CHADEMA ya sasa ni ya kizazi cha watu waoga sana

Mtondoli

Member
Nov 9, 2021
70
174
Inawezekana mkanipinga kama ilivyokawaida yenu huwa hampendi kuambiwa ukweli. Chadema hii ni ya vijana waoga sana sana, wako Dkt. Slaa CHADEMA walikuwa wakitangaza maandamo yanakuwa maandamano kweli. Watu walikuwa wanasafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine kushiriki maandamano. Si kwamba vitisho havikuwepo la hasha vilikuwepo, polisi walikuwepo,matumizi ya bullet yalikuwa zaidi ya sasa.

Nilikuwepo Arusha kwenye maandamo yaliyokuwa yameitishwa na chadema, viongozi walikuwa mstari wa mbele wakiwa na vitambaa vyeupe nakumbuka Dkt. Slaa aliongoza hayo maandamano, akiwemo Freeman Mbowe, Godbess Lema, Mzee Ndesamburo, watu walisafiri kutoka mikoa yote Tanzania kuja kusapoti maandamano hayo.

Nchi ilizizima huku polisi wakiendelea kupiga mikwara ya kutisha kabisa, umati wa watu ulifunga barabara karibia kila sehemu, watu walifunga maduka wakaja kuungana na wanamageuzi wenzao chadema, kama ilivyo ada polisi walianza kurusha risasi ovyo na mabomu ya machozi, wengine walipata kipigo akiwemo na mke wa Dkt. Slaa, Josephine Mushumbusi aliumizwa vibaya Sana

Kuna vijana walikufa na wakazikwa kishujaa na bendera za chama zikapepea nusu mlingoti. Hiyo haikuwatisha maandamano yaliendelea kila mahari. Nasema nyinyi vijana wa sasa hamuisaidii demokrasia mkiwa waoga namna hiyo

Kwa suala la Mbowe mpaka leo pangekuwa hapatoshi, nani wa kuwa mstari wa mbele kututia morali ya kutokuogopa vitisho vya polisi? Hayupo ni Dkt. Slaa peke yake ndie angethubutu, CHADEMA mmepoteza watu muhimu sana kwa ajili ya mkate wa siku moja, mrudisheni Dkt Slaa mtaona jinsi mpinzani anavyotakiwa awe.
 
Ukiacha ya chadema kuna tozo, kuungua kwa masoko, madai ya katiba mpya, kukua kwa Deni la taifa kiholela, kupanda kwa bei ya bidha

Je, nadhani chadema ndo wanazuia wananchi wasiandamano?
 
NI sawa na umfunge kamba mtu halafu umpige wee alafu umwambie wewe ni MUOGA.
 
Back
Top Bottom