CHADEMA wasiwachezee akili wapiga kura

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
CHADEMA, MMESHAKAA NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC)?

Habari za chini kwa chini tangu juzi nilisikia Chadema wameanza kutoa fomu za kumpata Mgombea ubunge wa jimbo la Siha na Kinondoni, siku amini taarifa hizo.

Leo nasoma mitandaoni nakutana na habari Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu amechukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Kinondoni. Makubwa haya!

Sote tunajua Chadema waliamua kususia chaguzi zote nchini kwa kutokusimamisha wagombea mpaka watakapokutana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili kujadili kasoro mbalimbali zilizojitokeza kwenye uchaguzi wa marudio wa kata 43 ambayo Chadema walipata kata moja tu.

Hata uchaguzi mdogo uliofuata ulioshirikisha majimbo 3 na kata 5 Chadema hawakushiriki kabisa kutokana na kutokukaa na NEC ili kujadili kero zao.

Leo hii wanapoamua kushiriki uchaguzi, kikao chao hicho na NEC walishaketi? Matatizo, madai na kero zao zimeshatatuliwa mpaka waamue kushiriki uchaguzi huu? Ni wapi na lini walitupa mrejesho juu ya madai yao yalipofikia mpaka wafikie hatua ya kuanza kushiriki uchaguzi?

Hawa wanaochukua fomu sasa ya kugombea wamepewa idhini ya kushiriki na Mbowe au na Chadema Kinondoni maana Mwenyekiti Mbowe alishakataa? Nani mwenye kauli ya mwisho Mbowe au Chadema Kinondoni?

Au wanataka kutuaminisha majimbo ya Songea Mjini, Singida Kaskazini na Longido hayakuwa na maana wala umuhimu kwao Chadema ndio maana hawakushiriki?

Kitendo cha Chadema kukubali kushiriki chaguzi hizi pasipo kukutana na Tume ya uchaguzi (NEC), pasipo kero zao kutatuliwa zinatupa majibu kuwa tatizo la wao kususia uchaguzi uliopita chanzo si NEC wala hakuna kero ya msingi wanayodai bali ni mambo yao binafsi, matatizo yao yamewafanya wasisishiriki.

Kama ni sababu zao binafsi ziliwafanya wasishiriki iweje wadanganye umma kuwa tatizo ni NEC? Iweje wawanyime haki ya kidemokrasia wanachama wao ya kuchagua na kuchaguliwa?

Chadema waache kuwachezea akili wapiga kura!! Kama hawajaketi na NEC na wameamua kushiriki, Chadema wajitokeze kwanza hadharani wawaombe radhi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Watanzania kwa kuwadanganya; Wawaombe radhi Wanachama wao kuwanyima haki ya kidemokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa; mwisho watengue kauli zao za uongo ndipo washiriki uchaguzi huu.

Kinyume na hapo Chadema watatuaminisha kuwa siku zote hawana madai ya kweli bali ni waongo. Wanatuaminisha kuwa siasa zao zimeegemea kwenye nguzo ya udanganyifu kwa Taifa. Na siku zote chama kilichojaa uongo na udanganyifu hakiwafai Watanzania wa sasa.

Na Shilatu E.J
Januari 19, 2018
 
CCM mlitegemea kujizolea mizoga kama ile ya Singida na Songea bila ushindani wowote eti mtu anashinda kwa 99.1% this time ujinga huo haupo.

Badala ya CHADEMA kuwaomba radhi kwanza CCM wanatakiwa wawaombe radhi wapiga kura wa Kinondoni na Siha baada ya kuwarudishia wapiga kura matapishi yale yale.
 
Uko sahihi kk Shilatu E. J. Chadema siku zote ni waongo sana. Hawasemii ukweli hata siku moja. Ndo maana wanaitwa Chadomo.
 
Mleta mada ukiambiwa ukweli kuhusu tabia yako utasema jibuni hoja kwa hoja. Sasa hoja gani uliyoleta kwenye bandiko lako? Wewe ni memba Wa siku nyingi Jf, kushiriki hoja za kitoto za akina Pohamba na Coco ni kujidhalilisha. Waliposusia uchaguzi uliopita ulikuja na lawama kibao humu, Leo wameshiriki umerudi tena na lawama. Au unatafuta uteuzi mpya mkuu? Taarifa zilizopo ni kwamba ulupoteuliwa awali ulivurunda, hebu rekebisha kasoro za uteuzi Wa awali ili uonekane upya.
 
asante mtoa mada umejitahidi kuweka details.na hiyo ndio heshima ya jf.mwalimu anatosha kinondoni kwani hana siasa za ushabiki na fujo.he is a factman always hana woga katika kuzungumza kweli.
Nb;angalizo paskal mayala ataicopy hii.
#bann_wahusike
 
Chadema tunaomba maelezo sisi wananchi juu ya hoja hizi,msipaniki mnapoambiwa ukweli mleta uzi kaeleweka tunaomba na nyinyi mueleweke
 
..kwa kinondoni na siha ccm msiweke wagombea mlionunua toka upinzani.

..haiwezekani mtu anajiuzulu ubunge, eti kwasababu anataka kumuunga mkono Raisi, halafu ghafla anageuka anagombea nafasi hiyohiyo kupitia ccm.
 
Back
Top Bottom