CHADEMA: What on earth is this?

Kama hayo yaliyoandikwa yako sawa, then chama mbadala hakina vision, huwezi kufirikia kwa mtizamo wa karibu kiasi hicho.

Huwezi kufikiria utakuwa mpinzani forever, huwezi kufirikia siku zote mpinzani wako ni CCM?

Huwezi fikiria always issue ni mafisadi...

It is real a shame, chama kinaandika dira yake kama shairi la rusha roho!

Mkuu Kasheshe,

Umeongea yote, lakini pia hata proofreading hawakufanya. Wote tunafanya makosa ya lugha lakini unapoongelea chama mbadala lazima vitu vidogo kama hivyo uwe na watu wa kuviangalia na kuvirekebisha.
Mrengo nafikiri ilitakiwa iwe Mlengo, uoza nafikiri ilitakiwa iwe uozo.

Zaidi ya hayo message yenyewe ni kama shallow mno na ni mambo ya kijuweni ile mbaya.

Huenda utangulizi huo umeandikwa bila hata vichwa wa CHADEMA kupitia na kuona kama ni sawa.
 
chadema inajaribu kusema kiswahili kile wapiga kura wao wanakielewa labda :)
 
Hapana Shala kuwa kaka yangu Wanakijiji umeleewa vibaya maana ya chama Mbadala, Baada ya kuona kuwa CCM wameshindwa kwa yote na kuwa lazima watu wanahitaji siasa mbadala, na kuona chama ambacho cha kuchukua nchi ya Tanzania hata Bunge kwa ujumla, sijaona kuwa kuna tatizo lolote kwa maneno hayo ya hapo chini kuhusu Chadema, Mbona hujasema kuwa CCM na Maisha Bora KWA KILA MTANZANIA.hivyo ndio siasa za kila Dunia. Mbona Marekani Obama alikuja na Changes, Hivyo ni Vibwagizo katika siasa, Watu wanataka Chama Mbadala badala ya Chama Cha siasa.
 
I personally do not see a problem na hiyo message. Ukiangalia context nzima, lazima ukumbuke hiyo imeandikwa katika tovuti. Hichi ni kitu rahisi kubadilishwa, na kinakuwa 'updated' kulingana na nyakati. Hii messege inaenda na nyakati hizi hasa tunapokaribi Uchaguzi Mkuu 2010. narudia tena, lazima uangalia context nzima waheshimiwa.
 
To begin with, I don't know what is "mrengo", although I know about mlengo if that is what they mean. The site could use some proofreading.

According to the "Kamusi ya Kiswahili-Kiingereza" toleo la kwanza 2001, iliyochapishwa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, "mrengo" (siasa) is wing....
 
According to the "Kamusi ya Kiswahili-Kiingereza" toleo la kwanza 2001, iliyochapishwa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, "mrengo" (siasa) is wing....

I had thought so. Asante kwa kutupa FACTS!
 
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama mbadala kinachokua na kinachoongozwa kwa Falsafa ya "Nguvu ya Umma" na kuamini katika itikadi ya "Mrengo wa Kati".

CHADEMA kinataka Watanzania waelewe kuwa Mabadiliko ya kweli yataletwa kwa kubadilisha mfumo mzima wa utawala. Maendeleo ya kweli hayawezi kuletwa na mafisadi walewale, wa chama kilekile, chenye uoza uleule, wakiendeleza yaleyale kwa ari, nguvu na kasi mpya.

Haya yamethibitishwa na Serikali ya awamu ya nne kwani sera na juhudi zao zimeambulia kutuletea usanii mpya, maahadi mapya na hakuna jipya; Kwao maisha bora ni kwa kila fisadi!
haya maneno yanafaa kwa siasa za TZ, lazima watu mtofautishe uwezo wa kuelewa wa waTZ walio wengi(ni mdogo) na wale elite ambao ni kidogo lakini uwelewa wao ni mkubwa. kama hauna rhetoric huweza kushinda wala kuvutia watu TZ kwenye chama, sio TZ hata US kama huna rhetoric huwezi kushinda wala kuvutia watu

Kama hayo yaliyoandikwa yako sawa, then chama mbadala hakina vision, huwezi kufirikia kwa mtizamo wa karibu kiasi hicho.

Huwezi kufikiria utakuwa mpinzani forever, huwezi kufirikia siku zote mpinzani wako ni CCM?

Huwezi fikiria always issue ni mafisadi...

It is real a shame, chama kinaandika dira yake kama shairi la rusha roho!

wakichukua serikali na maneno yanabadilika, sasa hivi wao ni wapinzani kwa hiyo lazima waandike kama wapinzani na wakiwa serikalini wataandika wanatufanyia nini

maneno ya kwenye website hayawezi kuwa hayo hayo kila siku, yanatakiwa yabadilike kutokana na position yao, wakiingia serikalini maneno yatabadilika

inaonekana wewe unafikiria ki-ccm na kudhania kwamba maneno hayatakiwi kubadilika na ndio maana mpaka leo baadhi ya viongozi wa ccm wanatuambia wao ndio chama walichotuletea uhuru.... wanatakiwa wabadilike waende na wakati na kutueleza wanatufanyia nini
 
Last edited:
According to the "Kamusi ya Kiswahili-Kiingereza" toleo la kwanza 2001, iliyochapishwa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, "mrengo" (siasa) is wing....

