Makala Jr
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,395
- 1,110
Sherehe za uhuru wa "TANGANYIKA" zimedoda. Mitaani watu hawana habari kwani wanaona mafanikio ya uhuru yamekuwa neema kwa wachache huku wengi wakiachwa kwenye wimbi la ujinga,maradhi na umasikini kinyume na ilivyotarajiwa na waasisi wa uhuru mnamo tar.9.12.1961. Bila shaka yoyote, waasisi wa taifa la Tanganyika haswa Mwl.Nyerere waliweka misingi ya kujenga taifa lenye usawa,uzalendo,mshikamano na uchapaji kazi ili kuleta maendeleo ya uchumi kwa watu wote na kuinua hali ya maisha ya watu. Ashakum si matusi, CCM wakawa wana wapotevu waliorithi nyumba yenye misingi mizuri na kuanza kuibomoa.Ndipo miiko ya uongozi ilipofutwa na maadili yake, viwanda vikafa kwa sera mbovu na hata kilimo kusuasua. Leo hii CCM (Wajamaa) hunadi Kilimo Kwanza huku somo la kilimo katika shule zetu likipewa kisogo.CCM wako busy na CHADEMA na kusahau kujinadi japo kwa machache waliyofanya, wamepoteza dira!