CHADEMA yaandaa semina maalum kwa viongozi wote wa Mikoa...

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kimeandaa semina maalum kwa wenyeviti na makatibu wote wa mikoa nchini.

Lengo la Semina hiyo ni kuwajengea uwezo wa kusimamia operesheni M4C katika mikoa yao. CDM kimeamua kupeleka operesheni ya M4C kuanzia ngazi ya shina. Chama kimeamua kupeleka operesheni hii kwa wananchi wenyewe na itasimamiwa na viongozi wa maeneo husika.

Semina hiyo itafanyika kwa siku mbili November 22 na 23 huko Karagwe mkoani Kagera.

Source: Clouds TV/ITV

------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
More Updates from Tanzania Daima....

Wakati CCM ikianza ziara mikoani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeanza kujiimarisha kwa kuendesha mafunzo ya darasani na vitendo, kwa lengo la kuwajengea uwezo wenyeviti na makatibu wa mikoa 32 ya kichama.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni wa CHADEMA, Benson Kigaila, alisema kuwa mafunzo hayo yatafanyika Novemba 22 hadi 23, mwaka huu, wilayani Karagwe, mkoa wa Kagera.
Kigaila alisema baada ya mafunzo hayo wataingia kwenye vitendo ambapo makatibu na wenyeviti hao watasambaa kushambulia vitongoji na vijiji vyote vya wilaya ya Karagwe, kwa kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo hayo.
Alibainisha kuwa mafunzo hayo ya vitendo ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya ujenzi na uimarishaji wa chama, hususan operesheni ya M4C ambayo imesaidia viongozi kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya ndani na hadhara.
Kuhusu M4C, Kagaila alisema wakati viongozi hao waliopata mafunzo wakiendelea, chama kitatoa ratiba ya operesheni hiyo kubwa itakayoendelea kufanyika kwa nchi nzima.
 
Naona Chadema wanapita njia zile zile wanazopita CCM mambo ya semina ni matumizi mabovu ya ruzuku kulipana posho ambazo ni kodi zetu...inaingia akilini watu wanatoka mikoani waende Karagwe Kagera, kwa nini wasifanyie Makao Makuu Dar es Salaam.
 
Mkuu vipi mmetatua utata wa Uraia wa Katibu mkuu wenu?
 
Naona Chadema wanapita njia zile zile wanazopita CCM mambo ya semina ni matumizi mabovu ya ruzuku kulipana posho ambazo ni kodi zetu...inaingia akilini watu wanatoka mikoani waende Karagwe Kagera, kwa nini wasifanyie Makao Makuu Dar es Salaam.

Kimwili CCM, kiroho CDM.......wewe pa1 na mwenyekiti wako, mnashindwa kabisa kujizuia.mtajibeba mwaka huu
Mwambie TUNTE aje na cooked figures juu ya bajeti ya semina hii
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kimeandaa semina maalum kwa wenyeviti na makatibu wote wa mikoa nchini.

Lengo la Semina hiyo ni kuwajengea uwezo wa kusimamia operesheni M4C katika mikoa yao. CDM kimeamua kupeleka operesheni ya M4C kuanzia ngazi ya shina. Chama kimeamua kupeleka operesheni hii kwa wananchi wenyewe na itasimamiwa na viongozi wa maeneo husika.

Semina hiyo itafanyika kwa siku mbili November 22 na 23 huko Karagwe mkoani Kagera.

Source: Clouds TV

So wenyeviti na makatibu mikoa yote watenda kwenye simina Karagwe itakuwa njema.
 
Mmmmmmmmhhhhhhhh sijaelewa........... If not a joke then it has to be discussed further
Mbona Taarifa ya habari hii imepewa coverage kubwa tu leo na Tv Station wakati taarifa za habari za usiku? Ni Benson Kigaira ndiye aliyetangaza.
 
Naona Chadema wanapita njia zile zile wanazopita CCM mambo ya semina ni matumizi mabovu ya ruzuku kulipana posho ambazo ni kodi zetu...inaingia akilini watu wanatoka mikoani waende Karagwe Kagera, kwa nini wasifanyie Makao Makuu Dar es Salaam.
kwa hiyo nani afadhali cdm ama ccm katika hili?
 
Sasa inabidi wahakikishe wakimaliza mkutano huko..wasambaratishe ccm kabla ya kurudi makwao....sio trip ya bure tu...lazima hao ccm waondolewe
 
Litz akili yako haina AKILI, ni mafilifili matupu. Wewe ni against na kila kifanywacho na CDM. Hupendi? Kufa basi tukuzike.
 
Kimwili CCM, kiroho CDM.......wewe pa1 na mwenyekiti wako, mnashindwa kabisa kujizuia.mtajibeba mwaka huu
Mwambie TUNTE aje na cooked figures juu ya bajeti ya semina hii

Na lazima atapetape vibaya huku sisi tukisonga....
 
Back
Top Bottom