- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Na Mwita Mwija
Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika ameeleza kuwa kutokana na uhaba wa fedha, kwa sasa wagombea wote ngazo za mitaa, vijiji na vitongoji lazima wachangie kukiwezesha chama shilingi Laki nne (400,000) hii itasaidia uwezeshaji katika usimamizi wa chaguzi hizo kwa kuweka mawakala wa kusimamia zoezi hilo.
"Pia chama bado tunaendelea kutafuta wafadhiri wa kutufadhiri katika chaguzi hizi ili tuwe na nguvu kubwa na vigezi vyote watakavyo vitoa ili kutupa msaada huo wa kifedha tutavitimiza na hadi sasa tumemtuma Mhe. Tundu Lissu huko huko duni (nje ya nchi ) azungukie wadau na kutafuta fedha kwa masharti yeyote yale watakao yatoa tupo tiyari kuyatimiza na hadi sasa yuko mbioni kufanikisha hilo," amesema Katibu Mkuu CHADEMA John Mnyika, leo katika mkutano wake na waandishi wa habari.

- Tunachokijua
- Oktoba 17, 2024, Katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika alifanya mkutano na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine Mnyika amezungumzia Michakato ya uteuzi ndani ya Chama kuwa inapaswa kuanza mara moja na kutarajiwa kukamilika ifikapo oktoba 25, 2024.
Baada ya mkutano huu, limeibuka chapisho (post) linaloyosambaa mtandaoni likionesha kuwa limetengenezwa na Televisheni ya mtandaoni, Watetezi TV ambapo linahusisha maandishi ambayo yanadai kuwa John Mnyika amesema wagombea serikali za mitaa wa CHADEMA watachangia kiasi cha shillingi laki nne ambapo pia kumekuwepo na barua inayoonekana kuwa ya CHADEMA ikihusisha madai yanayofanana na hayo ikiwaelekeza matibu wa chama kanda zote kusimamia agizo la kuwachangia wagombea hao.
Ni upi uhalisia wa chapisho hili?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa chapisho hilo si la kweli kwani halijachapishwa katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za Watetezi TV. kadhalika chapisho hilo limebainika kuwa na utofauti wa mwandiko (fonts) katika kichwa cha habari ukilinganisha na mwandiko (fonts) ambao hutumiwa katika machapisho rasmi ya Watetezi TV.
Aidha JamiiCheck imewasiliana na msimamizi wa kurasa za Watetezi TV, Harith Jaha, ambaye amesema kuwa Taarifa hiyo siyo ya Kweli na ipuuzwe kwa kuwa haijaichapishwa kwenye kurasa rasmi za Watetezi TV.
Hata hivyo JamiiCheck pia imefuatilia mkutano wa John Mnyika na waandishi wa habari ambapo imebaini kuwa John Mnyika hakutoa kauli hiyo wakati wa mkutano huo uliofanyika Oktoba 17, 2024.
Kwa upande wa barua ambayo inadaiwa kutolewa na CHADEMA, JamiiCheck imebaini kuwa barua hiyo si ya kweli kwani haijatolewa na CHADEMA na haijachapishwa katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya chama hicho. Vilevile barua hiyo imebainika kuwa na mapungufu kadhaa ikiwemo kutokuwepo kwa nembo yenye rangi ya chama hicho badala yake uwepo wa logo yenye rangi nyeusi tofauti na barua rasmi za CHADEMA.
Barua na chapisho hilo vimehifadhiwa hapa na hapa.