CHADEMA Yabwagwa NA CCM KISUTU--DIWANI WAKI AVULIWA UDIWANI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA Yabwagwa NA CCM KISUTU--DIWANI WAKI AVULIWA UDIWANI

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kachanchabuseta, Nov 11, 2011.

 1. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  MATOKEO ya uchaguzi wa udiwani wa kata ya Kijitonyama, Kinondoni jijini Dar es Salaam yaliyomtangaza mgombea Uloleulole Athumani wa CHADEMA kuwa ni mshindi, yamebatilishwa na Mahakama ya Hakimu mkazi kisutu.

  Uamuzi huo umetolea leo Mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Genvitus Dudu katika kesi ya kupinga matokeo hayo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo.

  Dudu katika uamuzi wake alisema amesikiliza mashahidi wa pande zote mbili, mahakama imeona mdaiwa katika fomu ya
  kugombea nafasi hiyo, aliandika jina la Uloleulole Juma Athumani wakati kwenye hati ya kisheria lipo jina la Juma Uloleulole Athumani.Alisema mahakama hiyo imeona kwamba hao ni watu wawili, inakubaliana na Bulembo (mdai) kuwa kungekuwa na hati ya kiapo inayoonyesha mdaiwa alibadilisha jina lake.

  Alisema kutokana na kukosekana na hati hiyo, inatosha kumvua mdaiwa nafasi aliyokuwa nayo na pia katika hati ya kisheria anayotakiwa kutia saini mbele ya hakimu, mdaiwa imeweza kuleta mashaka kwa kuwa ina tarehe mbili tofauti.Alisema hati hiyo inaonesha mdaiwa alitia saini Agosti 14, mwaka 2010 na ya pili inaonesha hakimu alitia saini Agosti 18, mwaka 2010 mahakama inashindwa kuelewa kama kweli mdaiwa alitia saini mbele ya hakimu au la.

  Aidha Hakimu huyo alisema wananchi wananyimwa haki yao kutokana na kutotimiza matakwa ya kisheria hawakuweza kujua vigezo vya mgombea kutokana na kwenda kinyume cha Sheria ya Uchaguzi mahakama hiyo inaona uchaguzi wa udiwani wa kata ni batili.Kutokana na hayo, alisema maombi ya mdai yamefanikiwa kwamba matokeo ya uchaguzi yaliyomtangaza mdaiwa ni mshindi ni batili.

  Hata hivyo alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kumtangaza Bulembo kuwa ni mshindi na kusema uchaguzi urudiwe kwani mamlaka hayo yapo kwenye mamlaka nyingine.Bulembo alifungua kesi hiyo, akidai kutoridhishwa na matokeo hayo ya uchaguzi huku akiwa amewasilisha sababu sita.

  Katika sababu hizo aliiomba mahakama itamke matokeo batili, atangazwe yeye ndiyo diwani au kufanyike kwa uchaguzi wa
  wazi na huru.Hata hivyo mahakama ilisema pande zote mbili kama kuna ambaye hajaridhika na uamuzi huo anayo haki ya kukata rufani.
   
 2. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Haina mvuto!!!
   
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kha! Yeye ndio alitype majina yk au tume? Kinachotakiwa ni uchaguzi mpya si kumvua madaraka diwani wa cdm na kumvika hy guluguja wa ccm kwani ni dhahir kw ht wananch walimchagua wa cdm. Ht bungeni wanatamkaga ZUBERI ZITTO KABWE, ZITTO ZUBERI KABWE yt 2najua kw anayetajwa ni ZITTO KABWE.
   
 4. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #4
  Nov 11, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  huyu bulembo alilisha sana ubwabwa raia pale kwa mtogole. lakini mpaka mateja walienda kumpigia kura uloleulole... alikuwa na mvuto wa kisiasa kwa kweli!
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Nov 11, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  What a lose! Tatizo lingine la mahakama zetu. Hawaangalii matakwa ya wananchi. Watu wamepiga kura na kumchagua diwani wao. Ingekuwa majina yaliwachanganya wapiga kura na kusababisha kuvuruga uchaguzi, hapo ningekubaliana nao. Lakini kurudia uchaguzi kwasababu ya typing error ambayo haikuathiri uchaguzi ni ufinyu wa fikra na woga wa kutoa maamuzi hasa kwa mahakama zetu ambazo kwa sasa zinaingiliwa sana na wanasiasa wa chama tawala. Poor Tz. U have a very long way to go!
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  Nov 11, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,156
  Trophy Points: 280
  Maandiko ya kijinga namna hiyo ndio yanawakosesha haki, jaribu kuwa na nidham ya kuandika kwanza ndipo utapomuelewa Hakim kamaanisha nini. Kama wewe unashindwa kufata utaratibu wa kuandika uliofunzwa na Mwalim wako darasani ukaona kuandika utakavyo wewe ndio bora, ujuwe hayo ndio anayaongea Hakim "kutokana na kutotimiza matakwa ya kisheria", matakwa ya kisheria ni pamoja na namna ya kuandika karatasi za kutumia kisheria na mpaka "spacing na indent" hutumika zilizoainishwa kisheria, si kujiandikia tu utakavyo, msifikiri waliowawekea mitaala ya kuwafundisha namna ya kuandika walifanya makosa, wanajuwa huko mbele mtakumbana na nini.

