Chadema wataka madiwani waadilifu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,073
1,250
Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) kimesema hakitasita kuwachukulia hatua madiwani wake pale watakapobainika kuwa wanaongoza bila kufuata misingi ya utawala bora pamoja na kujihusisha na vitendo vya ufisadi.
Akizungumza na madiwani wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, alisema chama hicho hivi sasa kinafanya operesheni nchi nzima kwa lengo la kutoa elimu ya uongozi bora pamoja na kuwaelimisha kutambua majukumu ya kiongozi na kwamba elimu hiyo wanaitoa kwa madiwani waliochaguliwa kupitia chama hicho pamoja na wa vyama vya upinzani waliokubali kushirikiana nao.
Dk. Slaa alisema elimu hiyo wanayotoa itamsaidia kiongozi kupanga mpango kazi ambao utamsaidia katika kuongoza pamoja na kujali majukumu ya kazi pia kuepusha ubadhirifu ambao ni tatizo katika halmashauri nyingi nchini.
Aidha, alisema madiwani ndio jicho la wananchi katika kuwaletea mabadiliko ya uchumi kupitia rasilimali zilizopo katika kila eneo husika.
“Sisi Chadema tunataka diwani awe kiongozi wa wananchi na si kiongozi wa serikali na tunataka halmashauri zote zinazoongozwa na Chadema ziwe halmashauri za mfano hapa nchini,”alisema Dk. Slaa.
Mwenyekiti wa chama hicho mjini hapa, Charles Kaele, alimtambulisha Diwani wa kata ya Nyamatare Alex Kisurura kuwa ndiye aliyeteuliwa kuwa Meya wa Manispaa ya Musoma pamoja na Diwani wa Kata ya Kamnyonge, Angela Lima, kuwa ndiye aliyeteuliwa kuwa Naibu Meya.
Kaele alisema kuwa viongozi hao wamepita bila kupingwa kwa kuwa asilimia kubwa ya madiwani wa halmashauri hiyo wanatoka Chadema,ambapo manispaa ya Musoma ina kata 13 ambapo kata nane zilichukuliwa na Chadema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom