CHADEMA wasipoe, ushindi uko karibu

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,677
2,000
Kwenye hii ishu ya katiba mpya na haki ya mikutano ya kisiasa iliyoko kwa mujibu wa katiba, kwa vyovyote vile Samia atakavyoamua kudeal na Chadema, Chadema bado wataibuka washindi.

1. Ni kwa faida ya legacy yake mwenyewe kutogeuka dictator
Kama angekuwa mwanafunzi mzuri wa hayati Magufuli, angejifunza kuhusu chuki kubwa ya wananchi dhidi ya yule mzee. Chuki hiyo ilitokana na uonevu, kutoheshimu sheria na uongo mwingi aliokuwa nao yule mzee. Sasa Samia naye kama anataka kuwa rais wa kuchukiwa na wananchi na kunyanyapaliwa akiwa nje ya madaraka basi aendeleze mtindo wake huu wa kutotenda haki kwa mujibu wa katiba!

2. Kutumia miguvu mingi kuzuia mikutano ya Chadema, pia kunawafanya wananchi wapate meseji ya katiba mpya
Samia na serikali yake wanajaribu kuzuia ujumbe wa katiba mpya na haki nyingine za kikatiba za vyama vya siasa kuwafikia watu wengi, lakini hata hiyo pia inabackfire, kwanza kupitia fujo ambayo serikali inawafanyia wapinzani wananchi kupitia taarifa za kukamatwa viongozi wa Chadema wanajenga interest ya kujua kinachijiri nchini, na hivyo ujumbe wa kutaka katiba mpya unawafikia. Lakini at the same time wananchi wanaiona serikali kuwa ni onevu, na hivyo kuwa sympathetic nao, kwa hiyo CHADEMA wanaua ndege wawili kwa jiwe moja!

3. Fujo za serikali dhidi ya wapinzani zinaifanya diplomasia yetu kwa wahisani kuwa ngumu
Samia anahitaji fedha ili kuwezesha kufanikisha programu zake, vyanzo vya ndani bya mapato havitoshi. Sasa matendo yake haya ya kutumia maguvu kuonea wapinzani yanaongeza ugumu wa kuonyesha kuwa serikali yake inaheshimu demokrasia. Hii inaweza kufanya asipewe pesa au acheleweshewe pesa. Kwa vyovyote vile hii haijakaa sawa kwake

4. Fujo za mara kwa mara za serikali dhidi ya wapinzani zitafanya shughuli za maendeleo kusuasua
Jeshi la polisi hata lifanyeje haliwezi kufanya kazi moja tu ya kuzuia wananchi kuenjoy haki zao za kikatiba. Iwapo Chadema hawatapoa, ina maana resources za hili jeshi ikiwemo rasilimali muda na rasilimali fedha zitakuwa zinatumika tu kufanikisha fujo za serikali dhidi ya raia wake. Hii ni counterproductive kwa sababu fujo hizi za mara kwa mara zitakuwa zinadisrupt shughuli za wananchi, wananchi watakasirika maisha yao kuvurugwa na kwa kuona operation za mara kwa mara kuzuia wapinzani kutumia haki yao ya kikatiba kufanya siasa, na serikali itawekwa kikaangoni iwaache wapinzani kufanya mikutano ambayo ni haki yao

5. Hizi fujo za serikali dhidi ya wapinzani zitatishia hata wawekezaji
Iwapo Chadema wataamua kutopoa, iwapo wataamua kufanya mikutano licha ya kuzuiwa mara kwa mara, na iwapo polisi wataendelea kuwafanyia fujo, basi hata mazingira ya uwekezaji nchini hayatakuwa rafiki. Malengo ya Samia kuvutia wawekezaji hayatatimia, na atajikuta ndoto zake za "uchumi kwanza" zinayeyuka.

Ushauri kwa Chadema.
Wasipoe! , wasipoe! , Wasipoe! . Kuzuiwa kwa mkutano mmoja iwe ni mwanzo wa maandalizi ya mkutano mwingine. Ukisitishwa mmoja, uitishwe mwingine na viongozi wawe thabiti katika hili.

Wakipoa, huu utakuwa mwisho wa chama chao kisiasa.

Viongozi wa Chadema wawe tayari kusacrifice.
 

Mkongwee

JF-Expert Member
Jul 29, 2018
362
1,000
hahahahaha
sasaa mbona hawapambani na kyombo kya dola
tuone mtifuanoo liveee
 

Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
4,641
2,000
Samia ni mstaarabu sana ila CDM ni wakorofi! Walimtukana sana Kikwete pamoja na kuwabeba sana, wakaja kumtukana Magu, now Samia hata miezi mi4 hajamaliza wameshaanza kumtukana tena! Kwa nini wagombane na marais wote 3?

Ukiwa mtu unayegombana na kila mtu watu wataanza kukushangaa wewe! Rais kaingia kipindi ambacho dunia nzima imechanganyikiwa na suala la Covid, uchumi dunia nzima umeyumba, nyie hata miezi 4 hajamaliza mnataka katiba, na mnaitaka kwa nguvu, vitisho na kejeli juu! Hata ningekuwa mimi nisingekubali hiyo kitu, mmeambiwa msubiri hamtaki!! Nyie ni watu wa namna gani?

Kinachotokea ni kwamba mnafosi Rais kufanya maamuzi ambayo hayakuwa kwenye plan zake. The good thing is wananchi wamewapuuza, wamebaki wapiga kelele wachache mitandaoni ambao hawana impact yeyote
 

Mkongwee

JF-Expert Member
Jul 29, 2018
362
1,000
l0m.mmmml.m}0)/.0,,

Badala ya kujiiliza kwa nini hawapambani na vyombo vya dola, jiulize kwa nini vyombo vya dola vinaminya haki za kikatiba za wananchi?
hahahahaha mambo hayo nilishaga jiuliza zamaaniii
ila kwa sasaaa
inshuuu za wanasiasaa ngoja tuwaache wenyewee wamalizaneee
 

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
7,799
2,000
Samia ni mstaarabu sana ila CDM ni wakorofi! Walimtukana sana Kikwete pamoja na kuwabeba sana, wakaja kumtukana Magu, now Samia hata miezi mi4 hajamaliza wameshaanza kumtukana tena! Kwa nini wagombane na marais wote 3?

Ukiwa mtu unayegombana na kila mtu watu wataanza kukushangaa wewe! Rais kaingia kipindi ambacho dunia nzima imechanganyikiwa na suala la Covid, uchumi dunia nzima umeyumba, nyie hata miezi 4 hajamaliza mnataka katiba, na mnaitaka kwa nguvu, vitisho na kejeli juu! Hata ningekuwa mimi nisingekubali hiyo kitu, mmeambiwa msubiri hamtaki!! Nyie ni watu wa namna gani?

Kinachotokea ni kwamba mnafosi Rais kufanya maamuzi ambayo hayakuwa kwenye plan zake. The good thing is wananchi wamewapuuza, wamebaki wapiga kelele wachache mitandaoni ambao hawana impact yeyote
Nitajie tusi ambalo Chadema wamemtukana Mama mpaka sasa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom