Chadema wataka kuinywesha serikali maji lakini wao mbona hawaachi chupa ya mvinyo?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Pamoja na JK kuwa ni mbambaishaji lakini kuna hoja moja angeliweka vyema machoni pa wapigakura pengine asingelihitai kuchakachua kura zetu na Uraisi wake tungeliukubali lakini utashi na hekima Mwenyezi Mungu hakumpatia..................

Hoja hii ya Jk ina uzito ya kuwa vyama vya upinzani ni fokopi lakini JK alishindwa kulijibu swali ya kwa namna ipi?

Jawabu hapa ni kwa kuiga katiba ya CCM kwa karibu nyanja zote.....na eneo ambalo linaiweka Chadema mahali pabaya ni katika eneo la kuunganisha kofia za kichama na serikalini.....yaani mbunge aweza kuwa na wadhifa ndani ya chama........huo ni UCCM na ungelikitegemea chama makini kingeliondokana na huo ukiritimba wa kuwarundikia wachache madaraka wakati watanzania wenye sifa wapo wengi...........

La pili, Chadema wanataka serikali iendeshwe kitaalamu zaidi yaani mawaziri wasiwe wabunge lakini wakirudi ndani ya chadema wabunge ni vibosile wa chama........

Jamani hapa siyo wankunywa mvinyo huku wakitaka serikali inywe maji?

Wajirekebishe wenyewe halafu kuirekebisha serikali itakuwa uji tu.....au niseme mboga tu...........
 
Una hoja lakini mimi umenichanganya. Kwani wapi duniani kuna clear demacations za hizo responsibilities? Kuna madhara yo yote ya hiyo arrangement? Ebu tusaidie sisi wengine
 
Back
Top Bottom