CHADEMA + Werema v/s Zitto : Naombeni tamko la CHADEMA kuunga mkono serikali

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,560
1,195
Juzi katika kikao cha Bunge, Serikali Kupitia Mwanasheria wake Mkuu Jaji Werema ilitoa taarifa kwamba Mh Zitto Zuberi Kabwe aliyedai kwamba ana Majina ya Watanzania walioficha Pesa Uswisi Kinyume na Taratibu Amesema mbele ya Kiapo kwamba "Hatambui hata Mtanzania Mmoja aliyeficha Pesa Uswisi".

Baada ya Kauli hiyo kumeendelezwa Mijadala Mbalimbali na nimeshuhudia "THREAD" Mbalimbali zikianzishwa lakini zote zikiwa na Maudhui yale yale "CHADEMA WAMEUNGANA NA CCM KUMNANGA ZITTO", "CHADEMA YAMTOSA ZITTO KWENYE ISHU YA MABILIONI YA USWISI"

Mbaya zaidi nimeona "watu wale wale" wakiishia tu Kutunga "Hypothesis" Kujaribu kuelezea "Ni Kwa Nini Zitto ameahirisha Kutaja Majina Kama aliyovyahidi" na "Kwenda Mbali zaidi Kukana Kujua Majina ya Walioficha Uswisi".

Na watu wale wale wameendelea Kutoa Shutuma kwa CDM "Kwa nini Hawajamuunga Mkono Zitto" au "Kwa Nini Wamemuunga Mkono Warema" Katika hili nimeshangaa sana kuwaona watu ambao mimi nawaamini sana na wenye wameshika Bango hoja hii ya CCM

Mods with due respect najua mtashawishika kuinganisha hii thread na zile zingine ambazo zimeshindwa kujibu Maswali ya Msingi

Ninependa kama kuna mtu mwenye Tamko la CDM la Kumuunga Mkono Werema aliweke Hapa ili kama tunailaumu CDM kwa Kuunga Mkono CCM basi tuzungumze kwa Ushahidi na Si Hisia za Watu

Kama zilivyoachwa Thread zingine natumai kwamba na hii itaachwa vile vile bila kuunganishwa

NAOMBENI TAMKO LA CHADEMA KUUNGA MKONO KAULI YA WAREMA
Invisible Paw PainKiller
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,156
1,250
They say "silence means yes"!!!!!!

Sijui ni valid na reliable kwa kiasi gani!!!!!!!
 

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,560
1,195
They say "silence means yes"!!!!!!

Sijui ni valid na reliable kwa kiasi gani!!!!!!!

Silence Could Mean "Wanamuunga Mkono Zitto" kwa nini umechagua Maana?

Mkuu Bado unaleta Hisia

NATAKA TAMKO LA CHAMA
 

mjasiliaupeo

JF-Expert Member
Apr 21, 2013
1,967
2,000
mkuu hii kitu wameikuza tuu, zito kutofautiana hoja na lema ni kutokana na mitazamo binafsi, sioni haja ya kuunganisha chama kwenye hili ukizingatia ile ilikuwa hoja binafsi haikubeba vision ya chama.
 

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,560
1,195
mkuu hii kitu wameikuza tuu, zito kutofautiana hoja na lema ni kutokana na mitazamo binafsi, sioni haja ya kuunganisha chama kwenye hili ukizingatia ile ilikuwa hoja binafsi haikubeba vision ya chama.

Kamanda mimi nawataka wale wote wanaodai kwamba "CDM IMEUNGA MKONO KAULI YA WEREMA" walete tamko.

@Njano 5 OLESAIDIMU Ritz ZeMarcopolo FaizaFoxy Rutashobolwa n.k NATAKA TAMKO LA CHAMA
 

CHAMVIGA

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
7,689
2,000
Tamko washatoa. Kwasasa hawana haja na mabilioni ya Uswis madam aliyenangwa na Zitto Z Kabwe.
 

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,905
2,000
Kama Lema angeshambuliwa na Werema, CHADEMA wangetoa tamko. Ila kwa vile aliyeshambuliwa ni Zitto ndo maana chama kimekaa kimya! Hoja ya werema imetiwa nguvu na kaulimya Lema kuwa yeye yupo tayari kuyataja hayo majina na hahitaji ulinzi katika kufanya hivyo. Swali la kujiuliza, ujasiri wa Lema umetokana na nini? Kama ameshindwa kutaja majina ya watu aliodai kuwa wametengeneza na kusambaza zile picha zake za kulawitiwa (ingawa anajua kuwa zile oicha hazikuwa za kutengwneza), ataweza hili la Mafisadi?
 

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,349
2,000
Silence Could Mean "Wanamuunga Mkono Zitto" kwa nini umechagua Maana?

Mkuu Bado unaleta Hisia

NATAKA TAMKO LA CHAMA

Kama unataka tamko la chama kaonane na Mnyika Tamko la chama hapa jf wewe kweli mbulula.
 

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,217
2,000
Silence Could Mean "Wanamuunga Mkono Zitto" kwa nini umechagua Maana?

Mkuu Bado unaleta Hisia

NATAKA TAMKO LA CHAMA

Kijana wa Nyaga, Unasubiri tamko la chadema ndiyo uende Serena Hotel kumtetea mteja wako...
 

kiabasaka

Senior Member
Nov 28, 2013
146
0
Tamko la Chama anatoa katibu Mkuu sasa JF member tutakupa chini ya kapeti ila usinirekodi Au unataka nivuliwe madaraka Albedo
 

NO EXCUSE

JF-Expert Member
Sep 10, 2012
417
250
mkuu hii kitu wameikuza tuu, zito kutofautiana hoja na lema ni kutokana na mitazamo binafsi, sioni haja ya kuunganisha chama kwenye hili ukizingatia ile ilikuwa hoja binafsi haikubeba vision ya chama.

Awali ilikuwa hoja ya chama lakini ikiwa kwenye popeline dogo akimbia nayo akaibinafsisha.
 

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,560
1,195
Naona Vijana wa Lumumba wamelielewa Vizuri hili Bandiko langu kwa Tahadhari kubwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom