CHADEMA yaendelea kujiimarisha Korogwe vijijini

FakeID

Member
Feb 29, 2016
89
96
908bd29173ef42e3eb19c1504258766a.jpg


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeanza ziara zake rasmi za kukutana na wanachama katika jimbo hilo kwa lengo la kukagua uhai wa chama, pamoja na kufanya tathmini ya uchaguzi wa mwaka Jana 2015. Ziara hiyo iliyoongozwa na viongozi wa jimbo pamoja na aliyekuwa mgombea wa ubunge mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA (EMMANUEL KIMEA) imeanza leo katika vijiji kata ya Kwashemshi na Kerenge na inatarajiwa kuendelea katika kata nyingine za jimbo hilo.

Katika Ziara hiyo pia msafara huo umeambatana na madiwani wa Chadema katika jimbo la Korogwe vijijini ili kutoa chachu kwa kata nyingine kuchagua viongozi wa Chadema kwani ndio ambao wanatekeleza mambo wanayoahidi.
 
Chadema kazi yenu ni kuwakusanya wazee kuwanunulia boha na mnazi halafu mnasema uhai wa chama huu ni usanii mtupu.
 
Watu wanajuta sana kuchagua CCM, wanashangaa maisha yanakuwa magumu kila kukicha, wanadai hawamuelewi mkuu hata kidogo
 
Hivi mbona Maji Marefu bado yupo?
Huyo mganga anamalizia muda wake, kachaguliwa na wananchi yeye anaenda kuwakilisha waganga wa kienyeji. Mbunge anayesema mafuta yapandishwe bei ili sukari ipunguzwe hawatakii mema wananchi wake.
 
Back
Top Bottom