Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,276
Tunaomba kukutaarifu na kualika chombo chako kwenye mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika Ofisi za CHADEMA Kanda ya Pwani (Magomeni) kuanzia saa 9 mchana, ambapo Viongozi waandamizi wa Chama watazungumza juu ya masuala muhimu. Tunasisitiza yatakuwa masuala muhimu. Tunatanguliza shukrani zetu.
========UPDATES
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali wamefika Ofisi za Chadema Kanda ya Pwani.-
Baada ya mawaziri wawili kutoka wizara tofauti kuongea na waandishi wa habari kuhusu kifo cha mwanafunzi wa NIT - Akwilina, CHADEMA wakosoa kauli zao za maswala ya uchunguzi; wadai mawaziri wanaleta siasa katika vitu vyenye maana.
CHADEMA kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Mahusiano, Itifaki na Mambo ya Nje, John Mrema amewataka Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba na Naibu Waziri wake Hamad Masauni kujiuzulu kufuatia kifo cha mwanafunzi aliyeuawa kwa kupigwa risasi.
Tumemsikia Kamanda Mambosasa akieleza kuwa polisi wanamtafuta mwenyekiti wetu Freeman Mbowe. Mwenyekiti yupo hajajificha tunamshangaa Kamanda Lazaro Mambosasa anamtafuta mtu ambaye anajua anakaa wapi: Benson Kigaila Mkrugenzi wa Oparesheni ya Uchaguzi CHADEMA.
"Tunamtaka Masauni na Mwigulu wakumbuke Mwinyi alijiuzulu wakati wafungwa walipofia Gerezani Shinyanga," -John Mrema
"Serikali haiumii kupoteza raia wake bali inaumia raia aliyekufa amepoteza mkopo, unaweza ukashangaa sana, eti Serikali wao wanasikitishwa kwa sababu Serikali imetumia pesa nyingi kumgharamia mwanafunzi huyu ni mnufaika wa mkopo" John Mrema
Tumesikia Mambosasa na amekuwa very specific amesema anamtafuta Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe Freeman Mbowe M/kiti wetu hajajificha mpaka polisi wakatangaze kwenye vyombo vya habari kwamba wanamsaka, yupo wampe wito, wanazo taratibu za kumuita mtu polisi"
"Au wakamkamate, wanajua ofisini kwake Makao Makuu ya CHADEMA, Ofisi za Bunge au ofisi za biashara zake binafsi na hata nyumbani kwake kote wanajaua na taratibu za kumuita mtu polisi zinajulikana"
" Polepole amesema CHADEMA tuliwapakia vijana kwenye mabasi ili wakashiriki maandamano, eti hata huyu binti alikuwa miongoni mwa waliokuwa wamepakiwa kwenye bus kwenda kwenye maandamano, hii ni kauli ya hovyo kabisa, sio kauli ya Kiongozi"
" Polepole anataka kuwaambia nini wazazi wa yule mwanafunzi? inasemekana mwanafunzi huyu alitoka kwenye safari zake alikuwa kwenye daladala, Jeshi la polisi likamuhoji Polepole inawezekana anaelewa zaidi tukio hili lilivyotokea "
"Sisi CHADEMA tulitoka kwenye mkutano wa hadhara tukawa tunaenda na mawakala wetu kwa Mkurugenzi kudai viapo na barua za mawakala wetu, kama polisi waliona ni kosa, kuna utaratibu wa kuzuia maandamano na upo kwa mujibu wa sheria, sheria iliyounda jeshi la polisi" John Mrema
““Mambosasa anasema ilipigwa risasi moja juu, kisha anasema wamekamatwa askari sita, walipigaje hiyo risasi na aliyeamuru risasi zipigwe juu ni nani,”
"Viongozi wa aina hii hawastahili hata kuongoza kikundi cha ngoma,”-
“Risasi ziliwalenga viongozi wa juu wa Chadema, lakini leo wanasema sisi tumesababisha, tunawezaje kujipiga risasi wenyewe,”- Benson Kigaila, Kamanda wa Operesheni Uchaguzi Kinondoni.
"Ukisema yule binti alibebwa na mabasi ya Chadema, wakati ndugu, jamaa na marafiki zake wanajua alikuwa wapi, hata ukienda kwenye msiba ndugu zake wanakuonaje,”- Benson Kigaila, Kamanda wa Operesheni Uchaguzi Kinondoni.
“Watu waliopigwa risasi ni walinzi wanne wa viongozi na wanatibiwa katika hospitali mbalimbali, risasi hazikupigwa juu, zilikuwa zinalenga nyonga na miguu,”- Benson Kigaila, Kamanda wa Operesheni Uchaguzi Kinondoni
.“Mtu wa kwanza aliyesababisha mauaji hayo ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni, ambaye tangu mwanzo tulisema ni jeuri, hakuna siku watu wameapa wakaacha viapo vyao wakaondoka,”- Benson Kigaila, Kamanda wa Operesheni Uchaguzi Kinondoni.
“Kesho wanasheria wetu watatoa tamko kuhusu hatua za kisheria tutakazochukua kuhusiana na suala la uchaguzi na kifo cha mwanafunzi,”- John Mrema Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje.