CHADEMA + Werema v/s Zitto : Naombeni tamko la CHADEMA kuunga mkono serikali

Kamanda mimi nawataka wale wote wanaodai kwamba "CDM IMEUNGA MKONO KAULI YA WEREMA" walete tamko.

@Njano 5 OLESAIDIMU Ritz ZeMarcopolo FaizaFoxy Rutashobolwa n.k NATAKA TAMKO LA CHAMA
Kuna Zuzu mmoja sijui linaitwa Saint nani nani, nimeliambia lionyeshe tamko la CDM la kumuunga mkono werema likaishia kuniporomoshea matusi. Kweli nimeamini kuna watu wanawaza kwa kutumia makalio.
 
Mkuu, tamko baso halijatolewa na CHADEMA hawana haja ya kufanya hovyo so long aliyenangwa ni mbaya wao

Jamani ehe... naona wengi hamjamuelewa mwanzisha thread au mmemuelewa lakini hamtaki kumjibu. Ni hivi: Amesema hapa kwenye forum kuna baadhi ya members ambao wanasema kuwa Chadema imeungana na CCM kumkandia Zitto eti hana majina ya wenye fedha chafu nje ya nchi. Sasa anauliza liko wapi tamko la Chadema la kukubaliana na AG? Mimi nafikiri ameuliza swali zuri tu kwa sababu kwa kadiri mimi ninavyojua mpaka muda huu sijaona tamko lolote la Chadema kukubaliana na AG na mtu huwezi kusema wamekubalina na AG bila kuona tamko!!
 
Kama Lema angeshambuliwa na Werema, CHADEMA wangetoa tamko. Ila kwa vile aliyeshambuliwa ni Zitto ndo maana chama kimekaa kimya! Hoja ya werema imetiwa nguvu na kaulimya Lema kuwa yeye yupo tayari kuyataja hayo majina na hahitaji ulinzi katika kufanya hivyo. Swali la kujiuliza, ujasiri wa Lema umetokana na nini? Kama ameshindwa kutaja majina ya watu aliodai kuwa wametengeneza na kusambaza zile picha zake za kulawitiwa (ingawa anajua kuwa zile oicha hazikuwa za kutengwneza), ataweza hili la Mafisadi?

Toka mwanzo wa sakata hili la fedha za uswis Lema alishasema kama zito anaogopa kuwataja ampe yeye Lema awataje hii kauli si mpya tatizo liko kwa Zito ambae mambo yake yote binafsi hayafiki mwisho na yanaambatana na hila. sa kama lingekuwa swala ni la CDM zito angekabidhi hoja yake kwa CDM sa ye kaficha utete kitu usichokijua hili nilake kama yalivyomengine asitafute mchawi ataje majina aache unafiki na kutafuta sababu za kitoto za kuanza kulaumu watu wengine wakati analopoka alilopoka kwa manufaa yake binafsi. kama ye kashindwa awape wanaume wayataje hayo majina,
 
Le big show bana nakukubali sana vipi hii avatar sio tumia ile ile yako mkuu. indicator kuwa ni wewe "with due respect"
 
Juzi katika kikao cha Bunge, Serikali Kupitia Mwanasheria wake Mkuu Jaji Werema ilitoa taarifa kwamba Mh Zitto Zuberi Kabwe aliyedai kwamba ana Majina ya Watanzania walioficha Pesa Uswisi Kinyume na Taratibu Amesema mbele ya Kiapo kwamba "Hatambui hata Mtanzania Mmoja aliyeficha Pesa Uswisi".

Baada ya Kauli hiyo kumeendelezwa Mijadala Mbalimbali na nimeshuhudia "THREAD" Mbalimbali zikianzishwa lakini zote zikiwa na Maudhui yale yale "CHADEMA WAMEUNGANA NA CCM KUMNANGA ZITTO", "CHADEMA YAMTOSA ZITTO KWENYE ISHU YA MABILIONI YA USWISI"

Mbaya zaidi nimeona "watu wale wale" wakiishia tu Kutunga "Hypothesis" Kujaribu kuelezea "Ni Kwa Nini Zitto ameahirisha Kutaja Majina Kama aliyovyahidi" na "Kwenda Mbali zaidi Kukana Kujua Majina ya Walioficha Uswisi".

