Chadema yaanza tena kuvurumisha Makongamano ya Katiba Mpya, Magu na Tunduma hapatoshi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,549
217,825
Hii ndio taarifa mpya kwa leo , Kwamba sasa ni Rasmi CHADEMA imefungulia upya Makongamano ya kuelimisha wananchi Kuhusu Umuhimu wa Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi , leo ilikuwa Zamu ya Tunduma na Magu .

Kaa tayari kwa Ratiba kamili pamoja na Majina ya Watu Wazito watakaotoa mada .

UVUMILIVU UNA MWISHO .

FB_IMG_1619042485662.jpg
 
Chadema ndio ilianzisha mwendo,wale wasiojiamini ndio wametoka amfichoni nao sasa wanasema katiba muhimu,sasa wakomalieni kwamba sio tu ni muhumi ila ni 'sasa',ile kamati ya kichawi unayotaka tuanze sijui na tume halafu baada ya 2025 ndio tupate kabisa ikafie mbele
 
Hivi haya makongamano ya ndani mpaka lini? mbona kama Chadema wamekubali kutii uvunjifu wa sheria unaofanywa na CCM na serikali yake?

Waitishe mikutano ya hadhara sasa tuanze kuiona sehemu tofauti za nchi yetu, hiki kifungo cha "mikutano ya ndani" sasa kinatosha.
 
Anzisha ya Nje 😁😁
 
Kazi ya chadema ni ni Chama cha Matamko.

Hivi ile join the Chain sijui na Chadema Digital sijui na nini na nanihii ziliishia wapi?
 
Back
Top Bottom