Chadema yadai kesi za ufisadi zinajenga tabaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema yadai kesi za ufisadi zinajenga tabaka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Dec 7, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,610
  Likes Received: 82,194
  Trophy Points: 280
  Date::12/6/2008
  Chadema yadai kesi za ufisadi zinajenga tabaka
  Na Salim Said
  Mwananchi

  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeitaka serikali kuwafikisha mahakamni watuhumiwa wa ufisadi waliomo ndani ya serikali ya awamu ya nne ili kuondoa matabaka katika ushughulikiaji kashfa hizo.

  Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Vijana wa chama hicho, John Mnyika, wakati wa ufunguzi wa kongamano la siku mbili la kuwajengea uwezo vijana wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam linalofanyika kwa ubia baina ya chama hicho na Hoyre cha Norway.

  Mnyika aliwataka wananchi wasiweke matumaini makubwa kwamba serikali ya awamu ya nne ina nia madhubuti ya kushughulikia ufisadi wakati watuhumiwa waliomo mdani ya serikali bado wanaendelea kuvinjari katika mitaa.

  “Serikali ya Rais Jakaya Kikwete bado haijaonyesha nia ya kweli na dhamira madhubuti ya mapambano dhidi ya ufisadi nchini, kinachofanyika ni kujenga matabaka tu katika kushughulikia kesi hizo, kwa sababu wanashughulikiwa watuhumiwa wa serikali ya awamu ya tatu na kuachwa wa awamu ya nne,” alidai Mnyika na kuongeza.

  “Kama Basil Mramba na Daniel Yona wamefikishwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka yao, kwa nini wasifikishwe waliokuwa mawaziri wake ambao walijuzulu kwa kuwajibika kutokana na uzembe uliotokea kwenye nyadhifa zao?” alidai zaidi.


  Alifafanua kuwa, ufisadi unaoshughulikiwa na serikali hadi sasa ni robo tu ya ufisadi wa 1.3 trilioni ulioibuliwa na kambi ya upinzani katika sekta ya madini, mikataba mibovu na Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  “Hii ni robo tu ya sehemu ya ufisadi mkubwa wa 1.3 trilioni ulioibuliwa na kambi ya upinzani katika sekta za madini, mikataba mibovu na EPA ambapo pia tulitaja orodha ya watuhumiwa 11 wa wizi huo,” alisema Mnyika.

  Aliwaambia vijana waliohudhuria katika kongamano hilo kuwa, Dar es Salaam ndio kitovu cha Tanzania na kwamba mabadiliko katika nchi yoyote duniani huanzia katika miji kwa kuwa huko ndiko hukusanya watu kutoka sehemu mbalimbali.

  “Tunafanya semina hii katika mtaa huu wa Lumumba ambao zamani ulikuwa ukijulikana kwa jina la ‘The New Street’, hapa ndio ilipozaliwa TANU na baadaye kufanikiwa kumuondoa mkoloni wa kiengereza, basi na sisi kongamano hili liwe ndio chachu ya kumng’oa mkoloni mweusi CCM na viongozi wake madarakani,” alisema Mnyika.

  Alieleza kuwa, baada ya kunyakuwa madaraka kutoka kwa mkoloni, vizazi vya TANU na baadaye CCM vimegeuka kuwa mkoloni mweusi na kwamba hawapaswi tena kukaa madarakani.

  Aliwataka vijana hao kuyapa nguvu mabaraza ya vijana ya chama hicho na kuwa mabalozi wazuri wa vijana wenzao walioko vijijini kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya kweli ya kisiasa na kiuchumi nchini.

  Kongamano hilo limeanza jana na linatarajiwa kumalizika leo baada ya wakufunzi kutoka Norway na Tanzania kutoa mafunzo ya kuwawezesha vijana hao kisiasa.
   
 2. M

  Mutu JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kuna point nzuri humu !
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Dec 7, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Tuwe na Subra jamani subra!..
  Hizi ndizo nondo zenu Chadema Uchaguzi 2010.. mnachotakiwa kutafuta sasa hivi ni misumari tu, Ujenzi mtaufanya nyie!..
   
Loading...