Chadema yaandaa maandamano kupinga bei mpya ya umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema yaandaa maandamano kupinga bei mpya ya umeme

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Dec 23, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Chadema yaandaa maandamano kupinga bei mpya ya umeme
  Wednesday, 22 December 2010 20:07

  Hussein Issa na Eveline Kijumbe
  CHAMA Cha Demokrasia (Chadema), kimeandaa maandamano makubwa nchi nzima kupinga bei mpya ya umeme iliyotangazwa Desemba 20 mwaka huu na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura).

  "Tutawaunganisha wanachama wetu wote wa mikoani tujumuike pamoja katika maandamano hayo ili kudai haki zetu za msingi, "alisema Mkurugenzi wa Oganization na Mafunzo wa Chadema, Singo Kigaira.

  Kigaira aliwataka wafuasi wa chama hicho, wanachama na wananchi kuacha woga akieleza kuwa kila kitu kinahitaji mipango na katika maandamano hayo, kiongozi wa mipango hiyo ni Chadema.

  Awali akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Habari wa Chadema, Erasto Tumbo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa chama hicho kimeamua kuandaa maandamano hayo baada ya kutambua kuwa bei hiyo mpya ya umeme inamwumiza mwananchi wa kawaida.

  "Maandamano hayo tutayafanya mwezi Januari na tutaomba wananchi watuunge mkono kwa sababu hii ni haki ya msingi. Hakuna sababu ya kuonewa hapa. Junuari tutatangaza siku maalumu ya maandamano hayo,"alisema Tumbo.

  Aliendelea "Katika hali ya kawaida kabisa, mtu anakuwa na matumizi ya Sh1000 kwa siku, leo hii unampandishia umeme kwa asilimia 18.5, unadhani maisha yatakuwa rahisi kweli?”

  Kwa mujibu Tumbo, Serikali ingeweza kutumia njia nyingine mbadala kuboresha upatikanaji wa umeme nchini bila kuwapandishia wananchi bei ambao kimsingi ni mzigo kwao.

  Alisema moja kati ya njia hizo ni kufunga mitambo ya kisasa ya kuzalisha umeme ndani ya bahari ili kundokana na tatizo la upungufu wa maji ya kuzalisha nishati hiyo.

  Tumbo alisema baadhi ya nchi duniani, zinazalisha umeme kwa kutumia maji ya bahari jambo ambalo lingeweza pia kufanyika Tanzania kama viongozi wangekuwa wabunifu.

  “Pia Serikali ilipaswa kuboresha vifaa vya kutengenezea umeme wa jua ili umeme huo uzalishwe kwa wingi na sio kupandisha gharama za umeme kiholela na kutuumiza (wananchi),”alisema.

  Kwa mujibu wa Tumbo, kiini cha kupanda kwa bei ya umeme ni deni kubwa la Serikali katika taasisi zake, wizara na ofisi nyingine ambazo kwa kawaida hazilipi kodi hivyo kinachotakiwa ni kuwaeleza wananchi ukweli kuhusu madeni hayo.

  "Lazima tuelezwe ukweli kwamba Serikali na vigogo wake wanadaiwa shilingi ngapi kwani ndio hasa chanzo cha ongezeko la bei za umeme hapa nchini. Wananchi tumeshachoka kuburuzwa kama hatuna elimu, "alisema Tumbo.

  Alisema ongezeko hilo la bei ya umeme la asilimia 18.5, linaamanisha kuwa uniti moja sasa itakuwa inauzwa kwa Sh 367.80 kiasi ambacho kitamuumiza mwananchi wa hali ya chini.

  Tumbo alienda mbali zaidi na kusema anaamini kuwa Serikali imeamua kupandisha bei hiyo ya umeme ili kupata fedha za kuilipa kampuni ya Dowans inayoidai Tanesco mabilioni

  Alisema haiingii akilini kuona Tanesco inapandisha bei ya umeme wakati baadhi ya Watanzania hadi sasa wanashindwa kumudu gharama za kuingiza nishati hiyo majumbani mwao.

  Desemba 20 mwaka huu Ewura, iliruhusu Tanesco kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 18.5 kuanzia Januari Mosi mwakani.

  Mkurugenzi wa Ewura, Haruna Masebu, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa ongezeko hilo la bei ni chini ya mapendekezo ya Tanesco kwa asilimia 16.1.