Na watu wale wale wameendelea Kutoa Shutuma kwa CDM "Kwa nini Hawajamuunga Mkono Zitto" au "Kwa Nini Wamemuunga Mkono Warema" Katika hili nimeshangaa sana kuwaona watu ambao mimi nawaamini sana na wenye wameshika Bango hoja hii ya CCM

Mods with due respect najua mtashawishika kuinganisha hii thread na zile zingine ambazo zimeshindwa kujibu Maswali ya Msingi

Ninependa kama kuna mtu mwenye Tamko la CDM la Kumuunga Mkono Werema aliweke Hapa ili kama tunailaumu CDM kwa Kuunga Mkono CCM basi tuzungumze kwa Ushahidi na Si Hisia za Watu

Kama zilivyoachwa Thread zingine natumai kwamba na hii itaachwa vile vile bila kuunganishwa

NAOMBENI TAMKO LA CHADEMA KUUNGA MKONO KAULI YA WAREMA
Invisible Paw PainKiller

Kwenye uzi wako, ilo unalotaka ili iweje mkuu?
 
Jamani ehe... naona wengi hamjamuelewa mwanzisha thread au mmemuelewa lakini hamtaki kumjibu. Ni hivi: Amesema hapa kwenye forum kuna baadhi ya members ambao wanasema kuwa Chadema imeungana na CCM kumkandia Zitto eti hana majina ya wenye fedha chafu nje ya nchi. Sasa anauliza liko wapi tamko la Chadema la kukubaliana na AG? Mimi nafikiri ameuliza swali zuri tu kwa sababu kwa kadiri mimi ninavyojua mpaka muda huu sijaona tamko lolote la Chadema kukubaliana na AG na mtu huwezi kusema wamekubalina na AG bila kuona tamko!!


Na hatuwezi kusema wanampinga bila kuona tamko!!!!!!
 
Acheni kuzungumzia vitu nyeti kitoto! Kwa mujibu wa WEREMA, ZITO alikuwa anadai eti kuna watanzania wameficha mabilioni Uswisi. Serikali ilimuomba Zito atoe hiyo orodha ili serikali ianze uchunguzi wake, but ZITO akawa anapiga chenga, hadi pale alipolazimishwa chini ya kiapo kufanya hivyo. Chini ya kiapo hicho, ZITO akatoa maelezo ya kutokua na jina hata moja la mtu aliye na mapesa Uswisi!!!

Ikumbukwe kwamba kabla AG WEREMA hajazungumza bungeni juzi, LEMA alishatoa maelezo ndani ya bunge kuhusu hayo madai ya ZITO. Alichosema LEMA ni hiki: ZITO ayataje bungeni hayo majina ya watu walioficha fedha USWISI, na kama anaogopa kuyataja kwa sababu za usalama wake basi ampe AG majina ya watu hao ili sheria ichukue mkondo wake. Na kama bado ZITO anaogopa kumpa AG hayo majina, basi ampe LEMA ayataje bungeni kwani yeye hahitaji kinga yoyote!


Uki-analyse vizuri maelezo ya hapo juu, utapata hitimisho lifuatalo: ZITO anatengeneza FAKE PATRIOTISM ili awahadae WATANZANIA kwa kumpa FAKE GOOD POLITICAL IMAGE! Hii ni agenda binafsi ya ZITO kumjenga yeye binafsi na kitendo cha yeye kushindwa kuthibitisha chini ya kiapo majina ya wenye mapesa Uswisi inaonyesha namna ambavyo ZITO alikuwa akiwahadaa WATANZANIA kwa agenda fake! [

ZITO akaamua kujificha kwenye KICHAKA cha "KUHAKIKISHIWA USALAMA WAKE KWANZA" ndipo ayataje majina hayo. Kimsingi Mwanamapinduzi makini hahitaji kinga ya "usalama wake" ili alete mapinduzi halisi kwa watu wake. LEMA alimuonyesha ZITO tafsiri halisi ya MWANAMAPINDUZI kwa kumpasha hapo hapo bungeni kuwa yeye hahitaji kinga ya usalama wake ili ayataje majina ya watu walioficha fedha USWISI!


