Mwenyekiti Bavicha) na baadhi ya wabunge wa chama hicho.

Kesi hiyo ya madai inatarajiwa kupangiwa Jaji Jumatatu ijayo.

Polisi ilisambaratisha mkutano wa Chadema uliokuwa ufanyike Kahama katikati ya wiki, ambapo mabomu ya machozi na magari ya 'washawasha' vilitumika kuondoa wafuasi wa chama hicho waliokuwa wasikilize hotuba za viongozi wa kitaifa.

Chadema imepanga kufanya mikutano nchi nzima kulaani inachodai uonevu unaofanywa dhidi ya wabunge wake Bungeni.

Chanzo: Mpekuzi
 
Asanteeee,baada ya hii miaka mitano au kumi mtaona Baba jesca akingangania kubaki madarakani,take it from me kiloriti.iko siku mtakuja niambia

Nimeliona hilo.Maana baada ya kutumbua majipu atajikuta hajafanya chochote nafuu ya aliyemtangulia.Kingine ninachofikiri kipindi hiki ch ausiri ndicho kitakuwa kipindi ambacho wizi mkubwa kupita yote utafanyika.
 
Bongoland+bongolala=ccm

Chama kinacholindwa kwa kutumia nguvu ya jeshi..
Inasikitisha sanaa .

Huenda tukarudi nyuma sana kiuchumi kuliko awamu zilizopita.. ok time will tell.. yetu macho
 
Kahama. Chadema kimesema leo kinatarajia kufungua kesi Mahakama Kuu kanda ya Mwanza dhidi ya Polisi, kupinga zuio la maandamano mikutano ya hadhara ya kisiasa.

Akizungumza mjini Kahama jana, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alisema mikutano ya hadhara ni haki ya kikatiba na hawatanyamaza inapozuiwa na mtu, au mamlaka yoyote.

“Tutapambana kwa njia na nguvu zote kulinda demokrasia nchini, hata kama itabidi kufia uwanjani. Ikibidi kwenda mahakamani kudai haki hiyo tutafanya hivyo.” alisema

Hata hivyo, Mbowe hakuwa tayari kuthibitisha taarifa za Chadema kufungua kesi jijini Mwanza, leo.

Mawakili wa Chadema akiwamo Peter Kibatala na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu walitarajiwa kuwasili Mwanza jana tayari kutoa ushauri wa kisheria na kufungua kesi.

hii culture ya kutumia mahakama nadhani itakuwa very relevant kuitumia chini ya utawala huu. ni njia pekee ya kuhakikisha kuna fairness.

embu angalia issue ya wale watoto wetu walioitwa "vilaza" - je, wanasheria wetu kweli hamuwezi kusaidia kwenye hili? maana mahala pengine kuna mtu alimwita mtu "bwege" na amehukumiwa jana tu hapa.
 
Wameondoka bungeni na kuwaachia posho yenu na uhuru wa kupitisha bajeti yenu mnavyotaka lakini bado mnataka kuzuia na mikutano halali ya kisiasa ambayo ipo kisheria na kikatiba huu sasa ni udikteta
cdm bungeni hamfiki asilimia 20. kulazimisha matakwa yenu tena kwa manufaa ya mafisadi si ndio udikteta. au ndio demokrasia yenu.
 
Ni kupoteza muda tu na rasilimali, unadhani hio kesi watashinda.Dola na mihimili yake unajua ni kitu kimoja afu matumain ya kushinda yatoke wapi sasa
 
wafungue tu kesi watashinda kama walivyoshinda kipindi cha MAITI YA MAWAZO
 
..remorsing a fallen politico hero on downway trending. Oh nawalilia wapinzani; ukawa na chadema. Kwa nini hamwezi kuelewa njia mpya ya siasa za Tanzania ya zama hizi! Bungeni kuna Tulia anawatisha, nanyi mnamkimbia. Huko Mahakamani pia kuna Jaji. Actually, had you used your freely gifted brain, it lesser facing a daunting Tulia than surrendering your powers to a single Judge. Eh.. Wake up men.
 
Hizo hela wanazohangaika kuandaa maandamano, kufungua kesi ,sisi wanachadema tunapendekeza wajenge ofisi za chama.


Ofisi ya chadema pale ufipa inatia kinyaa
 
Hizo hela wanazohangaika kuandaa maandamano, kufungua kesi ,sisi wanachadema tunapendekeza wajenge ofisi za chama.


Ofisi ya chadema pale ufipa inatia kinyaa

Hicho kinyaa itakuwa tayari kimekatikia wala usisingizie ofisi yetu
 
Hizo fedha mnazozitumia kuandaa mikutano na kwenda mahakamani mngekuwa mnawasaidia watu wenye shida mbalimbali hapa nchini tungewapongeza sana.
 
kwa mahakama zetu hakuna kipya, rejea hukumu ya mita 200, mgomo wa walimu
 
Back
Top Bottom