  Wewe kwa jinsi ulivyoandika hufai hata kidogo kuitetea hii hoja hapa JF mliambiwa muwache kutumia namna hizo za maandishi, hamsikii.
   
 7. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #7
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huna jipya!!!!!
   
 8. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #8
  Nov 11, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,788
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Ukiwaona ditopile mzuzuri ilikuaje akapewa dhamana kesi ya mauaji?
   
 9. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #9
  Nov 11, 2011
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,044
  Likes Received: 383
  Trophy Points: 180
  We mdada upo makini sana katika kuandika. Lakini katika hili ni wazi maneno ya Mbowe kuwa Mhimili huu unainigiliwa ni kweli
   
 10. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #10
  Nov 11, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,675
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mimi naamini kuna tofauti kubwa sana kati ya sheria na busara. Ni kweli hajatimiza matakwa ya kisheria hilo liko wazi.
  Lakini tuwe wakweli, je hili kosa liliathiri vipi mchakato mzima wa upigaji kura? Pia nini hitaji la msingi la wapiga kura, ni mwakilishi wao au ni jina lake?
  Nio maana nimesema hapa haijatumika busara hasa kwa mlalamikaji. Huyu ni mtu anayeguswa na maeldeleo ya jamii yake kweli? Endapo utaitishwa uchaguzi mwingine, ni nani atagharamikia.

  Inavyooneka hoja ya mlalamikaji ni jina tu na tarehe za kula kiapo, sio vitu kama rushwa ambavyo vina influence kwa wapiga kura, vipi uchaguzi ukifanyika halafu watu wakamchagua yuleyule kwa kuwa wao wanahitaji kiongozi sio jina lake? Hatuoni kama haya ni matumizi mabaya ya fedha ya walipa kodi wenzake. Ama kweli siku hizi wanaotaka madaraka wapo kibinafsi zaidi kuliko wanavyotuaminisha. Mambo mengine aibu kweli.
   
 11. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #11
  Nov 11, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  haya kama mmeshinda fanyeni mabadiliko sio tu mnalidhika kwa kwenda mahakamani..
   
 12. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #12
  Nov 11, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hongera kwa kuitoa cdm
   
 13. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #13
  Nov 11, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  nyege mbaya sana!
   
 14. siemens c25

  siemens c25 Senior Member

  #14
  Nov 11, 2011
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 198
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Me sioni kama jina ni tatizo ila naamini kwajinsi ulole anavyokubarika ata burembo atoe gari kwa kila mtu wa kata ya k*nyama awezi kushinda namjua bulembo
   
 15. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #15
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  mahakama mbovu na ujinga wa mahakimu
   
 16. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #16
  Nov 11, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  MUWACHE NI Kihindi au kichina? YN MM NINGEKUA WW NINGEACHA KIHEREHERE CHA KUJIDAI NAJUA. we hujui na hujui km hujui hvy ww ni mpu.mbavu.
   
 17. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #17
  Nov 11, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,156
  Trophy Points: 280
  Mie niite upendavyo wala hunishtuwi ndio kwanza unanipa hamasa ya kuendelea kuwapa darsa watu kama wewe. Naona darsa limekuingia, laiti lingekuwa halijakuingia usinge ng'aka. Kuhusu hayo maneno yako yaki sms, ni utawala wa JF ambao walitangaza hawayataki. Ukiendelea wanakuona humu, watakulamba ban halafu useme oohhh sijaambiwa. Ohhhooo shauri lako.
   
 18. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #18
  Nov 11, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  sasa darsa ndio nini? Vibibi vingine bwana! Ndo nyie 20 years post menopause lakini bado mnavaa vimini,aafu mnalalama eti mabinti wa siku hizi wanavaa vibaya!
   
 19. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #19
  Nov 11, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,156
  Trophy Points: 280
  Darsa ndio darsa, na nnadhani hata nawe umefaidika, hivi bado wanavaa? siye huko hatuko kabisa, siye tuko kwenye stara. Tunajistiri.
   
Loading...