Elections 2010 CHADEMA Yaanza Kuwanoa Wagombea Ubunge

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864


Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kinatarajia kuanza Mafunzo kwa Wagombea Ubunge Watarajiwa. Mafunzo hayo yanalenga kutoa Mafunzo muhimu kwa Wagombea hao ambayo yatakwenda sambamba na mafunzo kwa Makatibu wote wa Majimbo, Wilaya na Mikoa. Mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika kwa Mfumo wa Kanda kama ifuatavyo;

Kanda ya Kati- Dodoma,Morogoro na Singida ambapo Kituo cha Mafunzo kitakuwa Dodoma. Mafunzo yatafanyika tarehe 1-2 Juni 2010.

Kanda ya Magharibi – Tabora,Kigoma,Shinyanga na Rukwa ambapo Kituo cha mafunzo kitafanyika Tabora.Mafunzo yatafanyika tarehe 1-2 Juni 2010.

Kanda ya Ziwa- Mwanza,Mara na Kagera- ambapo Kituo cha mafunzo kitafanyika Mwanza.Mafunzo yatafanyika tarehe 5-6 Juni 2010.

Kanda ya Kaskazini- Arusha,Manyara na Kilimanjaro ambapo Kituo kitakuwa ni Arusha.Mafunzo yatafanyika tarehe 5-6 Juni 2010.

Kanda zilizobaki Ratiba itatangazwa baadaye baada ya Mafunzo haya.

Wale wote wanaotarajia kugombea na bado hawajaza fomu za chama,mnashauriwa kujaza fomu hizo mapema iwezekanavyo.Fomu zinapatikana kwenye ofisi zote za Mikao,Wilaya na Makao Makuu au tembelea website ya chama; www.chadema.or.tz

Wagombea warajigharamia nauli lakini Chakula na Malazi vitagharamiwa na chama.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na

Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo -Bw Benson Kigaila 0787 383167, Afisa Mafunzo- Bi Regia Mtema- 0713 760534 au barua pepe regia@chadema.or.tz au John Mnyika 0784 222222, 0754 694553 au barua pepe mnyika@chadema.or.tz.


 
Mtu akikushawishi uichague chadema sema baabaa aaapeeeendiii!
Ila akikwambia mchague John Mnyika sema hapo ndipo peenyeewee
 
Mtu akikushawishi uichague chadema sema baabaa aaapeeeendiii!
Ila akikwambia mchague John Mnyika sema hapo ndipo peenyeewee

Naomba niongeze na Dk Slaa, Zitto, Tindu Lissu, na Dr Kitila kama kama atajitokeza.
 
Tuwahamasishe wapigaji vijana kugombea kupitia CHADEMA, kwani tumeona mchango wa wabunge wa chadema pamoja na uchache wao. Kwa hiyo tusisite kuwahamasisha kugombea kupitia chadema. CHADEMA ni chama cha kuungwa mkono katika harakati ya kuleta mabadiliko TANZANIA.

Mimi nawaunga mkono, wewe unasubiri nini?
 
Back
Top Bottom