Njombe: Mkuu wa Wilaya, Ruth Msafiri adaiwa kushusha na kuchana bendera za CHADEMA

Chadema imewafanya vibaya hawa watu maana benders ni nyingi wao wanashughulika na chadema 2015 hawataisahau
 
KWAKO NDUGU RUTH MSAFIRI, MKUU WA WILAYA YA NJOMBE

Salaam.

Nichukue nafasi hii kutoa masikitiko yangu kwako kwa kitendo chako cha kuamuru kuondolewa kwa Bendera zetu na kuzichana kwenye halmashauri ya Mji Mdogo wa Makambako kwa madai KUWA Bendera zetu ni takataka.

Huu ni ushamba wa MADARAKA na Chuki zisizo na tija kwa maendeleo ya wilaya yetu ya Njombe.

Ziko kero nyingi ambazo wewe Kama Mkuu wa wilaya ulitakiwa kuzishughulikia badala ya kuhangaika na Bendera ambazo Kimsingi hazikuongezei chochote kwenye CV yako zaidi ya kujenga Chuki na kujiandalia mazingira magumu ya maisha yako baada ya kunyang'anywa nafasi hiyo ambayo Kimsingi si mali yako ya kudumu.

Ndugu Ruth Msafiri nikukumbushe tu kwamba hiyo nafasi wamepita wengi kabla ya kuwepo kwako,wengine bado wako hai na wanatamani wangeendelea kubaki kwenye hiyo nafasi lakini imeshindikana na wengine tayari walishatangulia mbele za haki.

Nikukumbushe tena ndugu Ruth Msafiri kwamba iko siku hutakuwa tena na mamlaka ya kutoa amri hizi batili, hutalindwa tena na polisi ambao Leo wanakufanya ujione Mungu mtu.

Kitendo cha kung'oa Bendera zetu na kuzichana na kuziita takataka si cha kiungwana na ni kinyume na Katiba ya nchi hivyo nichukue nafasi hii kukutaka ujitathmini Kama unatosha kuwepo kwenye nafasi au upishe watu wengine Maana haya mambo ya kishamba unayoyafanya yanadhalilisha na kuitukanisha nafasi ya aliyekuteua ambaye Kimsingi hajui chochote Kama unafanya mambo haya.

Nashauri
Tafuteni namna nyingine ya kuwashawishi watu wakubaliane na mitazamo yenu kuliko kutumia nguvu ya vitisho ambavyo vitapelekea machafuko kwenye nchi yetu.

KUMBUKA BENDERA SIO WATU.

PAMOJA NA SALAMU ZA CHAMA
NDIMI
ROSE JOHN MAYEMBA
MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA NJOMBE
Mnawachekea

Ilitakiwa mfanye kitu Cha tofauti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani kuna maDC, kama huyu Ruth, wana uwendawazimu wa aina fulani. Sifhani kama Rais Magufuli anawaagiza wafanye huu uwendawazimu. Tatizo la Rais ni kuwavumilia baadhi ya watu aliofikiria kuwa ni wazima kumbe ni wendawazimu, kuendelea kuwa viongozi.

Rais inabidi asisite kuwaondoa viongozi wateule wake wanaogundulika baada ya uteyzi hawana akili sawasawa.
Lakini kumbuka yeye mwenyewe mkulu aliwahi sema kuwa yeye anateua wendawazimu, kama yeye mwenyewe, katika nafasi zake za uteuzi!

Hakika huyu mama ni dhahiri ni "mental case" aliongelea Mkulu katika uteuzi wake!
 
Katika nchi iliyostaraabika,na yenye kujari haki,usawa na democracy,hujenga tamaduni za kuheshimiana,na viongz wake husimamia haki zaid..
Kwa alichokifanya si haki,maana sheria yenyewe inapinga jambo hili
 
huu ujinga unabarikiwa na m\kiti wa ccm taifa ambaye kwa upande mwingine ndiyo rais alipaswa kwa nafasi yake ya mkuu wa serikali kupinga matendo yanayoenda kinyume na sheria.
 
Unajipendekeza kwa Boss hadi unapitiliza, njaa Mbaya sana, nawashauri CCM watu kama hawa wanawaharibia Chama nikuwatoa. M/kiti Shughulika na hawa watu wasikutafsiri tofauti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom