CHADEMA yaandaa semina maalum kwa viongozi wote wa Mikoa...

Naona Chadema wanapita njia zile zile wanazopita CCM mambo ya semina ni matumizi mabovu ya ruzuku kulipana posho ambazo ni kodi zetu...inaingia akilini watu wanatoka mikoani waende Karagwe Kagera, kwa nini wasifanyie Makao Makuu Dar es Salaam.
Acha unafiki, aliyekwambia wanaenda kulipwa ruzuku na serikali ni nani?
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kimeandaa semina maalum kwa wenyeviti na makatibu wote wa mikoa nchini.

Lengo la Semina hiyo ni kuwajengea uwezo wa kusimamia operesheni M4C katika mikoa yao. CDM kimeamua kupeleka operesheni ya M4C kuanzia ngazi ya shina. Chama kimeamua kupeleka operesheni hii kwa wananchi wenyewe na itasimamiwa na viongozi wa maeneo husika.

Semina hiyo itafanyika kwa siku mbili November 22 na 23 huko Karagwe mkoani Kagera.

Source: Clouds TV/ITV

------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
More Updates from Tanzania Daima....


Wakati CCM ikianza ziara mikoani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeanza kujiimarisha kwa kuendesha mafunzo ya darasani na vitendo, kwa lengo la kuwajengea uwezo wenyeviti na makatibu wa mikoa 32 ya kichama.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni wa CHADEMA, Benson Kigaila, alisema kuwa mafunzo hayo yatafanyika Novemba 22 hadi 23, mwaka huu, wilayani Karagwe, mkoa wa Kagera.
Kigaila alisema baada ya mafunzo hayo wataingia kwenye vitendo ambapo makatibu na wenyeviti hao watasambaa kushambulia vitongoji na vijiji vyote vya wilaya ya Karagwe, kwa kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo hayo.
Alibainisha kuwa mafunzo hayo ya vitendo ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya ujenzi na uimarishaji wa chama, hususan operesheni ya M4C ambayo imesaidia viongozi kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya ndani na hadhara.
Kuhusu M4C, Kagaila alisema wakati viongozi hao waliopata mafunzo wakiendelea, chama kitatoa ratiba ya operesheni hiyo kubwa itakayoendelea kufanyika kwa nchi nzima.

Updates zingine unabidi ucheke tu...
 
Back
Top Bottom