Chadema yaandaa maandamano kupinga bei mpya ya umeme

Ni swali zuri. Nakupongeza. Naomba nikupe "lecture". Chukua kalamu na karatasi unakili points zifuatazo. Ni kweli maandamano yanayofanyika sehemu mbalimbali nchini ni ya kipuuzi lakini yana mwisho wake, yatakwisha iwapo:

1. Nchi itakuwa na utawala bora na utawala wa sheria.
2. Ufisadi utatokomezwa na watuhumiwa wote kufikishwa mahakamani.
3. katiba mpya itaundwa na kuridhiwa na wananchi wote.
4. CCM ambayo ndio chanzo cha maandamano ya kipuuzi itang'oewa madarakani.
5. Maliasili itatumika kwa faida ya wote
6. Jeshi la polisi litatenda haki kwa vyama vyote na si kuwa jeshi la ccm au chama kingine.
7. Sheria ya nchi itakuwa na usawa kwa wote na sio wengine kuwa juu ya sheria.
8. Maadili ya uongozi yatarejeshwa na uzalendo wa nchi utazingatiwa.
9. Kazi za kitaalamu zitapewa vipaumbele na motisha mzuri kuliko siasa kama ilivyo hivi sasa ambapo nchi imedumaa kwa vile wataalamu wote wameparamia siasa kwenye masilahi mazuri. Wengine wanakimbilia masilahi nchi nyingine.
10. Maisha vijijini yataboreshwa ili watu wasisongamane mijini.
11. Maadili na moyo wa kufanya kazi kuzingatiwa.

Mlolongo ni mrefu unaweza kuongeza. Zitunze points hizo uwe unajisomea kila siku. Lakini iwapo kweli mang'amuzi ya kiakili ni mapana, hata kama wewe ni miongoni mwa mafisadi, bado unaweza kugundua kuwa CCM ndio chanzo cha migomo ya kipuuzi kama unavyoiita. Uamke basi kutoka usingizini na utambue kuwa mtu asiyedai haki yake ndiye mpuuzi! Lakini hao wanaoandamana kudai haki sio wapuuzi hata kidogo!
 
Pumba hizi!

Dr Masanilo

Kuna wasomi wetu wengine wameridhika na hali zao za maisha basi wanaona kila kitu kiko shwari. Hawaangalii nchi yetu as a whole, wao wanajiangalia wao wenyewe walivyofanikiwa kimaisha na kusahau kwamba kuna Watanzania chungu nzima ambao wanaishi maisha yenye dhiki kubwa pamoja na utajiri mkubwa tuliokuwa nao wa rasilimali mbali mbali.

Watu kama hawa ndiyo wanaoipigia debe CCM kwamba ni nambari one pamoja na chama hicho kuwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya nchi yetu. Hawa hata ukiorodhesha matatizo mbali mbali ya uongozi dhaifu na usio na maadili hasa kuanzia awamu ya pili hadi sasa hawakuelewi wanakuona kama unaongea kichina. Ukiwakumbusha jinsi ambavyo nchi yetu haina utawala wa sheria ndiyo maana mafisadi wa EPA waliochota bilioni 133, wale wa Meremeta waliochota Bilioni 155, wale wa Richmond/Dowans waliolipwa mabilioni ya pesa na siajabu kuendelea kulipwa mabilioni mengine bila hata kuzalisha tone moja la umeme. Ufisadi uliokithiri uliofanywa katika awamu ya tatu e.g. Mkapa kujiuzia KCM, Mkapa kufanya biashara akiwa Ikulu, Mkapa kujiuzia nyumba za Serikali pamoja na mawaziri wake kwa bei ya kutupa na kuipa Serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 200, wale wahusika walioneemeka kwa ufisadi wa IPTL, ununuzi wa rada pamoja na kuwepo ushahidi wa kutosha, ununuzi wa helicopters na magari ya kijeshi, mikataba mbali mbali ya kuvuna rasilimali zetu ambayo haina maslahi kwa nchi yetu. Matatizo mbali mbali yanayoikabili nchi yetu kama vile ukosefu wa ajira kwa Watanzania walio wengi, wanafunzi kukaa chini au kuwa na madarasa ambayo hayana hata hadhi ya kufanywa vyoo, hospitali zisizo na madawa, vifaa muhimu au vitanda hata siku maoja hawakuelewi.

Wasomi kama hawa ndipo wanapopata madaraka hufikiria kujitajirisha wao na familia zao na kusahau kabisa kwamba wamekabidhiwa madaraka ya kufanya kazi kwa ajili ya Taifa a Tanzania, huweka mbele maslahi yao binafsi na kusahau yale ya Taifa ili tu na wao wawe mabilionea kwa kutumia njia za kifisadi.

Wasomi kama hawa watakwambia nao wana mapenzi ya kweli na Tanzania, kumbe ukweli wana mapenzi ya kweli na maslahi yao bila kujali yale ya Watanzania wengine

Unatamani kulia ukikutana na watu kama hawa wakianza kuongea/kuandika pumba zao ya viini macho ambavyo wao huona ni mafanikio ya CCM. Unashangaa kuona hawa ni wasomi na kuna ushahidi chungu nzima wa kudhibitisha kwamba CCM wameshindwa kuongoza nchi lakini hawa wasomi hawauoni ushahidi wote ulio mbele ya macho yao. Unatamani tu kupiga ukulele wa nguvu zako zote na kusema CRAAAAAPPPPPP!

MERRY XMAS
 
Siyo utamaduni wetu. Wa-Tz ni watu wa amani wanaojadili tofauti zao kwa kujenga hoja na kufikia maridhiano.

Mfano hai upo Zenj.

ACHA KUIGA KILA KITU KICHWA-KICHWA ETI KWA SABABU KINAFANYWA NA MATAIFA YA MAGHARIBI.

Kuna njia tatu tu za mwanadamu kudai HAKI 1- DIPLOMACY 2-VIOLANCE 3-COMBAT Zaidi ya hapo ni kukamua BEBERU MAZIWA!
 
Back
Top Bottom