Chadema yaamua kutimkia mikoani kutimua vumbi la mchakato wa katiba mpya

Scolari Ndenga

JF-Expert Member
Aug 4, 2008
271
43
Wadau,

Katika kile kinchoonekana ni kuwaweka wananchama wake na wananchi kwa ujumla mguu pande mguu sawa, Chadema imeamua kusambaza viongozi na wabunge wake Tanzania nzima ili kuweka kinagaubaga msimamo wake na mchakato wake wa kuelekea kupata katiba mpya.

Katika kufanikisha hilo, Chadema kimeagiza kuitishwa kwa mikutano mikuu ya majimbo na mjadala wa katiba kwa maana ya kuweka wazi kwa nini wabunge wake walitoka bungeni, waraka wa chama kwa Rais kikwete, na msimamo wake wa kutoshiriki mchakato wa katiba iwapo hakutakuwapo na mabadiliko makubwa na ya msingi kama wanavyodai.

Ninachokioona hapo, Chadema wana mikakati mingi ambayo hawajataka kuioweka wazi kwa public kwa kua wanasubiri mabadiliko ya sheria kama walivyokubaliana na rais huku wakiendelea na michakato ya kuwaweka wanachama wao mkao wa kijeshi.
 
Mimi ni MCHADEMA ila kitendo cha Chama changu kwenda Ikulu na Kuongea na JK kimeniuthi na kunikatisha tamaa. Haikuhitajika hata elimu ya darasa la saba kujua eti Rais yule yule aliyewashinikiza wabunge wake wapitishe mswaada eti atagoma kuusaini mswaada mara baada ya kupitishwa na wabunge wake. Mbowe, Lissu, Baregu, Mnyika, Safari, Arfi, etc kwa kweli imani yangu kwenu imepungua sana.
 
Huu ni mpango mkakati(strategic plan) mzuri...na nadhani tungepewa ratiba officially..najua wapo makamanda wetu humu ndani chini ya dada Regia wanaweza kutupa official information.....otherwise I think for the time being this is right decision till further notice especially after actions from the Government of magamba and JK regarding to the memorandum of understanding which was signed by Kamanda Mnyika as representative of our part and Nchimbi on the other side as GVT representative......
 
Mimi ni MCHADEMA ila kitendo cha Chama changu kwenda Ikulu na Kuongea na JK kimeniuthi na kunikatisha tamaa. Haikuhitajika hata elimu ya darasa la saba kujua eti Rais yule yule aliyewashinikiza wabunge wake wapitishe mswaada eti atagoma kuusaini mswaada mara baada ya kupitishwa na wabunge wake. Mbowe, Lissu, Baregu, Mnyika, Safari, Arfi, etc kwa kweli imani yangu kwenu imepungua sana.

Mkuu ni kweli,lakini nadhani ni njia nzuri ya kuanza kwa mazungumzo...ili wakipuuza kwa kipindi kingine tunapoingia barabarani wasiwe na sababu...rudisha imani mkuu,CHADEMA ni chama makini,na nyuma yake kina wasomi wakufa mtu ambao wanatoa strategic plan za ukweli..kama akina Prof.Baregu,Dr Mkumbo nk...Jipe moyo mapambano bado yanaendelea...
 
Tip walizozipata ikulu zimeshaisha?

Si mmezoea kutoa tips eeh...pumbavu!! hii sio CUF au NCCR huu ni mziki mwingine...sisi maskini jeuri hatutishwi na hela zenu za kijambazi common!!!
 
Tukubali tu chadema kwa issue ya katiba wamechemsha. Kitendo cha kutoka bungeni, then baada ya muda wakaenda kujikomba kwa JK ikulu, kimefanya kila mtu akose na imani nacho
 
Hii nadhani ni kichekesho cha kumalizia mwaka. .....Rejao ulikuwa na imani na CDM lini, ambayo sasa imekutoka baada ya kumuona JK?
 
Mimi ni MCHADEMA ila kitendo cha Chama changu kwenda Ikulu na Kuongea na JK kimeniuthi na kunikatisha tamaa. Haikuhitajika hata elimu ya darasa la saba kujua eti Rais yule yule aliyewashinikiza wabunge wake wapitishe mswaada eti atagoma kuusaini mswaada mara baada ya kupitishwa na wabunge wake. Mbowe, Lissu, Baregu, Mnyika, Safari, Arfi, etc kwa kweli imani yangu kwenu imepungua sana.
mkuu mi nadhani walikua sahihi,kwani unapo dai haki unatakiwa uidai hatua kwa hatua kutoka nje ilikua hatua ya kwanza kwa lengo la kutokua katika kundi la kuupitisha mswada,lakini pia njia ya pili ni kwenda kumlalamikia rais juu ya haki ya wananchi kupokonywa,then ni kwenda kuishitaki serikali kwa wananchi kwani wao ndio wawakilishi wao kwa serikali,mwisho ni nini wananchi wataamua hapo ndipo nguvu ya umma yenye mkono wa mungu husimama kitete mpaka kieleweke
 
Wadau,

Katika kile kinchoonekana ni kuwaweka wananchama wake na wananchi kwa ujumla mguu pande mguu sawa, Chadema imeamua kusambaza viongozi na wabunge wake Tanzania nzima ili kuweka kinagaubaga msimamo wake na mchakato wake wa kuelekea kupata katiba mpya.

