figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,481
TAARIFA KWA UMMA
UTEUZI WA WAGOMBEA UBUNGE EALA
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyokutana Zanzibar katika kikao chake cha siku moja, Mei 2, mwaka huu, imewateua wafuatao kuwa wawakilishi wa CHADEMA kugombea Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA);
1. Profesa Abdalla Safari
2. Salum Mwalim
3. Ezekia Wenje
4. Josephine Lemoyan
5. Lawrence Masha
6. Pamela Massay
Walioteuliwa watakamilisha hatua zingine za uteuzi kwa mujibu wa taratibu na Kanuni za Bunge na Uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki.
Imetolewa leo Jumatano Mei 3, 2017 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA