Chadema wataka polisi imwachie Naibu Katibu Mkuu wao Mh Salum Mwalimu .

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,502
23,582
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimelitaka Jeshi la Polisi kutoa taarifa rasmi juu ya tukio la kukamatwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu na wanachama wengine na kuwaachia huru mara moja.
mwalim-1.jpg


Jeshi la Polisi mjini Mafinga, mkoani Iringa, linamshikilia Mwalimu baada ya kumkamata mchana wa leo Jumapili Desemba 16, alipokuwa akiwasili kuongoza kikao cha ndani cha chama mjini hapo.

Taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene, zimeeleza kusikitishwa kwao huku wakilitaka jeshi hilo kuwaachia huru mara moja kwa kuwa hawajaona kosa la wanachama hao.

“Tukio la kukamatwa kwa Mwalimu lilitanguliwa na kitendo cha askari takribani saba kumfuata na kumtoa ndani ya gari kwa nguvu bila kutoa maelezo yoyote ya sababu ya kufanya hivyo.

“Awali, takribani polisi 40 waliokuwa kwenye magari matatu wakiwa na silaha za moto walifika ukumbi wa Mamu ambapo maandalizi ya kikao hicho cha ndani yalikuwa yanaendelea, wakisema kuwa wameagizwa kuzuia kikao hicho na Mkuu wa Wilaya,” amesema Makene katika taarifa yake hiyo.

Aidha, amewataja wengine waliokamatwa pamoja na Mwalimu kuwa ni, Katibu wa Chadema Mkoa wa Iringa, Jackson Mnyawami na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (Bavicha), Mbeya mjini, Jailos Mwaijande ambapo wote wanashikiliwa Kituo cha Polisi Mafinga hadi sasa.
 
CCM wana vikao vya chama ambavyo vinaanza rasmi kesho lumumba, sio kosa na hawata kamatwa. Ni haki yao kufanya vikao hivo.

Ila upinzani wakifanya vikao vya chama, ni kosa na wanakamatwa. Sheria haiwaruhusu kufanya vikao.

*** Hata mtu asiekua na akili timamu (mwendawazimu) ataelewa kua huu NI UONEVU WA HALI YA JUU, uliovuka mipaka.

*** Serikali inachokitaka kutoka nchi za nje, itakipata safari hii, acha wajiuguze wehu. Maana hazijapita hata siku 3 toka EU na USA watoe tamko dhidi ya ukandamizwaji unaofanyika Tanzania, na kutoa WITO mabadiliko yafanyike. Leo wanafanya yale yale!!!! Kuwaonesha sisi ni JEURI!!!

*** Raia ndio tunapewa sababu za kuichukuia CCM na ukandamizwaji unaofanyika.

TUKUMBUKE Kuna viongozi nchi za wenzetu walikua na jeuri zaidi yetu, kwa kila kitu (Fedha na Silaha) ila baada ya kutekenywa waliishia kuzikwa.
 
EU na US nawachukia kwa LGBTI.
Mengine haya nawaunga mkono.
Naona somo Lao bado halijaingia akilini mwetu.
We need to rule ourselves as human beings, not as a slave and master relationship.
Not all opposition members are criminals, they are our fellow citizens too.
Dear God, have mercy on black race, stop injustice.
 
Ahh mm tangu saa nne mpk sahv nakandamizaaa leo hamna mishe
Alafu biashara na deals hazieleweki
Ndomana tunapiga tungi maana lzma tutafaakari kesho itakuwaje

Ova
Kesho Mungu ataibariki maana na Mimi nimepiga mpaka sioni kama nimelewa. Sijui wamepunguza kilevi?. Natamani niagize k v ila nipo mwenyewe na hana ndogo ndio najishauri.
 
Kesho Mungu ataibariki maana na Mimi nimepiga mpaka sioni kama nimelewa. Sijui wamepunguza kilevi?. Natamani niagize k v ila nipo mwenyewe na hana ndogo ndio najishauri.
Nmekunywa bia 8 Kabla ya bia nlikikata kisichana,nkaamiaa kwenye mzinga size ya kati cha kwanza tumekikata sahv tko cha pili tunachanganya na bia
Labda alcohol wamepunguza

Ova
 
Nmekunywa bia 8 Kabla ya bia nlikikata kisichana,nkaamiaa kwenye mzinga size ya kati cha kwanza tumekikata sahv tko cha pili tunachanganya na bia
Labda alcohol wamepunguza

Ova
Nimepata kampani nimeagiza muda usonge nikapumzike. Ingekua ule Uzi wetu ningetupiamo kapicha.
 
Hahaha kwani CHADEMA walitajwa kwenye report ya EU?! Kama hawajatajwa watakoma, hasira zitaishia kwao. UAMSHO wako gerezani kifungo cha maisha bila hukumu, naona CHADEMA wanaelekea hukohuko.
 
Hivi huyu salum si ni naibu katibu mkuu Zanzibar mbn naona anahangaikaga na Tanganyika tu?!
 
Back
Top Bottom