CHADEMA wawakejeli waasisi wa CCJ; Wasaliti waomba kazi za CDM kuziuza kwa CCM - Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA wawakejeli waasisi wa CCJ; Wasaliti waomba kazi za CDM kuziuza kwa CCM - Mbeya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 18, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]Na Waandishi wetu, Mbeya


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Mbeya kimewataka makada wasaliti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliosisi Chama cha Jamii (CCJ) akiwemo Waziri wa Afrika Mashariki Samuel Sitta kuacha unafiki, badala yake wajipange kuimarisha upinzani wakiwa ndani ya chama tawala.

  Kauli hiyo ya CHADEMA imekuja siku moja baada ya CCM kuandamana wakiongozwa na wanaodaiwa kuwa waasisi wa CCJ na kupokea wanachama wapya ambao ni viongozi na diwani wa Nzovwe kwa tiketi ya CHADEMA.

  Pamoja na Sitta wana CCM wengine wanaodaiwa kukianzisha CCJ ni Dk. Harrison Mwakyembe ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mwenyekiti wa zamani wa UVCCM mkoani Arusha, Daniel Ole Porokwa.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Katibu wa CHADEMA mkoani Mbeya, Edo Mwamalala, alisema maandamano yaliyofanywa na CCM hayana mashiko kwa kuwa yalilenga kulumbana badala ya kuueleza umma mambo ya maendeleo.

  Mwamalala alisema kitendo cha waanzilishi hao wa CCJ kusimama na kuanza kuikosoa serikali yao kwa maelezo kwamba imeshindwa kusimamia vema sekta ya umeme na dhana ya kujivua gamba, ni wazi kuwa wameshindwa kutekeleza wajibu wao hivyo wanaiunga mkono CHADEMA.

  "Ninadhani hawa watu wana ajenda ya siri…hata mchezo uliofanyika ndani ya CCM kununua kadi za chama chetu kutoka kwa wanaowaita wafuasi wa CHADEMA tunaufahamu na tayari mmoja kati ya waliotumiwa kutimiza azma hiyo tumemkamata na yuko polisi Mbozi," alisema Mwamalala.

  Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Jeremia Mwakatumbula mkazi wa Mbozi aliyekutwa na kadi 10 za CHADEMA ambapo baada ya kuhojiwa alikiri kuzinunua kadi hizo kwa sh 10,000 kila moja.

  Mwingine ni aliyekuwa Katibu wa Mbozi Magharibi Joseph Kaminyoge aliyerudisha kadi ya CHADEMA mbele ya waasisi wa CCJ walioshindwa kukiendeleza, alidai kufanya hivyo kwa kuwa haelewani na viongozi hali iliyofanya asimamishwe uongozi, hivyo alikuwa akisubiri kuhojiwa.

  "Huyu mtu wiki mbili zilizopita alikwenda makao makuu ya chama kule Dar es Salaam kuomba kadi za chama kama kiongozi kwa kuwa alikuwa akisubiri kuhojiwa hivyo makao makuu hawakuwa na taarifa za kuhojiwa kwake alikabidhiwa kadi 100 alizowauzia CCM.

  "…Haitoshi akapanda jukwaani kujisalimisha kwa CCM kwani anajua aliyoyafanya ndani ya CHADEMA yasingeweza kuvumilika," alisema Mwamalala na kufafanua kwamba kitendo cha uongozi wa CCM mkoani hapa kutangaza kuwa wamepokea wanachama 397 kutoka CHADEMA si kweli.

  Kuhusu kuhama kwa diwani wa Nzovwe, Hezron Mwakalembo, ambaye hakuwepo eneo la mkutano wala kushiriki maandamano ya CCM alisema Nape alipigwa changa la macho na viongozi wake kwa kuwa hakuna ukweli katika hilo.

  Alipohojiwa na waandishi wa habari, Mwakalembo alishangazwa na taarifa za kuhamia CCM hivyo kuwataka viongozi wa chama hicho mkoani Mbeya wamwombe radhi kwa uzushi huo.