Katika kufanikisha hilo, Chadema kimeagiza kuitishwa kwa mikutano mikuu ya majimbo na mjadala wa katiba kwa maana ya kuweka wazi kwa nini wabunge wake walitoka bungeni, waraka wa chama kwa Rais kikwete, na msimamo wake wa kutoshiriki mchakato wa katiba iwapo hakutakuwapo na mabadiliko makubwa na ya msingi kama wanavyodai.

Ninachokioona hapo, Chadema wana mikakati mingi ambayo hawajataka kuioweka wazi kwa public kwa kua wanasubiri mabadiliko ya sheria kama walivyokubaliana na rais huku wakiendelea na michakato ya kuwaweka wanachama wao mkao wa kijeshi.

In chadema I trust.
 
Mmmh.. ndugu imani hailazimishwi,Waachie wenye imani waiamini CDM yao.. Wewe endelea na GAMBA lako kwani ungemsikiliza vizuri Mnyika /Lissu ungefahamu sababu ya wao kwenda Ikulu..Bunge lilipitisha mswada,na ili uwe sheria ni lazima Rais ausain ili uwe sheri.Wao walienda kumtaarifu mapungufu yaliyopo ktk ule mswada ili asi sign kutokana na mapungufu yaliyopo..
 
Hii nadhani ni kichekesho cha kumalizia mwaka. .....Rejao ulikuwa na imani na CDM lini, ambayo sasa imekutoka baada ya kumuona JK?
Chadema leo wanaweza wakafanya kitu kizuri ukaapreciate ambacho kweli kimapose threat kwa serikali,especilly Zitto na Mnyika but baada ya muda wanaharibu completely.
 
Mmmh.. ndugu imani hailazimishwi,Waachie wenye imani waiamini CDM yao.. Wewe endelea na GAMBA lako kwani ungemsikiliza vizuri Mnyika /Lissu ungefahamu sababu ya wao kwenda Ikulu..Bunge lilipitisha mswada,na ili uwe sheria ni lazima Rais ausain ili uwe sheri.Wao walienda kumtaarifu mapungufu yaliyopo ktk ule mswada ili asi sign kutokana na mapungufu yaliyopo..
Wangewatumia wananchi kuwaelezea hayo mapungufu na wananchi wafanye maamuzi cuz wao ndio waajiri wao. Kitendo cha kwenda Ikulu kimefanya serikali kurelax.
 
Thubutuu aingie mtu barabarani nani mjinga waingie wenyewe waone watakavyokamatwa ka kuku!!
 
MUBARAK, BEN ALLY WA TUNISIA NA GHADAFI WA LIBYA walituma polisi wengi na majeshi kukamata watu au kujaribu kupambana na nguvu ya umma ( PEOPLE'S POWER) leo hii wako wapi jibu unalo mwenyewe. misri kuna polisi wengi mara 10 ya idadi ya polisi wa Tanzania lakini walishindwa kufua dafu kwenye nguvu ya ummma itakuwa hawa polisi waliokondeana kwa kukosa mishahara.
 
Wadau,

Katika kile kinchoonekana ni kuwaweka wananchama wake na wananchi kwa ujumla mguu pande mguu sawa, Chadema imeamua kusambaza viongozi na wabunge wake Tanzania nzima ili kuweka kinagaubaga msimamo wake na mchakato wake wa kuelekea kupata katiba mpya.

Katika kufanikisha hilo, Chadema kimeagiza kuitishwa kwa mikutano mikuu ya majimbo na mjadala wa katiba kwa maana ya kuweka wazi kwa nini wabunge wake walitoka bungeni, waraka wa chama kwa Rais kikwete, na msimamo wake wa kutoshiriki mchakato wa katiba iwapo hakutakuwapo na mabadiliko makubwa na ya msingi kama wanavyodai.

Ninachokioona hapo, Chadema wana mikakati mingi ambayo hawajataka kuioweka wazi kwa public kwa kua wanasubiri mabadiliko ya sheria kama walivyokubaliana na rais huku wakiendelea na michakato ya kuwaweka wanachama wao mkao wa kijeshi.
Hawa jamaa bado sijawaelewa nia yao ya dhati ni ipi
 
Back
Top Bottom