CHADEMA wazindua kampeni za Udiwani kwa kishindo Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA wazindua kampeni za Udiwani kwa kishindo Mbeya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Mar 12, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimezindua kampeni zake za udiwani wa Kata ya Kiwira wilayani Rungwe na kufanikiwa kupata umati mkubwa watu waliofurika kusikiliza sera za chama hicho.
  Uchaguzi huo mdogo wa udiwani unakuja kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo, John Mwankenja (CCM), aliyeuawa kwa kupigwa risasi mwaka jana.
  Akizungumza katika mkutano huo wa uzinduzi juzi uliofanyika pembezoni mwa soko la ndizi mjini Kiwira, Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Mary Mallack, alisema kuwa wananchi wa kata hiyo wanahitaji mabadiko ya kimaendeleo, ambayo kwa sasa hayawezi kuletwa tena na viongozi wa CCM.
  “Tunaposema tunahitaji mabadiliko tunamaanisha wananchi kutoka hali duni kwenda kwenye maisha mazuri, hilo haliwezi kufanikishwa na viongozi wa CCM ambao hawana tena fikra mpya zaidi ya kudai nyongeza ya posho, sisi watu wa Kiwira kama tunahitaji mabadiliko hayo tuanze kwanza kubadilisha viongozi kutoka ngazi za chini,” alisema Mallack.
  Aliwataka wananchi wa Kiwira kumchagua mgombea udiwani kupitia CHADEMA, Lawrent Mwakalebule, kwa maendeleo ya kata hiyo kwa kuwa atahakikisha anatetea masilahi yao.
  Naye, Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija, maarufu kwa jina la ‘Mzee wa Upako’, aliwataka wananchi kumchagua mgombea wa CHADEMA kwa vile awali walifanya makosa ya kuichagua CCM.
  Mgombea udiwani wa kata hiyo, Mwakalebule (25) alisema kuwa ameamua kujitosa kuwania kiti hicho akiwa na umri mdogo ili wananchi waweze kumtuma kwa kila jambo na kila kero zinazowasumbua.
  Alisema dhamira yake ni kutaka kubadilisha maisha ya wanachi wa Kiwira kutoka hapo walipo na kuwafanya wapate maendeleo zaidi katika biashara, elimu, miundombinu na katika sekta ya afya.

  Source:Tanzania Daima
   
Loading...