CHADEMA yaandaa mkakati mzito kudai Katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yaandaa mkakati mzito kudai Katiba mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Facts1, Dec 14, 2010.

 1. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa kitawasha moto wa madai ya kutaka Katiba mpya itakayokidhi matakwa ya wote.

  Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano katika mahojiano maalum, Dk. Slaa alisema mabadiliko ya Katiba wakati huu ni ya lazima na kwamba chama chake kimejipanga kuuelimisha umma kudai mabadiliko hayo.

  Dk. Slaa ambaye alikuwa mgombea urais wa CHADEMA na kutoa upinzani mkali kwa mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, na kuambulia ushindi mwembamba, alisema hivi sasa chama chake kinaweka mikakati ya harakati hizo kwa kuwashirikisha wataalam wake wa ndani na nje ya chama.

  "CHADEMA ni chama makini, si chama kinachofanya mambo kwa kukurupuka. Tunaandaa mkakati wa mwaka 2011-2015. Ifikapo Januari mwakani, tutapeleka mkakati huo kwenye vikao vya bodi, Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Baraza Kuu baada ya hapo tutaenda kwa wananchi na kuwasha moto nchi nzima kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kudai Katiba mpya," alisema Dk. Slaa.

  Kwa mujibu wa Dk. Slaa, CHADEMA inatambua kuwa suala la mabadiliko ya Katiba ni kilio cha Watanzania wengi, hivyo iko tayari kushirikiana na vyama, taasisi na watu binafsi ili kuhakikisha Tanzania inapata Katiba mpya.

  Wakati wa mikutano yake ya kampeni, Dk. Slaa katika mambo 15 ya vipaumbele vyake, aliahidi kufanya mabadiliko makubwa ya Katiba ndani ya siku 100 za kwanza endapo chama chake kingeingia madarakani.

  Alikuwa akitoa ahadi hiyo kila mahali alipofika kuomba kura za kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

  Kasi ya CHADEMA kutaka mabadiliko ya Katiba, imechagizwa zaidi na matokeo ya uchaguzi mkuu ambapo mgombea wake, Dk. Slaa anaamini kushindwa kwake kumetokana na mfumo mbovu wa vyombo vinavyosimamia uchaguzi yaani Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), inayodaiwa kukibeba chama tawala.

  Kuhusu kumtabua au kutomtambua Rais Kikwete, Dk. Slaa alisema Kamati Kuu ilipokea taarifa ya matokea ya urais; akayajadili na kukubaliana kuwa matokeo yaliyompa ushindi Rais Kikwete yalichakachuliwa kutokana na mfumo mbovu wa Katiba.

  Alisema kutokana na sababu hizo, CHADEMA imependekeza kuundwa kwa kamati huru itakayochunguza matokeo hayo na kutoa taarifa itakayolenga kuweka wazi juu ya kila kitu kilichojiri kwa manufaa ya taifa.

  "Ushahidi wa matokeo kutoka katika vituo kutofautiana na yale ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi; karatasi za matokea kufutwa ni vielelezo tosha kuwa matokea hayo yalichezewa,"alisema Dk. Slaa.

  "Kisheria Tanzania ina Rais na sisi CHADEMA tunasema nchi hii ina Rais, lakini njia iliyotumika kumpata Rais huyo si halali na hilo ndilo lililosababisha wabunge wa CHADEMA kutoka nje siku ya ufunguzi wa Mkutano wa Bunge," alisema Dk. Slaa.

  Wakati kasi ya kutaka mabadiliko ya Katiba ikiwa juu, Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani, alitoa kauli iliyoibua mjadala kuwa serikali haiwezi kufanya mabadiliko hayo kwa madai kuwa haina fedha.

  Hata hivyo kauli hiyo ilipingwa na wengi wakiwemo baadhi ya majaji na viongozi waandamizi wastaafu. Moja wa majaji hao ni Amir Manento na Jaji Mkuu Augustine Ramadhan; lakini pia Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Waziri Mkuu wake, Frederic Sumaye, viongozi wa dini, wasomi na wanazuoni mbalimbali, wanaharakati, na wengineo wengi wanaunga mkono hoja ya kuandikwa Katiba mpya.
   
 2. oba

  oba JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  That is a great news
   
 3. N

  Nonda JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  mkuu,

  Katika Tanzania hii ambayo,wanaoongozwa ni kama kondoo itakuwa ni maajabu ya dunia Kupatikana katiba mpya. Sitaki kumvunja mtu yeyote moyo ila kwa kutegemea chama kimoja tu cha upinzani kuwa kitakuwa na sauti, ushawishi au nguvu ya kuleta katiba mpya itabaki kuwa ni ndoto.


