CHADEMA ‘wateka’ Bunge; Wawapeleka puta mawaziri; Waondoa shilingi, CCM wawazidi ujanja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA ‘wateka’ Bunge; Wawapeleka puta mawaziri; Waondoa shilingi, CCM wawazidi ujanja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 11, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  *Ni Tundu Lissu na John Mnyika
  *Wawapeleka puta mawaziri
  "Waondoa shilingi, CCM wawazidi ujanja

  Na Waandishi Wetu, Dodoma
  [​IMG]

  WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu wa Singida Mashariki na John Mnyika wa Ubungo, mwishoni mwa wiki ‘waliliteka' Bunge wakati wa mjadala wa Hotuba ya Makadirio ya Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Rais Mazingira na Muungano. Hotuba hiyo iliwasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.

  Lissu na Mnyika walionekana vinara wa mjadala huo wakati Bunge lilipokuwa limekaa kama kamati kupitia makadirio hayo kifungu kwa kifungu.

  Dalili za wabunge hao kuteka Bunge, zilianza baada ya Lissu kusimama na kuomba utaratibu kwa aliyekuwa Mwenyekiti ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai.

  Katika hoja yake hiyo, mbunge huyo alihoji muda ambao mbunge anatakiwa kutumia anaposimama kutaka ufafanuzi wa jambo fulani.

  "Kanuni ya 150 ibara ya 4 inaeleza kuwa kanuni zitatenguliwa kwa madhumuni yaliyokusudiwa.

  ‘Wakati wa kupitisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, kanuni zilitenguliwa ili wabunge watumie dakika tatu wakati wa kuomba ufafanuzi, lakini kwa leo mbunge akisimama kutaka ufafanuzi anatakiwa aendelee kutumia dakika tano kama kawaida na siyo dakika tatu tena,' alisema.

  Baada ya kauli hiyo ya Lissu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, alisimama na kusema uamuzi wa mbunge kusimama na kutumia dakika tatu siyo wa kudumu bali ni wa majaribio ya muda mfupi.

  "Labda tu nimpe taarifa Mheshimiwa Mbunge kuwa mabadiliko hayo katika kikao chetu cha Kamati ya Uongozi ambacho kwa upande wa Kambi ya Upinzani waliliwakilishwa na Mheshimiwa John Mnyika, tulikubalina mabadiliko hayo yatumike katika siku za mwanzoni baadaye tutakuja ‘ku-revew' lakini hoja haikutaja mwisho itakuwa lini,"alisema Lukuvi.

  Baada ya maelezo hayo ya Lukuvi, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika aliomba kutoa taarifa kuhusiana na makubaliano yaliyofanyika katika kikao alichokitaja Lukuvi.

  "Katika makubaliano yetu hatukukubaliana kutokutoa hoja ya kutengua kanuni, kwa hiyo kama tunataka kuendelea na makubaliano yetu ilibidi tutoe hoja ya kutengua kanuni,' alisema Mnyika.

  Baada ya mvutano huo, Naibu Spika, Job Ndugai alitoa ufafanuzi kuwa uamuzi uliokubaliwa katika Kikao cha Kamati ya Uongozi ulikuwa wa muda mfupi na wiki ijayo kikao kitakaa tena kufanya tathmini ya utekelezaji wa mabadiliko hayo.

  Pamoja na maelezo ya Ndugai, Lissu aliomba mwongozo tena lakini Naibu Spika aliukataa na kuamuru kikao kiendelee.

  Wakati huo huo, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), alisimama kutaka ufafanuzi kuhusu viwanda vinavyotoa kemikali kali inayowaathiri wakazi wa Mikocheni Dar es Salaam.

  Mdee pia alihoji kama kweli Serikali ya Mapundizi Zanzibar iliiandikia barua Serikali ya muungano kuwa mafuta siyo ya muungano.

  Katika kifungu kingine, alisimama Lissu akidai serikali haipo tayari kuwaelimisha watanzania kuhusu muungano.

