Chadema Yafanya Kufuru, Yavuna Wanachama 31,337 Morogoro!

Hayo ndio maneno,safi sana.Lakini wana JF walioko morogoro hamkututendea haki,
hamkutupia picha humu JF tukaona ccm walivyoshikiwa chini.
 
Nafikiri mwandishi wa hili Gazeti la Tanzania Daima ni mshabiki tu.

Nafikiri anahitaji kujua Si wanachama wote wana utashi wa kupiga kura. Lakin vile vile Tanzania sio kosa kisharia mtu kuwa na Kadi za vyama vya siasa zaidi ya moja.
Na akumbuke kuwa sharia za Tanzania zinaruhusu hata mtu asie mwanachama wa chama chochote cha siasa kuweza kupiga kura kwenyye uchaguzi mkuu.

Cha muhimu ni kueneza ilmu ya Uraia kwa wananchi ili waone umuhimu wa kupiga kura na kuchagua kile wakitakacho.

Huo ni msaada wangu kwa mwandishi huyo ambaye ni mshabiki.
 
Sumu tena? wakati CCM tupo madarakani na nyinyi ndio wapinzani? kwi kwi kwi teh teh teh! Sijui huwa mnakuja na hangover?

wewe bado unalala, au unajitia ujinga tu, tutawaona after 2015 mtasema nini.
 
wewe bado unalala, au unajitia ujinga tu, tutawaona after 2015 mtasema nini.

Tulizana mpaka 2015, umuombe mungu wako akufikishe ushuhudie.

Kwanza mpate japo kiti kimoja cha ubunge visiwa vya Zanzibar.
 
Kwa sababu CCM imeandikiwa iitawale Tanzania milele toka kwenye vitabu vitakatifu vya MwenyeziMungu?????/

Hapana, sio sababu hiyo, CCM haitatawala milele na hakuna ataetawala dunia hii milele. Walishindwa kina Firauni na Caesar na Mapapa itakuwa CCM, lakini chadema bado ni chama hafifu na hakina muelekeo, waongo, hawana sera, siasa zao chafu, wasusaji, wachochezi na Watanzania walio wengi hawawakubali, hatuwezi kuwapa kura za kuwafanya muongoze nchi, nyie mbaki na porojo za upinzani tu.

Kama chadema itakuja itawale basi si ya kina Mbowe na Slaa na Lema, wako very low kimaadili na kiufahamu.
 
Kinachoshangaza kwangu ni baadhi ya watu humu wanajenga dhamira kwamba ccm itatawala milele, wanasahau kuwa wanachama wao wanazeeka, wengine ni marehemu na wachache ni wanavijiji wasiojitambua kwa hofu ya vita pindi wapinzani wakishinda madaraka. Unfinished business of CDM versus CCM continues till they get rid of by 2015
 
Hapana, sio sababu hiyo, CCM haitatawala milele na hakuna ataetawala dunia hii milele. Walishindwa kina Firauni na Caesar na Mapapa itakuwa CCM, lakini chadema bado ni chama hafifu na hakina muelekeo, waongo, hawana sera, siasa zao chafu, wasusaji, wachochezi na Watanzania walio wengi hawawakubali, hatuwezi kuwapa kura za kuwafanya muongoze nchi, nyie mbaki na porojo za upinzani tu.

Kama chadema itakuja itawale basi si ya kina Mbowe na Slaa na Lema, wako very low kimaadili na kiufahamu.

ahahahahaaa, CDM wachochezi!!! Hapo ndipo nina mashaka na uelewa wako! Umesema vyema lakini kwa maana ya Siasa ni, UCHOCHEZI! Hivyo basi CDM wanachochea fikra mpya vichwani mwa watu ili watu wakiwaelewa waing'oe serkali iliyopo madarakani! Sasa kosa lao ni nini hadi uwalaumu?! wakati ndio shughuli yao!
 
Tulizana mpaka 2015, umuombe mungu wako akufikishe ushuhudie.

Kwanza mpate japo kiti kimoja cha ubunge visiwa vya Zanzibar.

Wote tuombe uzima, mbona hali halisi inaonekana kabisa mkuu, hili vuguvugu joto lake wewe hulipati au ndo gamba linazuia, ccm huwa wanategema kuchakachua lakini next time itakuwa kazi maana tofauti itakuwa kubwa sana.
 
Hivi hali ipi? hiyo ya kujazana majobless kwenye mikutano? nyie jitahidini sana, lakini bado. Hamna uongozi, ngoja uone watakavyoanza kutoana macho kwa fedha huko, ndio utaniambia. Josephine kisha anza kumtumia mzee kukopa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom