Chadema yafunga goli lingine

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Taarifa za wabunge wa chadema kutoka nje wakati rais wa Jamhuri alivyoanza kuhutubia, siku ile alipofungua bunge, zilisambaa kwa kasi dunia nzima kwasababu siku ile katika ukumbi wa mbunge kulikuwemo wawakilishi wengi kutoka nchi mbali mbali. Watu hao, waliojumuisha na waandishi wa habari walisaidia kufikisha habari hiyo huko walikokuwa wanatoka. Vivyo hivyo maandamano ya chadema ya leo, na matumizi ya nguvu yanayosemekana kuzidi kiwango, nayo pia yamesambaa haraka dunia nzima kwasababu leo hii inasemekana kulikuwepo watalii wengi mjini Arusha, walioshuhudia matukio hayo. Watalii hao, tayari wamekwisha tume taarifa hizo kwao, pamoja na picha za matukio hayo. Matukio hayo mawili yatakuwa yamekijengea umaarufu chadema katika medani ya siasa katika ngazi ya kimataifa.
 
Back
Top Bottom