Kweli kiswahili kinakuwa asante NYANI umenifanya nami niangalie kamusi na hii ni kwa kuongeza tu.

mrengo , pl mirengo { English: wing, pl wings } [ Terminology: political ]
noun 3/4

Swahili Example: Waziri Mkuu wa Italia Silvio Berlusconi amejiuzulu na kujiandaa kuunda serikali mpya ya mrengo wa kulia ya mseto [BBC 20 Aprili 2005]

English Example: Italian Prime Minister Silvio Berlusconi has resigned and is preparing to form a new right-wing coalition governement

mrengo , pl mirengo { English: outrigger for canoe stability, pl outriggers [Dialect: Kimvita]} [ Terminology: marine ]
noun 3/4 [ photos: upload ]
 
hata mimi nimeshangaa maaana JF na CHADEMA sawa na samaki na maji huwezi kuandika chochote kumcriticise Freeman au CHADEMA maana chances itaondolewa au itafutwa

mimi leo bado nipo kwenye shock!

GT,

Reducing these entire fora, with their entire spectrum from intellectuals, inflated ego prima-donnas, to one track minded airhead dingbats to a wing of the CHADEMA party says more about you than these fora.
 
Wakuu,
Chadema wanasema mrengo wa KATI wana maana gani?..ina maana sii kulia wala kushoto ila katikati au?.. na ni itikadi gani ktk lugha ya kigeni (kiingereza) inayowakilisha mrengo wa kati, wana maana - Centrism - ule mpango wa Maxism?..
 
Wakuu,
Chadema wanasema mrengo wa KATI wana maana gani?..ina maana sii kulia wala kushoto ila katikati au?.. na ni itikadi gani ktk lugha ya kigeni (kiingereza) inayowakilisha mrengo wa kati..Je wana maana Centrism! ule mpango wa Maxism?..

Ni idiology. Kama wanaiga wanavyofuata Wamarekani ni kwamba Marekani kuna Liberals (the left) na Conservatives (the right). Mtu akiwa na mrengo wa kati kwa kufuata ideology za Marekani ni kwamba ni mtu yupo open minded to both ideologies na hayuko extreme.

Sasa sijui wenzetu wana maana sawa au kama wao wana maana tofauti.
 
Tatizo la siasa (soma "si hasa") nchini Tanzania ni kwamba:

1) Viongozi waliopo wanadhani/wanaamini kwamba ni WAO wenye dhamana au majukumu ya kuwapelekea wananchi maendeleo, fursa sawa na maisha bora, badala ya wananchi kuwaongoza viongozi hao kwa kuwaambia nini kifanyike, na kibaya zaidi ni kwamba

2) Wananchi wenyewe wanaamini kwamba viongozi waliochaguliwa ndio wenye "muarobaini" wa kuwapelekea maendeleo, fursa sawa na maisha bora, kiasi kwamba wamekasimu hata majukumu ya "kufikiria" nini kifanyike kwa hao viongozi, wengi wao wakiwa WABABAISHAJI tu!

Suala la mapinduzi ya kifikra bado ni changa sana hapa nchini, mpaka hapo hali hiyo itakapofikiwa, CHADEMA watapata uhalali wa kuongoza nchi hii. Kwa sasa, BADO sana. Hawana tofauti na hiyo CCM wanayoipiga vita kwenye "front page" ya website yao... au ni weblogu? LOL

./MwanaHaki
 
Mwanafalsafa1,
Mkuu hicho ndio hasa kilichonichanganya maanake hapo awali niliambiwa kwamba Chadema wanafuata itikadi ya kulia (Conservative). Sasa napoona hii maswla ya kati (Moderate) kusema kweli yanatisha na kuchanganya zaidi iwe ktk mfumo wa Marekani au Urusi kwa sababu hatufahamu wao wanatazama upande gani....
 
Mkuu MMKjj, leo imekuwaje? Wengi humu tunafikiri wewe ni Chadema, sasa haya mambo si mungeyajadili kwenye vikao vyenu vya ndani?

sina control ya vitu ambavyo mtu mwingine anafikiri! Kwani, kuna wengine wanafikiri mwezi umetengenezwa kwa jibini, na wapo wanafikiri kuwa wanajua kitu ambacho hawajui na wanakipendekeza kwa wengine kama wanajua. Sasa nyinyi "wengi humu" mnaofikiri msingi wenu wa kufikiri hivyo hasa ni nini?
 
Mzee Mwankijiji,
Duh, wanafikiri wewe Chadema?... Hivi kweli hawalioni hilo jembe begani!
 
GT,

Reducing these entire fora, with their entire spectrum from intellectuals, inflated ego prima-donnas, to one track minded airhead dingbats to a wing of the CHADEMA party says more about you than these fora.
Bluray,
You sound like a guy I used to know a while ago by the name Pundit.
 
Ni idiology. Kama wanaiga wanavyofuata Wamarekani ni kwamba Marekani kuna Liberals (the left) na Conservatives (the right). Mtu akiwa na mrengo wa kati kwa kufuata ideology za Marekani ni kwamba ni mtu yupo open minded to both ideologies na hayuko extreme.

Sasa sijui wenzetu wana maana sawa au kama wao wana maana tofauti.

Sidhani kama siasa zetu zinafuata mfumo kama wa Marekani. Kwa mfano, ni misimamo gani inayomfanya mtu au mwanasiasa Tanzania kuwa liberal au conservative?
 
Ndiyo maana nikaelezea tu hiyo mirego huwa ina maanisha nini. Sijui kama wenzetu wa Chadema wana maana nyingine. Kwa sababu pia Chadema ni federalist kwa maneno ya Mbowe mwenyewe ambaye alisema njia madhubuti ya kupata maendeleo ni kwa smfumo wa majimbo which is also an American system.
 
Back
Top Bottom