  "Ninachokijua ndugu waandishi ni kwamba niliandika barua ya kujiuzulu udiwani na kuipeleka kwa Meya wa jiji baada ya kumkosa mkurugenzi, hata hivyo kabla ya muda wa kuthibitishwa kufanya hivyo viongozi wangu wa chama waliniita na nikabadili uamuzi.

  "Baada ya hapo nikaandika barua nyingine ikiambatana na kiapo ambayo niliipeleka kunakotakiwa mapema kabla ya saa 48 yanayotambuliwa kisheria kupita," alisema Mwakalembo.

  Kwa upande wake mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Mjini, John Mwambigija, alisema kuwa endapo kikao cha madiwani kitakataa kumruhusu diwani huyo kuendelea na vikao kutokana na barua yake ya awali, wapenzi wa chama hicho wataandamana kupinga uamuzi huo kwa kuwa zipo taarifa za diwani huyo kuzuiwa kuingia kwenye vikao vya baraza.

  Habari zilizolifikia Tanzania Daima zimeeleza kuwa licha ya diwani huyo kuondoa kisheria barua ya kuachana na nafasi ya udiwani, Meya wa Jiji la Mbeya Athanas Kapunga alipoipata haraka akachukua hatua za kisheria ikiwemo kuipeleka kwa mwanasheria wa serikali na Katibu Mkuu wa Tamisemi.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Source: Tanzania Daima a.k.a gazeti linalomilikiwa na mwenyekiti wangu.
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280

  sita na mwakyembe nasing kabisa
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  hii inaonesha KING MAKER aka ROSTAM AZIZ alikuwa na nguvu kubwa sana ndani ya ccm. yaani kujivua gamba tu na ubunge hawa jamaa eti ndo wanafurukuta kwa vimaandamano uchwara!
   
 5. L

  LazaroSMtindi Senior Member

  #5
  Jul 18, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbona suala la CCJ linawasumbua zaidi CHADEMA kuliko CCM? Wanaodaiwa "kusalitiwa" hawalalamiki, CHADEMA inajiingizaingizaje huko kama siyo kukosa hoja? Hii inafanana kabisa na wana-CCM kulalamikia "maadili" ya Dk. Slaa as a leader of a major political party kumgeuza mke wa mtu kuwa "mchumba" na kumpa mimba in his 60s huku CHADEMA wakiwa hawana neno.
   
 6. J

  JajiMkuu Member

  #6
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 1, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sitashangaa kama Edo Mwamalala ni wale darasa la saba wanaojitokeza ghafla bin vu na digrii za internet na kujipenyeza kwenye vyama na kuukwaa uongozi. Badala ya hoja kujibiwa na hoja, Mwamalala goes for CCJ! Extremely cheap indeed!
   
 7. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #7
  Jul 19, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu hii avatar yako huwa inanifanya mimi nisitamani hata kusoma post zako. Tafadhari badilisha maana inatutisha si wengine. Imekaa kama jini au ya kichawi chawi fulani.
   
 8. opwa

  opwa Member

  #8
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 10, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uongo mwingine kwenye blog ya michuzi kuna pcha nape kamshka m2 anaitwa prince mwaihojo akidai ni katibu wa habari chadema mbeya. Ni kuudanganya umma mwaihojo alikuwa mgombea ubunge kwa tikeki ya cuf,nccr na tlp dhidi ya sugu na m.pesya. Leo wadanye wa2 eti wamevuna chadema mali za cuf. Nape kapunzke wilayani kwako utachoka utazeeka mapema ujekuwa **** kama 6 na magamba wengne
   
 9. Mpendwa

  Mpendwa Member

  #9
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimegundua nimuita huyu jamaa mkuu nitamuonea kwa sababu nahisi ana tope kichwani, siasa na private/persona issues issues wapi na wapi?? hizi ni kama swala la imani za ki freemason walionazo wana ccm ambalo hatutaki kulika hapa JF Mwenye mke yuko wapi na amechukua hatua gani hadi ivi sasa???la msingi ni kuweka mambo yanayoleta muskakabali (desitny) mzuri kwa taifa na si propaganda zisizo na maana. Jaribu kutafuta mahali watakapoku brush understanding yako, naona ipo chini mno
   
Loading...