  Vyama vya upinzani vilifikia kuandika rasimu ya Katiba mpya au tumeshasahau leo?..Kama vyama vilishirikiana kwa hili na wakashindwa kwa umoja wao kuhamasisha wananchi, wanachama wao, vyama vya wafanyakazi na asasi za kiraia kwa pamoja kuipa msukumo hii hoja, leo kwa ubavu gani walionao mmoja mmoja?


  Tusijidanganye, kama wako serious. Vyama vyote vya upinzani wanataka katiba mpya, hata hao wanaoitwa CCM-B, C, D katika hili wanakubaliana.


  Hata hao majaji wastaafu , Kisanga,Bomani, Warioba, na hao maprof,wanaosema kwenye vyombo vya habari tu kuwa tuipate katiba mpya ni domo tu.

  Wanajuwa kuwa watanzania wamelala usingizi wa pono, lenda linawatoka, ilikuwa wawaambie waziwazi kuwa katiba mpya katika nchi kama yetu ambayo watawala hawaambiliki wananchi wanatakiwa wafanye ,a,b,c. Wao wanaimba kama kasuku, ya,ya,Katiba mpya , Unajuwa ohh sasa inahitajika katiba mpya.


  Mimi naona wangekwenda hatua moja mbele kuwaambia wananchi kuwa bila ya Katiba mpya na kwa maana hiyo sheria zinazoweka a level playing field kwa vyama vyote, Tume huru, na pale tume inapofanya makosa katika kutoa matokea basi yawe challenged mahakamani hata yale ya urais, basi hakuna maana ya kufanya uchaguzi Mkuu.


  Watowe rai kuwa ususiwe..


  Lakini kila jua linachomoza asubuhi watakuja ,,ohhh, katiba mpya…unajua tupate katiba Mpya… Tutaipata vipi? Njia gani za amani zitumike kuipata hii Katiba mpya? na kama kwa amani haipatikani what is the alternative? wao wanamuogopa nani?


  Kwao itakuwa wanaitumia platform ya kuaminiwa na jamii kwa hiyo sauti zao zitakuwa tamu masikioni mwa wananchi.Ushauri wao utapewa kipaumbele..

  Kueleza haya watakuwa kwanza wanawaamsha wananchi waliolala lakini pia itakuwa wanawapa tahadhari wanaongoza nchi kuwa mukijifanya kichwa ngumu kuwa wanaiingiza nchi katika hali tete na pengine yatazuka machafuko.


  Nonda akizungumza kama Nonda bado hana sauti lakini Watu hawa wanaozungumza sasa hawatutendei haki kwa kusema tunahitaji katiba mpya bila ya kueleza vipi tutaipata katiba hiyo au vipi wananchi waidai.

  Kama hawawezi kuwa jasiri kwa hili ,they better shut up!
   
 4. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Steer up Dr. Slaa
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hii ni kupoteza muda na kutokuwa na mawazo endelevu, una dai katiba mpya wakati hilo ni jambo wala si kudai?

  Katiba mpya, kwa sasa, inawezekana. Kwani hata CCM wanatambuwa kuwa katiba ya zamani imepitwa na wakati. Na pindi hoja rasmi itapopelekwa Bungeni hakuna ataeipinga.

  Naona Chadema wamekosa ubunifu wa kisiasa na wanaona kudai katiba mpya ndio turufu iliyobaki. Nawasikitikia sana, hebu tazameni namna ya kujipanga Bungeni na kuwasilisha hoja zenye tija na si za kupoteza wakati.

  Hili la katiba mpya halina pingamizi na ni mtego mkubwa kwa Chadema, ikiwa hawauoni basi nawasikitikia sana.

  Haya nyie endeleeni na mambo ya kuiga. Tanzania na Kenya ni tofauti. Huko Kenya kwenye hiyo katiba mpya na yenyewe imeshaanza kulalamikiwa na wanataka ifanyiwe marekebisho.

  Katiba si msahafu unaweza ibadilisha wakati wowote. Msitake kudanganya wananchi kuwa serikali imekataa hilo.

  Nani aliesema isibadilishwe? Sijamsikiapo CCM wala Serikali kulikataa hili la katiba mpya, na wengi wa Vigogo wa CCM wanalishabikia kama si wote.
   
