CHADEMA yafungua kesi kupinga matokeo ya ubunge........................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yafungua kesi kupinga matokeo ya ubunge...........................

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Dec 1, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  CHADEMA yafungua kesi kupinga matokeo ya ubunge


  na Stella Ibengwe, Shinyanga


  [​IMG] CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Shinyanga kimefungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge yaliyofanyika Oktoba 31 mwaka huu ambayo yalimpa ushindi Steven Masele wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
  Katibu wa CHADEMA mkoani hapa, Shilungushela Nyangaki, jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa kesi hiyo ya nambari 5 ya mwaka 2010 ilifunguliwa Novemba 29 katika mahakama hiyo, kupinga ushindi wa aliyekuwa mgombea wa CCM ambaye kwa sasa ni mbunge.
  Katika kesi hiyo wanaoshitakiwa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa jimbo hilo Festo Kangombe, Mwanasheria wa Serikali pamoja na Masele aliyekuwa akigombea nafasi hiyo kabla ya kuchaguliwa kuongoza jimbo hilo.
  Habari zaidi zinaeleza kuwa kesi hiyo inatarajiwa kuanza kutajwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama Kuu ya Kanda ya Tabora Desemba 20 mwaka huu kwa kuhusisha washitakiwa wote wa watatu.
  Shilungushela alisema mawakili watakaomtetea aliyekuwa mgombea wa CHADEMA Shelembi katika kesi hiyo ni Mabere Marando na Tundu Lisu, ambao ni wanasheria wa chama hicho na mawakili wa kujitegemea.
  Hatua ya CHADEMA kwenda mahakamani imetokana na kutoridhishwa na mwenendo mzima wa zoezi la uchaguzi ambao ulisababisha vurugu hadi Ukumbi wa Manispaa ya Shinyanga kuchomwa moto na masanduku yote ya kura kuteketea huku polisi wakilazimika kufyatua mabomu ya machozi kuwasambaza waandamanaji.
  Vurugu hizo zilitokea muda mfupi baada ya Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa jimbo hilo KangÂ’ombe ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga kutangaza matokeo yaliyompa ushindi Masele.
  Kesi hiyo itakuwa ni ya pili kufunguliwa na CHADEMA dhidi ya wagombea wa CCM katika Jimbo la Shinyanga tangu kuanza mfumo wa vyama vingi mwaka 1995 baada ya ile ya mwaka 1995 ya kupinga matokeo ya mbunge wa CCM Leornad Derefa aliyembwaga mgombea wa CHADEMA, Bob Nyanga Makani, ambapo CCM ilishinda kesi hiyo katika Mahakama ya Rufaa.
   
 2. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  If the way it was reported by Media is how it was, then CHADEMA has all the right to do so. Hope the justice will find its way back. GO CHADEMA
   
 3. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  moto wa marando na tundu... patachimbika
   
 4. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Safi sana haki lazima itafutwe na itapatikana tu!
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  AlAFU NI KWA NINI KUFUNGUA KESI IWE 20MIL
   
 6. g

  gomezirichard Member

  #6
  Dec 3, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 71
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tutashinda bila shaka
   
 7. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  huko moshi vijijini vipi jamani, inasemekana chami kahonga chadema mkoa, asifunguliwe kesi ya wizi wa kura
   
 8. A

  ANDREW MBEGETE New Member

  #8
  Dec 6, 2010
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mahakama kuu kazi kwenu
   
Loading...