CHADEMA watakiwa kupeleka majina tena kwa ajili ya uchaguzi wa EALA na Bunge

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
Kwa ufupi
Katika uchaguzi uliofanyika Aprili 5, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waliwachagua wajumbe saba wa EALA, huku wagombea wawili wa CHADEMA wakipigiwa kura ya hapana, hivyo kushindwa kupitishwa.


Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetakiwa kupeleka majina ya wagombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) muda wowote kuanzia sasa.

Katika uchaguzi uliofanyika Aprili 5, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waliwachagua wajumbe saba wa EALA, huku wagombea wawili wa CHADEMA wakipigiwa kura ya hapana, hivyo kushindwa kupitishwa.

Awali, kuliibuka mabishano ya kanuni kuhusu wagombea wa CHADEMA kuwa wawili pekee wakati nafasi kwa ajili ya chama hicho zilikuwa mbili.

Mkuu wa Kitengo cha Bunge cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Owen Mwandumbya alisema ofisi hiyo itapeleka tangazo kwenye Gazeti la Serikali kwa ajili ya kufanyika uchaguzi huo wakati huu mkutano wa Bunge la Bajeti ukiendelea.
 
Uchaguzi wa EALA hauna demokrasia maana CCM wanauwezo wa kukataa wajumbe wanaotaka kuwakilisha Tanzania kupitia vyama vya CUF na CHADEMA lakini vyama viwili hivyo vya upinzani havina uwezo wa kukataa kwa kura nyingi wajumbe wa CCM walioteuliwa na chama tawala kuwakilisha Tanzania ktk bunge la EALA.

Bora utaratibu wa kuchagua wawakilishi wa Tanzania ktk EALA ubadilishwe ili waliopendekezwa na CCM pia wapitie zoezi la kupigiwa kura na vyama vya upinzani tu na kama watapata kura nyingi za wapinzani wapitei wakawakilishe Tanzania na pia iwe hivyo hivyo wawakilishi wa upinzani wapimwe kwa kura na CCM tu.

Utaratibu uwe walioteuliwa na vyama vya upinzani wapigiwe kura kwanza na baadaye walioteuliwa na CCM wafuatie kupigiwa kura ili CCM wawe makini kutotumia wingi wao vibaya. Maana CCM wakikataa majina yote na ''vyama vya upinzani wanyonge'' pia wakikomoe CCM kwa kuwakata kwa kura nyingi.

N.B
Article 50 of the Treaty requires that EALA
[2] Nine from each member state. Members can be re-elected for a second term.

[3] The ex-officio Members include one Minister from each partner state responsible for East African Community Affairs (currently there are five Ministers), the Secretary General of the EAC and the Counsel to the Community. They may participate in debates but have no right to vote in the Assembly. The Ex-officio Members report to EALA on the implementation of the Treaty and any other issues of interest to the Partner States.

[4] Article 50 of the Treaty also requires that an MLA (a) is a citizen of that Partner State;(b) is qualified to be elected a member of the National Assembly of that Partner State under its Constitution; (c) is not holding office as a Minister in that Partner State; (d) is not an officer in the service of the Community; and (e) has proven experience or interest in consolidating and furthering the aims and the objectives of the Community.
Source: Mandate and Functions of EALA —East African Legislative Assembly
 
Mwendo ni uleule
yakirudi yaleyale watapata Hapana kuliko za mwanzo
Hapana wanajikomoa wenyewe maana mnapunguza idadi ya wabunge wa TZ ndani ya East Africa.
So zikija ajenda ambazo zinahitaji kupigiwa kura TZ itashindwa tu.
Mkipunguza nguvu ya TZ, mnapunguza nguvu ya serikali yenu ndani east africa, habari ndio hiyo!
 
Mwendo ni uleule
yakirudi yaleyale watapata Hapana kuliko za mwanzo
Kwa taarifa yako litaongezwa jina moja tuu na kwa masharti ya uchaguzi hapo ni lazima wapite wawili. Hakuna cha ndio au hapana bali unapigia kura watu wawili tuu. Mnajihangaisha sana lakini mchezo hamtauweza.
Nyie mlisha chagua wenu hao wakina Mnyaa ambao hata lugha ya bunge lile haiwezi ili akapige makofi tuu, sasa acheni majembe ya kazi nayo yachaguliwe sasa.
 
CHADEMA komaeni.
Pelekeni walewale.

1. Lawrence Masha
2. Ezekiel Wenje .

Muwe na msimamo ktk mambo yenu. Hii tabia ya CCM kuwachagulia viongozi muikatae kabisa.

Hao vilaza Dizaini za yule wa sanamu ya Diamond wabaki huko huko CCM.
 
Back
Top Bottom