CHADEMA Wazindua Matawi vyuo Vikuu: St Johns, DIT, CBE, IFM na Mipango-Dodoma

Safi sana msisahau Tabora kunamadenti wengi sana, Iringa na hata singida kuna haja ya kuamsha ari ya mabadiliko.

Visiwani nako msikulazie sana wapo vijana wengi tu. mkumbuke huko hakuna upinzani kwa sasa ni vyema mkajipenyeza mapema mapema.

Ahsante sana
 
Kwa mwamko huu kuna watu, wakiwemo baadhi ya wanachadema maarufu, watakaopatwa na kiharusi!
 
Nimefarijika sana. Tuanzishe na kwenye shule za sekondari movements kama hizi. Tunahitaji vijana waamke na kuchukua hatua za ukombozi wa taifa lao. Najua wana wa mafisadi wamekasirika lakini hatupo kuwafurahisha
 
Wakuu habari.

Jana siku ya Jumamosi tarehe 12 Februari 2011 kwa nyakati tofauti Wabunge wa CHADEMA wamezindua matawi ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Vya Mt Johns na Mipango.Kabla ya Uzinduzi kulitanguliwa na hotuba fupi fupi za wabunge hao. Mikutano yote ilikuwa ni mizuri sana.

Wabunge waliowakilisha Chama ni

1. Prof Kahigi- Bukombe
2.Halima Mdee- Kawe
3.John Mnyika-Ubungo
4.Godbless Lema-Arusha Mjini
5.Rebecca Mgodo-Viti Maalum Arusha
6.Regia Mtema- Vitimaalum Kilombero

Wanafunzi zaidi ya 200 wa Chuo Cha Mt John wamejiunga na CHADEMA sambamba na ufunguzi wa ofisi ya tawi hilo.

Zaidi ya wanafunzi 1000 wa Vyuo vya Mipango na UDOM wamejiunga na CHADEMA Sambamba na ufunguzi wa Tawi.

Wabunge hawa walipokelewa kwa nderemo na vifijo na wanafunzi hao.

Mapambano yanaendelea,Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.

N.B: Picha za matukio yote mawili baadaye kidogo.

Zoezi hili linaendelea leo viwanja via Sabasaba jijini Dar es Salaam kwa vyuo vya DIT, IFM, CBE n.k

From Dodoma.

Aluta Continua

Weldone chadema you are in the right truck. Tunisia na Misri walipita uchochoro huo so keep it up
 
Hongerini Chadema. Tunawasubiri huku vijijini. Kuni zipo tayari ninyi njoni muwashe moto tu.
Haitachukua muda mrefu CCM watashangaa hawamo katika uongozi wa dola. Wananchi tunaelewa wazi sasa hivi CCM wanatutawala badala kutuongoza. Wenyenchi tunajua tunachohitaji na hilo CCM hawawezi kutupatia. Tumesema tunataka katiba mpya Rais anajifanya kuwa hilo ni jukumu lake, kama yeye na CCM wameshindwa kutupatia maisha bora katiba wataiwezaje?

Misri ilichukua tu siku 18 kiongozi wa nchi aliondoka madarakani. Tanzania tupo tayari, tunasubiri tu siku na sisi tuyaseme madai yetu wazi wazi.
 
Hapa ndio umuhimu wa CDM kuwa na combo chake cha habari Kama Radio au Tv unapoonekana,habri Kama hizi zilitakiwa zisambae Kama kimbunga nchi nzima ili mwamko uwe juu zaidi maana vyombo vingine vya habari sio vya kutegemea sana kutoa uzito kwa mambo Kama haya pamoja na umuhimu wake

Hili nalo ni neno zuri
 
Wakuu habari.

Jana siku ya Jumamosi tarehe 12 Februari 2011 kwa nyakati tofauti Wabunge wa CHADEMA wamezindua matawi ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Vya Mt Johns na Mipango.Kabla ya Uzinduzi kulitanguliwa na hotuba fupi fupi za wabunge hao. Mikutano yote ilikuwa ni mizuri sana.

Wabunge waliowakilisha Chama ni

1. Prof Kahigi- Bukombe
2.Halima Mdee- Kawe
3.John Mnyika-Ubungo
4.Godbless Lema-Arusha Mjini
5.Rebecca Mgodo-Viti Maalum Arusha
6.Regia Mtema- Vitimaalum Kilombero

Wanafunzi zaidi ya 200 wa Chuo Cha Mt John wamejiunga na CHADEMA sambamba na ufunguzi wa ofisi ya tawi hilo.

Zaidi ya wanafunzi 1000 wa Vyuo vya Mipango na UDOM wamejiunga na CHADEMA Sambamba na ufunguzi wa Tawi.

Wabunge hawa walipokelewa kwa nderemo na vifijo na wanafunzi hao.

Mapambano yanaendelea,Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.

N.B: Picha za matukio yote mawili baadaye kidogo.

Zoezi hili linaendelea leo viwanja via Sabasaba jijini Dar es Salaam kwa vyuo vya DIT, IFM, CBE n.k

From Dodoma.

Aluta Continua

Kilombero For Change(K4C)-Mfuko wa Maendeleo Kilombero

naomba jina na akaunti namba ya huo mfuko.
 
Regia,

..msisahau VYUO VYA UALIMU.

..waalimu wana ushawishi mkubwa ktk jamii zetu.

..pia wanapangiwa kazi maeneo ya vijijini ambako mnahitaji wanachama.

NB:

..msiishie vyuo vikuu tu, muwe na mkakati wa vyuo vya elimu ya kati pia.
 
Ushauri:

Kwanza, Kwakuwa hao wanachama ni wanafunzi washaurini pia wafaulu masomo yao wafanye biddi darasani si siasa tu....wamalize masomo (kwakuwa wazazi wao na taifa) wangependa wamalize masomo yao kwa faida yao..
 
Wakuu habari.

Jana siku ya Jumamosi tarehe 12 Februari 2011 kwa nyakati tofauti Wabunge wa CHADEMA wamezindua matawi ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Vya Mt Johns na Mipango.Kabla ya Uzinduzi kulitanguliwa na hotuba fupi fupi za wabunge hao. Mikutano yote ilikuwa ni mizuri sana.

Wabunge waliowakilisha Chama ni

1. Prof Kahigi- Bukombe
2.Halima Mdee- Kawe
3.John Mnyika-Ubungo
4.Godbless Lema-Arusha Mjini
5.Rebecca Mgodo-Viti Maalum Arusha
6.Regia Mtema- Vitimaalum Kilombero

Wanafunzi zaidi ya 200 wa Chuo Cha Mt John wamejiunga na CHADEMA sambamba na ufunguzi wa ofisi ya tawi hilo.

Zaidi ya wanafunzi 1000 wa Vyuo vya Mipango na UDOM wamejiunga na CHADEMA Sambamba na ufunguzi wa Tawi.

Wabunge hawa walipokelewa kwa nderemo na vifijo na wanafunzi hao.

Mapambano yanaendelea,Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.

N.B: Picha za matukio yote mawili baadaye kidogo.

Zoezi hili linaendelea leo viwanja via Sabasaba jijini Dar es Salaam kwa vyuo vya DIT, IFM, CBE n.k

From Dodoma.

Aluta Continua
Regia Regia Regia dada angu. Hapo penye cbe naomba udeliti. Tulihudhulia hilo tukio lakini sisi wenye bado hatujafungua tawi rasmi. Kuhusu members tuko wengi ila kwa sasa wengi wako likizo. Nipo cbe dom.
 
Tunaomba mje na chuo kikuu cha kiislamu hapa morogoro tunawasubiri kwa hamu sana.
 
Jamani hivi CDM hatuwezi kuwa na Vituo vya TV na Redio. Wakubwa angalieni hili tunahitaji sana.
 
Back
Top Bottom