Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,939
- 6,849
Huo ni uamuzi wa Chadema. Unamzuia vipi Msajili wa Vyama vya Siasa kuendelea na kikao chake na IGP na vyama vingine? Mnahangaika nini na chama mfu kama Chadema? Hata Chadema akiwepo hoja zake hazitakuwa na uzito mbele ya vyama vingine zaidi ya 10 vitakavyokuwa upande wa Msajili na IGP!Eti Benson Kigaila ana sema hatuwezi kuhudhuria kikao cha Msajili hadi zuio la siasa kwanza liondolewe na pili eti Mbowe aachiwe mara moja.
kwa hoja hizo dhaifu ndipo nimeona kweli Viongozi wa Chadema wamepoteza mwelekeo kabisaa.
Hoja ya Pili ya kushinikiza Mbowe aachiwe huru ni kinyume kabisa na utawala wa sheria lkn pia kitendo au kauli hiyo ya viongozi wa Chadema inaingilia uhuru wa Mahakama kwa kuishinikiza Mahakama ifanye maamuzi kinyume na utaratibu wa kisheria.
Pili nendeni mkaonane na msajili kisha muwasilishe hoja ya kwa nn zuio la kisiasa? ni ujinga kulalamika nje ya kikao, nendeni mezani kwa Msajili kwani mnaogopa nini?! nendeni mkawasilishe hoja zenu.
Kesi ya Mbowe lazima iendelee, ndio maana yuko mahakamani, Mahakama ndiye muamuzi wa mwisho.
hoja ya Bensoni Kigaila ni ujinga eti Chama kisiendelee na shughuli zake za kawaida kwa sababu eti Mbowe hayupo!!!
Amandla....