  Kwa mujibu wa Masebu, Tanesco ilipendekeza umeme upande bei kwa asilimia 34.6, lakini baada ya uchambuzi wa kina, mamlaka ilikubali kuruhusu nyongeza ya asilimia 18.5 kwenye nishati hiyo.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Umeme waiweka serikali pabaya
  • CHADEMA kufanya maandamano nchi nzima kupinga bei mpya

  na Mwandishi wetu


  [​IMG] KUKOSEKANA kwa umeme wa uhakika na kupandishwa kwa gharama za nishati hiyo hivi karibuni kunaiweka serikali ya Rais Jakaya Kikwete katika shinikizo kali la kupingwa na umma wa Watanzania nchi nzima ukiongozwa na chama kikuu cha upinzani – CHADEMA.
  CHADEMA jana ilitangaza msimamo mkali wa kufanya maandamano nchi nzima wenye lengo la kuhamasisha na kuwaongoza wananchi wote kupinga ongezeko kubwa la gharama za umeme ikiwa serikali haitatengua haraka gharama mpya za kutumia nishati hiyo zilizotangazwa hivi karibuni.
  Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Madini nchini (EWURA) juzi ilitangaza kupandisha gharama za umeme kwa asilimia 18.
  Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho zilizopo Kinondoni mtaa wa Ufipa jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, Erasto Tumbo, alisema kiwango hicho ni kikubwa mno kwa wananchi wa kawaida.
  Alisema ni vema gharama hizo za umeme zingebebwa na serikali kwa sababu yenyewe ni moja ya taasisi zinazolimbikiza madeni sugu ya TANESCO hivyo kulifanya shirika hilo kushindwa kujiendesha.
  "Kulingana na kipato cha wananchi wengi wa kawaida kuwa cha chini ongezeko hilo la asilimia 18 linakuwa mzigo mwingine mzito unaokuja kuyakandamiza maisha ya wananchi wa kawaida," alisema Tumbo.
  Aliitaka serikali kusitisha haraka ongezeko hilo kwani litawaongezea wananchi machungu ya maisha.
  "Tunaiomba serikali isitishe ongezeko hili na kama itashindwa CHADEMA tutaitisha maandamano ya amani nchi nzima kupinga ongezeko hilo," alisema Tumbo.
  Alisema kwa kuwa serikali ndiye mdaiwa sugu wa TANESCO ni vema ikaweka wazi inadaiwa kiasi gani na shirika hilo pamoja na madeni ya vigogo na taasisi nyingine badala ya kukimbilia kuutua mzigo huo kwa wananchi ambao wengi hawana uwezo wa kumudu gharama mpya za umeme zilizotangazwa.
  Kupandishwa kwa gharama hizo kunaweza kuwa ni mpango wa serikali wa kulipa deni la Dowans ambalo waliamriwa kulilipa na Mahakama ya Biashara ya kimataifa hivi karibuni.
  CHADEMA pia imeishutumu TANESCO kwa tabia yake ya kupenda kujitangaza kila kukicha kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari wakati bado inashindwa hata kuboresha huduma zake.
  Wakati CHADEMA ikitoa msimamo huo jana hiyo hiyo serikali kupitia kwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, ilitangaza kuridhia kupanda kwa gharama zilizotangazwa na Ewura.
  Ngeleja alisema kupanda kwa bei ya umeme hakuna uhusiano wowote na suala la kutafuta pesa ili kulipa deni la sh bilioni 185 ambalo TANESCO inadaiwa na kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans.
  Serikali imewataka wananchi kukubali gharama hiyo ili kulifanya shirika hilo kupata pesa kwani limekuwa likijiendesha bila kutegemea ruzuku kutoka serikalini.
  Ngeleja alitoa msimamo huo jana alipokuwa katika ziara ya kikazi kwenye ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura).
  "….. TANESCO linajiendesha lenyewe na halitegemei ruzuku yoyote toka serikalini. Katika kupanda kwa bei ya umeme tunajua wananchi ndio wanaoumia kwa hilo, lakini hatuwezi kumfurahisha kila mtu…bei wanazotoza haziendani na gharama halisi za uendeshaji.
  "Kwa hili lazima wananchi waelewe juu ya kupanda kwa gharama hizo, wote ni wa hapa hapa, suala sio kubinafsisha shirika bali kutafuta njia ya kutatua tatizo," alisema Waziri Ngeleja.
  Katika maelezo yake Ngeleja alisema gharama za umeme kwa wateja hapa nchini ziko chini ikilinganishwa na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Alisema mwaka 2006 shirika lilipata hasara ya sh bilioni 168 na mwaka jana ilipoteza sh bilioni 5 kama hasara.
  "Nchi inakosa umeme wa uhakika kwa sababu mbalimbali ikiwemo miundombinu mibovu na zingine; ambapo maombi ya kupandisha gharama hizo kwa Ewura ni ya msingi ingawa wananchi wanalalamika," alimalizia Ngeleja.
   