  "Serikali haipo tayari kukiri yale yaliyotokea wakati wa kuanzishwa kwa muungano. Waliokuwa viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakati huo wako wapi?

  ‘Mbona hamtaki kusema? Walipotea hivi hivi na haijulikani wako wapi!' alihoji Lissu.

  Akitoa ufafanuzi kuhusu hoja hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Hassan Suluhu, alisema watu waliotajwa na Lissu hata yeye hakuwahi kuwaona badala yake amekuwa akiwasoma katika vitabu.

  ‘Kama kuna watu walikufa wakati wa kuanzishwa kwa muungano walikuwa ni Wazanzibar. Tuliokaa kitako tukakubaliana kuhusu muungano ni Wazanzibar na kama walikufa kwa muungano tusilifanye jambo hili kuwa la siasa,' alisema.

  Baada ya mjadala huo mjadala mwingine ulioibuka ni baada ya wabunge hao kuhoji ni kwa nini Serikali imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Dar es Salaam badala ya Dodoma ambako ndiko yaliko makao makuu ya nchi.

  Hoja hiyo ilijibiwa na Kaimu Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, ambaye alisema fedha za ujenzi wa ofisi hiyo zimetengwa kukamilisha ujenzi kwa kuwa jengo limekwisha kuanza kujengwa na hakukuwa na sababu ya kuhamia Dodoma na kuacha jengo likiwa gofu.

  Pamoja na ufafanuzi huo, Mnyika alisimama na kuamua kuondoa shilingi katika bajeti ya wizara hiyo kwa kuwa alikuwa hakuridhsihwa na maelezo yaliyotolewa.

  Hata hivyo hoja yake ilipigwa mweleka baada ya Mwenyekiti kuwahoji wabunge na wengi ambao ni kutoka CCM kusema hawakubaliani na hoja ya mbunge huyo wa chama cha upinzani.

  Mjadala mwingine ulioonekana kutikisa Bunge na kutekwa na wabunge hao wawili huku Waziri Samia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk Terezya Huvisa wakiwa katika wakati mgumu wa kutetea bajeti yao ni kuhusu Sh milioni 420 zilizotengwa kwa ajili ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambazo wabunge hao walisema ni ndogo na haziendani na majukumu ya baraza hilo.

  Baada ya mvutano wa hapa na pale, Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene (CCM) alijitosa katika mjadala huo na kusema fedha zilizotengwa kwa ajili ya NEMC ni zaidi ya Sh milioni 420.

  Lissu alisimama tena na kupinga hoja hiyo na kuhoji mahali fedha hizo zilipoandikwa kwa kuwa katika bajeti zilikuwa hazionyeshwi jambo ambalo alisema anaondoa Shilingi katika bajeti hiyo.

  Kama ilivyotokea kwa Mnyika naye alishindwa baada wabunge wengi wa CCM kupingana na hoja yaje wakati walipoulizwa na Mwenyekiti.

  Pamoja na mvutano huo uliokuwa ukitawaliwa na wabunge wa CHADEMA huku wabunge wa CCM wakionekana kuwa wasikilizaji kwa asilimia kubwa, wabunge waliidhinisha makadirio ya bajeti ya ofisi hiyo.
   
 2. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  taarifa nzuri. CCM acheni hizo teteeni maslahi ya wananchi na si kusema ndiyoooooooooooo kwa kila hoja. historia itawahukumu!
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Maslahi ya taifa mbele na sio maslahi ya chama
   
 4. opwa

  opwa Member

  #4
  Jul 11, 2011
  Joined: Jun 10, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tanzania imewaamini na kuwapa dhamana kupitia CDM mkatetee maslahi ya watanzania woote.
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  kwa mara ya kwanza mtanzania wameandika habari ambayo ipo in fovour kwa CDM. Ni nadra sana kwa magazeti haya (Mtanzania, Uhuru, Mzalendo, Jambo leo, Hoja na habari leo) kukubali kwamba CHADEMA wanafanya vizuri.
   