Naomba kuhitimisha kwa kusema kuwa hakuna namna yoyote ambayo unaweza kuihusisha CHADEMA kama chama na yaliyojadiliwa bungeni juzi kwa sababu yale yalikuwa ni mazungumzo ya kawaida bungeni. QUOTE=CHAMVIGA;8089911]Tamko washatoa. Kwasasa hawana haja na mabilioni ya Uswis madam aliyenangwa na Zitto Z Kabwe.[/QUOTE]
 
Kwenye uzi wako, ilo unalotaka ili iweje mkuu?

Lengo ni Kuzithibitisha tuhuma kwamba CDM Wamemuunga Mkono WEREMA, So far siwezi Kuziamini Mpaka pale Mtakapoweka Tamko Kama Lipo
 
Kama Lema angeshambuliwa na Werema, CHADEMA wangetoa tamko. Ila kwa vile aliyeshambuliwa ni Zitto ndo maana chama kimekaa kimya! Hoja ya werema imetiwa nguvu na kaulimya Lema kuwa yeye yupo tayari kuyataja hayo majina na hahitaji ulinzi katika kufanya hivyo. Swali la kujiuliza, ujasiri wa Lema umetokana na nini? Kama ameshindwa kutaja majina ya watu aliodai kuwa wametengeneza na kusambaza zile picha zake za kulawitiwa (ingawa anajua kuwa zile oicha hazikuwa za kutengwneza), ataweza hili la Mafisadi?

Kwani Bungeni ni nani alimuunga mkono mwingine kati ya Lema na Werema? Nani alitangulia kuongea, ni Lema kusema kwamba yuko tayari kuwataja hao watuhumiwa akipewa majina au ni Werema kutamka kuwa Mh Zitto aliapa kuwa hana jina hata moja la mtuhumiwa? Kama Werema ndiye aliyetangulia kusema kuhusu Mh Zitto kutokuwa na majina ya walioficha pesa nje basi kama Mh Lema baadaye aliomba hayo majina (ambayo hayapo) ili ayataje basi atakuwa alichanganyikiwa. Ila kama kwa nia njema alidhani majina yapo ila watu wanashindwa au kuogopa kuyataja na akajitolea yeye kuyataja hadharani bila kuhitaji kinga yoyote hapo atakuwa amempingaje Mh Zitto? Naona kama alikuwa akiunga mkono juhudi za Mh Zitto kusaka na kuwaadabisha wahalifu!
 
Hivi katika hali ya kawaida huwezi kuona jinsi CHADEMA-Mbowe wanavyomuunga mkono werema!?au hili nalo linaitaji tamko na miwani ya jua kuling'amua

Nilishawaambia hii ni aibu yenu wahafidhina,leo mnaona aibu kisa siku mbili hizi mmejinasibisha na maCCM kisa kumkomoa Zitto,mnasaliti mapambano kisa kupambana na wapigania demokrasia

Leo mnataka tamko?!

Watoe kwanza tamko la kukubaliana na lema mini kaang kuhusu posho.

Mnatia kinyaa!

anayetia kinyaa i yule aliyetaka sifa na kusema ana majina kumbe hana hata moja tena chini ya kiapo katamka!!!huyu zitto kashachanganyikiwa akili,mbowe alimuokota akamleta kwenye chama na kumlea malipo yake ni matusi sababu ya vihela vya ccm.Sasa laana inamwangukia.
 
Usichanganye mambo!, ungekuwa na akili ungeanza kujiliuliza kwanza kwann ZZK hoja hiyo kaikumbatia peke yake bila kukishirikisha chama? Ukumbuke tu chama kilitaka kiihodhi hii hoja tangu mwanzo ZZK kwa kihelehele akajifanya kutoka nayo kivyake.... Kama unasubiri tamko utasubiri sana,, fikiria kwa kuustukia akili sio makalio

Chama hakijakatazwa kuibeba hiyo Hoja, kwa nini Kiliacha?

Chama kilikuwa na uwezo wa kumuita Zitto kabwe kwenye Kamati kuu na Kumwambia kwamba aiache hiyo hoja na badala yake ibebwe na Chama je Chama kilifanya hivyo?

Ni hoja gani haswaa ndani ya bunge iliwahi kubebwa na chama kizima?, Buzwagi?, EPA?
 
Sasa kiherehere chake cha kutuambia atataja kilikuwa cha nini?
Inaonyesha na wewe pia ni mmoja wa wenye viherehere alowasema JK.

Kiherehere uache kuwa wewe unayetafuta majina bila kujua utayafanyia nini,niwe mimi ambaye sina mda na hayo majina bali pesa zirudi hapa kusaidia kukuza uchumi

Wewe kwa akili yako kama ya lema unaamini kwamba majina yatakusaidia kwamba wakitajwa watarudisha tu kisa ni majina!,mimi nataka pesa zirudi kuwashtaki tutawashtaki sisi na sio CCM kama unavyofikiri.

#teamMajina mnakera
 
anayetia kinyaa i yule aliyetaka sifa na kusema ana majina kumbe hana hata moja tena chini ya kiapo katamka!!!huyu zitto kashachanganyikiwa akili,mbowe alimuokota akamleta kwenye chama na kumlea malipo yake ni matusi sababu ya vihela vya ccm.Sasa laana inamwangukia.

Mkuu nyabhingi ,

Tukianza kuongelea kuletwa kwenye chama list ni ndefu hatutamaliza hapa,

Ushawishi haijawahi kuwa kosa la jinai au sifa kwamba mimi nilikushawishi nyabhingi kuwa ujiunge CHADEMA,hata kama ulimleta mtu fulani kwenye chama si kigezo cha wewe kumfunga mdomo na kumzuia kugombea vyeo kwenye chama au taasisi

Majina hayana umuhimu wakati huu na wewe ni mmoja wa watu makini hapa JF ulitakiwa kulitambua hilo kabla...

Majina yatatusaidia nini katika wakati huu wa CCM Ambapo mafisadi wa EPA wanasamehewa??,

Tunaitaji pesa zirudi hayo majina tutashughulika nayo sisi come 2016 ambapo mgombea wa CHADEMA amekaa ofisini ikulu
 
Last edited by a moderator:
Mh Zitto mbunge kigoma kaskazini NITAJIBU MAPIGO YA WEREMA. Mbunge wa Kigoma kaskazini Zitto (chadema) amesema atamjibu mwanasheria mkuu wa serikali, Jaji Fredrick Werema juu ya kauli aliyoisema bungeni kwamba mbunge huyo hana majina ya watanzania waliyoficha mabilioni Uswis. Zitto alisema kwa kuwa Jaji Werema alimshambulia kupitia bunge naye atatoa majibu bungeni ili ukweli uweze kubainika. Nilimsikia mwanasheria mkuu wa serikali akinishambulia! Nitakachokifanya ni kwamba wiki ijayo nitamjibu hapa bungeni baada ya kumuomba spika anipe nafasi ya kuwasilisha maelezo binafsi alisema Zitto. Mwanasheria mkuu ni muongo nasema totally ni muongo kwa sababu nimehudhuria maranne na nikawakabidhi majina ya watuhumiwa. Tena kibaya zaidi niliwakabidhi hadi jina la Mchungaji wa kimataifa ambaye angeweza kuwasaidia ktk uchunguzi wao alisema zitto. Chanzo ni gazeti la rai
 
Kiherehere uache kuwa wewe unayetafuta majina bila kujua utayafanyia nini,niwe mimi ambaye sina mda na hayo majina bali pesa zirudi hapa kusaidia kukuza uchumi

Wewe kwa akili yako kama ya lema unaamini kwamba majina yatakusaidia kwamba wakitajwa watarudisha tu kisa ni majina!,mimi nataka pesa zirudi kuwashtaki tutawashtaki sisi na sio CCM kama unavyofikiri.

#teamMajina mnakera
Inaonyesha kama umesoma basi hujaelimika na hujui lolote unaloliandika hapa.
Kumbuka zitto kabeba hii issu kivyake na ubinafsi wake wala haihusiani na CDM. Pia kutuzungusha zungusha kama watoto wadogo na tabia zenu za kike sie hatutaki kama unasema unasema sio longolongo. Kaa subir tamko baba. Mna kiherehere cha kujifanya mnaweza kumbe waoga watupu.
 
Back
Top Bottom