CHADEMA wasipopeleka wabunge bungeni watapata faida kubwa sana

Mkamanga junior

Senior Member
Jul 27, 2018
159
250
CHADEMA wakubali tu kupoteza hizi seat,waishi maisha magumu lakini watapata faida sana huko mbeleni.

Lakini wakikubali kuingia mtegoni ,wakapeleka wabunge bungeni,ndio habari yao imekwisha.

Kwa sababu nchi wahisani nyingi zimeonyesha nia ya kulalamikia faulo zilizochezwa, tutegemee mbinyo mkubwa wa kiichumi.

Hakuna nchi iliyofanikiwa kuvuka vikwazo bila kuomba poo na kurudi kwenye meza ya maridhiano,hata hao wanaosema tunaweza, kuishi bila wao,wanajisahaulisha.wafuatilie historia ya Rais wa Nicaraguay.
 
santesandy

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
1,256
2,000
Mimi Nafikiri kukimbia ni mbinu ambayo kwa miaka yote haijatusaidia sana! Umefika wakati wa kucheza nao game lao! Kwanza tupeleke wanawake mashujaa, pili tuanze kupandikiza watu wetu kila idara muhimu! Tupenyeze watu kwenye system yao wakakipasue chama huko huko kama wao walivyo leta wa kwao kina Lowasa! Tusipo tumia hii formula yao tutakua wa kupigwa kila mwaka!
 
Nguseroh

JF-Expert Member
Jan 18, 2020
1,112
2,000
Kuna huu msemo think twice before you act. Jiwe na genge lake wanaendesha maisha yao kwa kubahatisha bahatisha. Sijui kwasababu ya ugali wa bure wanaoshindilia magogoni?. It'll come a time very soon the free bread they are getting they will have to work for it. Hapo Akili ndipo itafunguka na walivyo hawana aibu wanaweza hata kwenda Burkina Faso ama central African Republic na Haiti kukopa hela
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
79,119
2,000
Mimi Nafikiri kukimbia ni mbinu ambayo kwa miaka yote haijatusaidia sana! Umefika wakati wa kucheza nao game lao! Kwanza tupeleke wanawake mashujaa, pili tuanze kupandikiza watu wetu kila idara muhimu! Tupenyeze watu kwenye system yao wakakipasue chama huko huko kama wao walivyo leta wa kwao kina Lowasa! Tusipo tumia hii formula yao tutakua wa kupigwa kila mwaka!
Nakupinga vibaya sana !
 
Bulaya001

JF-Expert Member
Dec 21, 2018
5,535
2,000
Huyo Aida wa Nkasi aunge tela huko huko CCM laasivyo atawagharimu wananchi wa Nkasi maana atatumika kama chambo kwa serikali kumtolea mfano, maana majimbo mengine yatapewa maendeleo kasoro lake ili uchaguzi ujao wapate cha kusema!!
 
santesandy

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
1,256
2,000
Nakupinga vibaya sana !
Nakuelewa, lakini ujue siyo kwamba nakubali dhuluma! Mimi natoa ushauri tu kwamba ninyi majembe kwasababu kuna hizi fursa chache muende kule mkakwamishe hata jambo moja tu baya walilo kusudia.

Alafu tuunge juhudi ‘kinafiki’ kama wao lakini kwa malengo! Hizi njia zetu zimebuma, tuwapige kwa game yao!

Tuwekeze kwenye taasisi zote nyeti! Kwa wananchi, people’s power, CHADEMA ni msingi, sijui oparesheni gani hayujafanya?! Tubadili mbinu!!
 
Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
2,437
2,000
Nakuelewa, lakini ujue siyo kwamba nakubali dhuluma! Mimi natoa ushauri tu kwamba ninyi majembe kwasababu kuna hizi fursa chache muende kule mkakwamishe hata jambo moja tu baya walilo kusudia. Alafu tuunge juhudi ‘kinafiki’ kama wao lakini kwa malengo! Hizi njia zetu zimebuma, tuwapige kwa game yao!
Tuwekeze kwenye taasisi zote nyeti! Kwa wananchi, people’s power, CHADEMA ni msingi, sijui oparesheni gani hayujafanya?! Tubadili mbinu!!
"Knee-me-war-sea-key-a mme-sir-how mna-cha-tea kwa sir-u-tea huku m-key-war laivu car-bee-sir!"
 
Mkamanga junior

Senior Member
Jul 27, 2018
159
250
Mimi Nafikiri kukimbia ni mbinu ambayo kwa miaka yote haijatusaidia sana! Umefika wakati wa kucheza nao game lao! Kwanza tupeleke wanawake mashujaa, pili tuanze kupandikiza watu wetu kila idara muhimu! Tupenyeze watu kwenye system yao wakakipasue chama huko huko kama wao walivyo leta wa kwao kina Lowasa! Tusipo tumia hii formula yao tutakua wa kupigwa kila mwaka!
Haitasaidia, ni kuwaachia bunge lao. Hii miaka mitano tutakapopata kibano akili itawakaa sawa,tusijidanganye tunaweza kuishi bila dunia. Fikiria Zitto alivyozuia tu fedha za wahisani trilioni kelele zilivyokuwa nyingi. Je fikiria sasa msaada yote ifungwe, mashirika na taasisi za nje waondoke,hata hao wabunge wenyew hawatakuwa na furaha.
 
August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
6,554
2,000
Kushiriki bunge hili ni sawa na kushiriki karamu ya kula nyama za watu-Chadema wasikubali uwendawazimu huo!
Kama kuna mbunge Yeyote wa "saccos" aliyeshindwa kwa kura za maruhani anaruhusiwa kwenda mahakamani, mbona hawaendi?? Na wazi wameshindwa kihalali ndio maana wamekaa kimya na kuishia kufunga cinema na kura wanazodai ni za "Raisi" ambazo ni "fake", mbona na si za "ubunge"
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom