CHADEMA wawalilia wapambanaji, Halima Mchuka na John Ngahyoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA wawalilia wapambanaji, Halima Mchuka na John Ngahyoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chief Isike, Jan 1, 2012.

 1. Chief Isike

  Chief Isike JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2012
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  [FONT=&amp]
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI[/FONT]


  [FONT=&amp]SALAAM ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA, NDUGU NA TASNIA ZIMA YA HABARI, KUFUTIA VIFO VYA WAPENDWA WETU, HALIMA MCHUKA NA JOHN NGAHYOMA

  [/FONT]
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko, majonzi na maskitiko makubwa taarifa za misiba ya waandishi wa habari waandamizi nchini, waliokuwa wapambanaji hodari kuutumikia umma kupitia tasnia ya habari, Bi. Halima Mchuka (TBC) na John Ngahyoma(BBC), vilivyoripotiwa kutokea jana na leo.
  [FONT=&amp]
  [/FONT][FONT=&amp]Bi. Mchuka aliyefariki jana, daima atakumbukwa na Watanzania wenzake wote kwa uwezo na umahiri wake katika taaluma ya uandishi wa habari. Bila shaka yoyote kuondoka kwake kwa ghafla, kumeacha pengo la utaalam, uwezo na uzoefu katika tasnia ya habari nchini, ambao Watanzania walinufaika kutoka kwake tangu enzi za Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) hadi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Bi. Halima Mchuka, ambaye ujasiri wake wa kujaribu, kuthubutu na kuweza, vimemfanya aache historia kubwa nyuma yake kwa kuwa mwandishi wa habari pekee wa kike, kuweza kutangaza mechi za mpira wa miguu hapa nchini na Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Pamoja na utumishi wake kwa umma wa Watanzania kupitia taaluma yake hiyo muhimu, historia hiyo ya kipekee katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati, inayodhihirisha ishara ya ushujaa na uwezo wake wa kupambana dhidi ya mfumo dume, itamfanya Bi. Halima Mchuka aendelee kuishi daima katika kumbukumbu za watu vizazi na vizaji vijavyo.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  John Ngahyoma, mmoja wa waandishi wa habari waandamizi nchini atakumbukwa kwa uhodari, umahiri na uwezo wake, tangu akiwa vyumba vya habari vya Kampuni ya IPP (ITV na Redio One), kabla hajajiunga na Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), akiwa miongoni mwa Watanzania wachache waliofanikiwa kutokana na uwezo wao, kujiunga na kutumikia umma wa Watanzania wenzake na dunia kwa ujumla, kupitia shirika hilo kubwa la utangazaji duniani. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Ataendelea kuishi katika kumbukumbu za Watanzania wengi waliofanya naye kazi, waliokuwa wakimsikiliza tangu enzi za ITV/Redio One na wakati akitumikia BBC. Watanzania watamkumbuka alivyofanya uandishi unaowajibika kwa umma. Watakumbuka hata namna alivyokuwa akitafuta na kuwasilisha habari zake na aina za habari hizo, akiifanya kazi yake kwa kuzingatia maadili yanayosimamia taaluma ya uandishi wa habari. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  CHADEMA inaungana na Watanzania wote kokote waliko katika kutambua na kuenzi mchango wa wapendwa wetu hao waliotangulia mbele za haki. Tunaungana na familia za marehemu wote, ndugu, jamaa, rafiki zao na Watanzania wengine wote katika wakati huu mgumu, kuwalilia na kuwaombea kwa Mungu marehemu wetu hao.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  CHADEMA kinatoa pole za dhati na kuzitakia familia za marehemu moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi makuwa ya kuondokewa na wapendwa wao. Pole za dhati pia ziende kwa tasnia nzima ya Uandishi wa Habari nchini, ambayo kwa hakika imetikiswa kwa misiba hii miwili, kwa kuwapoteza wapambanaji hawa, katika wakati ambao bila shaka uwezo, uzoefu na utaalam wao ulikuwa bado unahitajika. [/FONT]

  [FONT=&amp]Pamoja na kuwalilia wana habari hawa, waliobaki katika tasnia hiyo hawana budi kujifunza kutoka kwao, wakiendeleza umuhimu wa kusimamia maadili yao, kutumikia na kuweka mbele maslahi ya umma kupitia kalamu zao. Ni ukweli pia usiopingika kuwa pengo hilo litaigharimu tasnia hiyo muda na gharama kuandaa watu wengine wa aina ya hawa waliotutangulia.[/FONT]

  [FONT=&amp]Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, Amina![/FONT]

  [FONT=&amp]Imetolewa leo, Desemba 30, 2011[/FONT]

  [FONT=&amp]Ofisi ya Kurugenzi ya Habari na Uenezi Makao Makuu ya CHADEMA, Dar es Salaam.[/FONT]
   
 2. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  imekaa njema
   
 3. Chief Isike

  Chief Isike JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2012
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Poleni mlio mbali na vyombo vya habari v ya nchini ambao hamkuweza kupata salaam za CHADEMA kwa Watanzania wenzetu hawa, ilioka katika vyombo vya habari juzi usiku na jana!
   
Loading...