 6. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Dar Es Esalaam
  usiwe nunda mwenye masikio asiye sikia,
  usiwe mbumbumbu mwenye anayeona ila akili hana,
  Inamaana hujaskia nini kasema waziri wako katiba na sheria??
  "Katiba ni jambo maana yake nini sasa, Uswahili wa maneromango haueleweki"
  Mabadiliko ya katiba ndiyo CDM inapoanzia maana yote tuliyaona juzi ktk uchaguzi chanzo ni katiba.
  Kinachoisumbua Ivory Coast kuwa na marais wawili, chanzo ni katiba mbovu,unatetea nini, unasimama kumtetea nani?:A S-omg:
   
 7. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  mkuu Dsm uko bongo? Serikali kupitia Selina Kombani ilisema katiba mpya ni ndoto kwani hamna fedha. Ina maana sirikali imegoma,mkuu wa nchi hadi leo yuko kimya. Majaji na wastaafu wetu wanaongelea vichochoroni,nani amfunge paka kengele? Kama cdm wamewekewa mtego basi wamejitega wenyewe maana walituhaidi katiba mpya tangu august 2010. Katiba ndo kila kitu.
   
 8. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  (hapo kwenye red)

  Hakuna kitu CCM wanaogopa kama kusikia hayo maneno.

  Forever Chadema.
   
 9. semango

  semango JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  acha kuongea kama mlevi.Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani alivyosema serikali haina pesa ya kubadilishia katiba alikua anamaana gani?yeye sio serikali?na yeye sio CCM?.........think critically before criticising mchakato unaopangwa.sio lazima mpaka uambiwe majani ni ya kijana ndio uelewe wakati unayaona kabisa rangi yake
   
 10. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #10
  Dec 15, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,533
  Trophy Points: 280
  Mnabishana na Malaria Sugu a.k.a Dar es Salaam a.k.a Jeykei a.k.a JeyKeiWaUkweli,mtaambulia upupu tu. Mpotezeeni huyo. Anyway bravo to CHADEMA kwa kuanza kujipanga katika mpambano wa kutaka katiba mpya. Ni vyema pia chama kikiwashirikisha wanachama na wapenzi katika mikakati yao ili madai haya yawe na nguvu ya umma. Asante.
   
 11. K

  Kabaya Member

  #11
  Dec 15, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja.
   
 12. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #12
  Dec 15, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hivi wewe ni wa jinsia gani?kwa sababu ninayo dawa ya kuzimua akili yako ila mpaka nijue wewe ni jike au?ili nijue hiyo dawa nipitishe wapi?
   
 13. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #13
  Dec 15, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mod mpuuzi huyu bado yupo, please modify your ban
   
 14. kmwemtsi

  kmwemtsi Senior Member

  #14
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  naunga mkono hoja kwa asilimia mia
   
 15. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #15
  Dec 15, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Jamani huyu mgonjwa akili ametoka wapi tena!!
   
 16. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #16
  Dec 15, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,586
  Likes Received: 2,972
  Trophy Points: 280
  Dar Es Salaam, una macho lakini ni kipofu na una masikio lakini hayafanyi kazi. Msemaje mkuu wa mambo ya sheria na katiba ni waziri Celina Kombani. Hivi alivyotamka kuwa hakuna haja ya kuandika katiba mpya na wala serikali haina pesa ya kufanya kazi hiyo, na kuwa hayo si matakwa ya watanzania bali akina Tundu Lisu na CHADEMA, hukusikia wala macho yako hayakuweza kuona TV au magazeti? Ama kweli kwenye JF tuna kazi ya ziada maana kuna adjuments nyingine zinazotolewa unafikia kujiuliza humu tuna watu wa namna gani maana kwa vyovyote wengine hawastahili hata kuitwa thinkers achilia mbali great thinkers.
   
 17. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #17
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hili suala si la CHADEMA ni la wananchi, sasa nashangaa hapa mnasema hongera CHADEMA. CHADEMA sio watu makini kama sie tunataka kuwapa jukumu la kutuongoza kudai katiba mpya mwisho wa siku tutapata 'bora katiba' na sio ' katiba bora', hawa jamaa sio makini nani vigeu geu sana hawana mwamana na hawaaminiki kabisa
   
 18. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #18
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nasikia katiba mpya wanayo idai CHADEMA Kadinali Pengo ndio ameitengeneza, duh watanzania tumekwisha aisee !!!
   
 19. d

  dotto JF-Expert Member

  #19
  Dec 15, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sina uhakika kama unaishi Tanzania au unafuatilia mambo ya TAnzania kwa Ukaribu sana. Celina Kombani alishasema CCM haina hoja hiyo na hata ilani yao haisemi hivyo. Kwani Celina Kombani sio wa CCM. Mbona unahoja finyu au ndo mlivyo watu wa CCM?
   
 20. P

  Patchu New Member

  #20
  Dec 15, 2010
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ikibidi katiba mpya ni lazima, watanzania walio wengi wameamka, waliolala ni wachache. Walioamka mungu anawaona na watafanikiwa kwa kutaka katiba, hakuna kulala mpaka kieleweke.
   
Loading...