CHADEMA yafanyiwa vurugu kubwa na CCM wilayani Meatu

Poleni sana mliojeruhiwa au kuumizwa na hao wahalifu, wauaji na mafisadi wa Genge la Kijani. MUNGU awaponye haraka ili mwendelee na maisha yenu pamoja na harakati za ukombozi wa nchi hii.

Tunajua Tanzania hakuna utawala wa sheria wala hakuna demokrasia. Sio polisi wala Tendwa watakao diriki kuchukua hatua za kisheria dhidi ya CCM na wanamgambo wao.

Naomba wana JF tuusome uzi huu mahiri na wenye kuendana na uhalisia wa mazingira tuliyona leo; hasa upande wa CHADEMA.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/325723-chadema-na-tanu-mfanano-na-tofauti.html
 
CCM ni chama cha Kikomunist, kama vilivyo vyama vya aina hii kina matawi yake ya kijeshi i.e. wanamgambo. Ingawa haitamkwi wazi wazi lakini ni uhalisia ulio uchi kama jua angani.

Ninalaani kwa nguvu zangu zote unyama huu waliofanyiwa wnaanchi wa Meatu na kundi la wanamgambo wa CCM. a
Pamoja na udhaifu mkubwa na wa wazi wa serikali ya Kikwete, lakini kwa vile sheria zipo basi tunataka uchunguzi kamili ufanyike na hatua kali na stahiki zichukuliwe dhidi ya wote waliohusika na utesaji huo.

Ni kweli udhaifu mkubwa wa serikali hii wa kufuata sheria za nchi ndio unaoifanya CCM iwe na jeuri hizi za kishetani. Lakini iwapo watajaribu kuendeleza choko choko za uonevu na uuaji dhidi ya wananchi huku wao wakidhani wanaiumiza/wanaithibiti CHADEMA basi nchi hii itaingia ktk machafuko ambayo kwa kila hali hayakuwa na sababu za kutokea.

Mara nyingi tu CHADEMA na hasa Dr. Slaa na Mh: Mbowe wameonesha uvumilivu wa hali ya juu sana pamoja na busara ili kuepusha kulipizana kisasi. CCM wasidhani hali itaendelea kubaki hivyo. Sote tunaipenda Tanzania. Sote tuwajibike kuilinda misingi ya umoja wa kitaifa na utulivu uliopo.
 
Macho yote sasa kwa John Tendwa; CCM hatarini sasa kufutwa kwa sheria ile ile waliotishiwa CHADEMA.
 
Tendwa amezeeka hawezi kwenda na kasi ya Mageuzi nchini. Anatakiwa abaki na kazi ya ushauri. Kazi nyingine aendelee kuwasimulia wajukuu zake jinsi alivyosaidia kuvuruga mfumo wa vyama vingi.
Tendwa hajitofautishi yeye na Katiba.

Hapo kwenye Bold, napata shida sana na huyu mtu na namna yake anavyo tafsiri mambo mbali mbali, akiwa mshauri huyu si ni balaa!
 
Nilitaka kumtukana tusi kubwa sana tendwa lakini nikakumbuka ban, then nmeacha. Ngoja niende fb nikamtukane weee hadia akome kuipendelea ccm.
 
Ivi mwenye CV yake ataondoka lini ofisini?? nikimuona napata kichefuchefu.

Mkuu mnafiki tendwa alichaguliwa na rais, haina kustaafu by statutory, ukumuonaga Luhanjo hadi alikuwa hawezi kuongea, lkn yumo tu. Labda JK amchoke....
 
Back
Top Bottom