Elections 2010 CHADEMA yafungua kesi kupinga matokeo ya ubunge...........................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
CHADEMA yafungua kesi kupinga matokeo ya ubunge

na Stella Ibengwe, Shinyanga

amka2.gif
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Shinyanga kimefungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge yaliyofanyika Oktoba 31 mwaka huu ambayo yalimpa ushindi Steven Masele wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Katibu wa CHADEMA mkoani hapa, Shilungushela Nyangaki, jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa kesi hiyo ya nambari 5 ya mwaka 2010 ilifunguliwa Novemba 29 katika mahakama hiyo, kupinga ushindi wa aliyekuwa mgombea wa CCM ambaye kwa sasa ni mbunge.
Katika kesi hiyo wanaoshitakiwa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa jimbo hilo Festo Kangombe, Mwanasheria wa Serikali pamoja na Masele aliyekuwa akigombea nafasi hiyo kabla ya kuchaguliwa kuongoza jimbo hilo.
Habari zaidi zinaeleza kuwa kesi hiyo inatarajiwa kuanza kutajwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama Kuu ya Kanda ya Tabora Desemba 20 mwaka huu kwa kuhusisha washitakiwa wote wa watatu.
Shilungushela alisema mawakili watakaomtetea aliyekuwa mgombea wa CHADEMA Shelembi katika kesi hiyo ni Mabere Marando na Tundu Lisu, ambao ni wanasheria wa chama hicho na mawakili wa kujitegemea.
Hatua ya CHADEMA kwenda mahakamani imetokana na kutoridhishwa na mwenendo mzima wa zoezi la uchaguzi ambao ulisababisha vurugu hadi Ukumbi wa Manispaa ya Shinyanga kuchomwa moto na masanduku yote ya kura kuteketea huku polisi wakilazimika kufyatua mabomu ya machozi kuwasambaza waandamanaji.
Vurugu hizo zilitokea muda mfupi baada ya Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa jimbo hilo Kang’ombe ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga kutangaza matokeo yaliyompa ushindi Masele.
Kesi hiyo itakuwa ni ya pili kufunguliwa na CHADEMA dhidi ya wagombea wa CCM katika Jimbo la Shinyanga tangu kuanza mfumo wa vyama vingi mwaka 1995 baada ya ile ya mwaka 1995 ya kupinga matokeo ya mbunge wa CCM Leornad Derefa aliyembwaga mgombea wa CHADEMA, Bob Nyanga Makani, ambapo CCM ilishinda kesi hiyo katika Mahakama ya Rufaa.
 
If the way it was reported by Media is how it was, then CHADEMA has all the right to do so. Hope the justice will find its way back. GO CHADEMA
 
huko moshi vijijini vipi jamani, inasemekana chami kahonga chadema mkoa, asifunguliwe kesi ya wizi wa kura
 
Back
Top Bottom