 6. F

  Froida JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hao vijana ni miamba kwa kweli wanatufundisha kwamba 2015 hakuna kupeleka magarasa ya ndioooooooooooooooooo
   
 7. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Duuuuh binge hili kweli kazi mwenyekiti anaulizwa mahali pesa ilipo haonyeshi bali anauliza kama kuna umuhimu wa kuondoa shilingi?
   
 8. desertfish

  desertfish Member

  #8
  Jul 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Watanzania tukiacha uoga wa kuambiana ukweli tunaweza kuikomboa nchi hii. Tuna tabia ya kufuata mkumbo hata kama mkumbo huo unatuumiza sisi wenyewe. Wabunge wa CCM iokoeni Tanzania jamani, acheni kushabikia siasa.
   
 9. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  it is interesting. Baada ya muda, naamini na wabunge wengi wataelewa umuhimu wa kuweka mbele maslahi ya Taifa. Maana kwa sasa inaonekana CCM wapo bungeni kupinga hoja za chadema si kuihoji serikali kwa niaba ya wananchi.
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Jul 11, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Taratibu wabunge wote watabadilika!
   
 11. m

  mndeme JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2011
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 322
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  we waache tu magamba waendelee na ushabiki! maana hata wazir aki.jamba watasema wanampongeza na wanaunga mkono hoja. Funny
   
 12. p

  politiki JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  hii ndio inaonyesha wazi kuwa wabunge wa ccm wanawakilisha ccm zaidi bungeni badala ya wananchi wao waliowachagua.
  wanaunga mkono hoja siyo kwa mantiki yake bali ni kwa kuwa imeletwa na serikali ya ccm hivyo wanajiona kama wanawajibika
  kwa serikali badala ya wananchi wao waliowachagua. this is insane.
   
 13. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #13
  Jul 11, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Maslah ya CHAMA MBELE THEN TAIFA BAADAYE.......NDIO UTARATIBU WA TANZANIA
   
 14. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #14
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Ukiwa mccm lazima upelekwe "giningi" ulishwe unga wa ndele; nyeusi utaiona nyeupe, na nyeupe itaonekana nyeusi. Yaani, unakuwa zuzu au zezeta. Mwl. Nyerere (1995) aliwafananisha viongozi wa CCM na serikali yao na mazuzu;wanaobadilishiwa almasi halisi kwa vipande vya chupa. Mazuzu!
   
 15. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #15
  Jul 11, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  hata mwenyekiti naye zuzu. Yeye yuko pale kujipendekeza kwa ccm, sio kuchambua mantiki ya suala linalohojiwa. Ku'act' ukidume. Sioni kama ccm wanatoa mchango kuboresha hali ya mwananchi. Wanachofanya ni kujaribu kushusha haiba ya wabunge wa kweli wa upinzani, walio na maslahi kwa wananchi yaani CHADEMA, the people's power and selection.
   
 16. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #16
  Jul 11, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mwenyekiti wa Kikao Ndugu Job badala ya kutumia busara ili wapate kujua ukweli wa mambo kwa manufaa ya Taifa, yeye anatumia wingi wa mazuzu kupitisha madudu Bungeni! Kwa style hii hakuna maendeleo kwa kipindi hiki cha lala salama cha JK.
   
 17. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #17
  Jul 11, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Angalau wanasaidia hao washkaji wa mkuu wa kaya kutolala kwa kuwa CDM mara zote wana hoja nzito. Xllent& keep it up
   
 18. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #18
  Jul 11, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hii inatufundisha watanzania kwamba ili bunge lifanye kazi kwa maslai ya taifa na si ccm 2015 tuwachague wabunge wengi wa cdm ili mchezo mchafu wa ndiyoooo na siyoooo uishe
   
 19. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #19
  Jul 11, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Hiki kifungunkimepita CCM NDIYO, CHADEMA SIYO, CUF HATUJUI!!!!
   
Loading...