 3. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,823
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Tujitokeze sasa kuwaonyesha mafisadi kwamba tumechoshwa na wizi wao na kwamba hatuko tayri tena kuwavumilia.
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Ngeleja atetea umeme kupanda


  *Asema lengo si kutafuta malipo ya DOWANS

  Na Rose Itono
  WAZIRI wa Nishati na Madini Bw. William Ngeleja ametetea kupanda kwa bei ya umeme kuwa ni kutokana na kupanda kwa gharama za endeshaji na si kulipa fidia ya kampuni ya Dowans kama inavyodaiwa.Juzi Shirika la Umeme nchini (TANESCO) lilipata
  baraka za Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (UWURA) kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 18.5 kuanzia Januari Mosi, hatua ambayo imelalamikiwa na wadau, huku baadhi wakidai huenda inakusanya fedha za kulipa deni la Dowans.

  Dowans ilishinda kesi katika Mahakama ua Usuluhishi ya Kimataifa kuwa inakiwa kulipwa dola milioni 69 na TANESCO kutokana kuvunjwa kwa mkataba baina yake, uliorithishwa na Richmond Development LCC, wa kuzalisha umeme wa dharura. Akizungumza jana Dar es salaam alipotembelea ofisi za EWURA, Waziri Ngeleja alifafanua kuwa bei zilizokuwa zikitozwa na TANESCO zilikuwa hazikidhi gharama za uendeshaji, na kulifanya shirika kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.

  Alisema kuwa, hata Desemba 2007 EWURA ilipitisha bei za umeme kwa TANESCO baada ya kulitaka Shirika hilo kuwasilisha taarifa kuhusu gharama halisi za huduma ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme nchini. Alisema hukumu juu ya Dowans na serikali imetolewa Novemba mwaka huu wakati TANESCO imeshapeleka mapendekezo juu ya bei mpya ya umeme EWURA.

  Alisema baada ya kupokea maombi la TANESCO Mei 28, 2010, EWURA ilifuata taratibu zote za kisheria kuchambua na hatimaye kufikia maamuzi.
  Bw. Ngeleja alisema umeme utaongezeka kwa wastani wa asilimia 18.5, na akawataka wananchi kuelewa maamuzi hayo. Alisema gharama hizo mpya zitaanza kutumika Januari mosi na kuongeza kuwataka wananachi kuonyesha ushirikiano kwa hilo ili kuliwezesha Shirika hilo liweze kujiendesha.

  Bw. Ngeleja alisema pamoja na shirika hilo kupandisha gharama hizo suala la kuwepo kwa mgawo wa umeme litakuwa likiendelea, na kasi ya mgawo itakuwa ikipungua siku hadi siku.Waziri alisema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha inamaliza kabisa kuwepo kwa tatizo la mgawo wa umeme ndani ya miaka mitano.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA, Bw. Haruna Masebu, kiwango hicho cha asilimia 18.5 kitakachoanza kutozwa na TANESCO Januari Mosi, mwakani ni karibu nusu ya ongezeko lililoombwa na TANESCO la asilimia 34.6.

  Bw. Masebu naye wakati anatangaza ongezeko hilo alitetea gharama hizo akisema kuwa wamefikia uamuzi huo bila kupendelea upande wowote na kwa kuzingatia mawazo yaliyotolewa na wadau wakati wa kujadili maombi ya shirika hilo."TANESCO waliomba ongezeko la asilimia 34.6 lakini baada ya kuangalia kwa makini gharama zao za uendeshaji na kwa kuzingatia mawazo ya wadau ambao walishirikishwa, tulifikia uamuzi wa kukubali ongezeko la asilimia 18.5 ili shirika liweze kujiendesha na hatimaye kutoa huduma nzuri kwa wananchi," alisema Bw. Masebu.

  Alisema kuwa baada ya kupata maombi hayo, waliyaangalia kwa kina na ilionekana kuwepo kwa hoja ya msingi, lakini haikukubaliwa kama ilivyowasilishwa.Kulingana mambo hayo, TANESCO iliomba kuongeza bei ya umeme kwa kipindi cha miaka mitatu kwa maana ya asilimia 34.6 kwa mwaka 2011, asilimia 13.8 kwa mwaka 2012 na asilimia 13.9 mwaka 2013.

  Kuhusu mambo hayo ya miaka miwili iliyobaki, Bw. Maseru alisema kuwa wataangalia baada ya suala hilo kufanyiwa utafiti wa kutosha na mtaalamu atakayependekezwa na EWURA hapo kufanyika na kumalizika mwakani.

  EWURA iliitaka TANESCO kuhakikisha inafungua akaunti maalumu zikiwemo za matengenezo na marekebisho, mpango wa uwekezaji wa mtaji, mpango wa gharama za kukunua umeme unaozalishwa nje.Masharti haya yanalenga kudhibiti mapato ya TANESCO ili kuhakikisha fedha zinazotengwa kwa kila mpango zinatumika kama ilivyokusudiwa, na akaunti hiyo itakaguliwa kila baada ya miezi mitatu.

  Akizungumza kuhusu hali ya uzalishaji umeme jana, Bw. Ngeleja alisema ufungaji wa transfoma ya Kipawa ulikamilika jana, hali itakayopunguza tatizo la mgawo kwa wakazi wa maeneo hayo.Mbali na suala la umeme, Bw. Masebu alimweleza Waziri Ngeleja kuwa mpaka sasa wamedhibiti suala la uchakachuaji wa mafuta kutoka asilimia 78 hadi asilimia 40 Juni 2010.

  Hata hivyo, Bw. Masebu alisema EWURA inakabiliwa na changamoto nyingi katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwa ni pamoja na ukosefu wa uhakiki na ubora.

  [​IMG]
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Point taken..........
   
 6. n

  nyantella JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Hivi busara za viongozi wa CDM ziko wapi? mseme tu mnataka umaarufu mkiandamana nchi nzima mnawakoa mafisadi? are you serious!! where is the logic besides CDM is a political party!!!!!!!!!! and not a pressure group!!!! kumbe hata CDM kuna vilaza wa siasa namna hiyo!!! waacheni chama cha watumiaji "consumers whatever they can call them selve" waandamana sana sana muwaunge mkono!!! shame on you. CDM is a powerful and very popular party to seek such a cheap popularity.

  Acheni vurugugu zenu mnatuharibia nchi nyinyi na mafisadi sawa tu! tuawaambieni tofauti if you you have any all you want is chaos we are now getting tired and sick of you!!!!!!!!!!!!!. And remmember whatever goes arround comes arround. unless you are sure that you are just a pressure group, so there is no way you will become a rulling party, be prepared to face the same chaos should CDM (GOD forbid! ) come into power in that form!

  CDM has greater potential to do well without being a bunch of thugs that is causing chaos every now and then. peolpe will hate it the was they hate FISADIS actully as of now the difference between the two of you is the SAME! (Sic!)
   
 7. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  katoka wapi huyu!
   
 8. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Wana JF hapa ndipo pa kuonyesha makucha yetu,hawa vichaa wa ccm lazima watambue kuwa ubabaishaji wao upo ukingoni.SWALI MUHIMU KWA WAZIRI tanesco inamakusanyo ya fedha kiasi gani kwa siku,mwezi?jee ina matumizi kiasi gani kwa siku mwezi ikiwa pamoja na wanazowalipa songas,dowans,iptl etc?jee madeni ni kiasi gani na list itolewe kwenye daily news tufahamu!
   
 9. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Hawachelewi kusema madeni ni siri yao ila watanzania mlipie ili wao wawakilishe!!
   
 10. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  I expect watu wote; CUF, CCM NCCR, na vyama vyote wataunga mkono hii issue. Unless wao hawaoni umuhimu wa hili issue; its comes a time when ushabiki tunauweka pembeni na tunajumuika wote kama wana jamii
   
 11. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2010
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  anaweza kuwa ni ngeleja.sishangai
   
 12. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tuko pamoja peoples power lazima ifanye kazi.

  Peoples power
   
 13. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #13
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  You are sick.
   
 14. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #14
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Kumekucha uwanja wa Nyamagana mwanza, Chadema 2 CCM 0 mpira unaendelea.......

  This is what so called political opportunity kwa mwendo huu hatuhitaji helkopta wala fedha nyingi kufanya campaign!!

  HAPA MWAKE!
   
 15. M

  MaryGeorge Member

  #15
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ametoka wapi huyu na comments za ajabu juu ya CDM kuandamana? anashangaa nini? ama kweli mwaka huu na ujao hakuna rangi waTZ hatutaacha iona...
   
 16. Elizaa

  Elizaa Senior Member

  #16
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 160
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  pamoja sana
   
 17. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #17
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  That's what I like to hear!!!!! Hip hip hooray CDM!!!!!!! Wananchi wote wenye akili zilizonyooka tuungane kwa dhati sasa kuonesha mafisadi nguvu ya umma!!! Natamani iwe kesho!!!!!!.... People's power for EVER!!!!!.....
   
 18. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #18
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wewe aliyekudanganya maandamano ni CHAOS ni nani???? Ina maana hata CCM wanavyoandamana kushabikia ujinga wao hua wanaleta Chaos????? Au imekua CHAOS kwa vile CDM wanaandaa???? Acha hizo wewe!!!!....
   
 19. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #19
  Dec 23, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hivi busara za viongozi wa sisi m waliochakachua udiwani zipo wapi?
   
 20. cumshot

  cumshot Member

  #20
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na huyu vp anaikalia ya ccm nini?
   
Loading...