CHADEMA wasipo kuwa makini yanaweza ya kawapata kama ya NCCR ya Mrema 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA wasipo kuwa makini yanaweza ya kawapata kama ya NCCR ya Mrema 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tukundane, Jun 8, 2012.

 1. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,312
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Cdm ni chama ambacho kimetokea kupendwa na wananchi wengi hasa vijana na wasomi wengi hivyo kuaminika kuwa huwenda ndio chama pekee chenye wasomi wengi kuliko chama chochote tz na kimekuwa tishio kubwa kwa ccm.

  Kutokana nakupata wanachama wengi vijana wa mijini, vijijini, wazee na umati mkubwa unaohudhuria mikutano yao imejengeka imani kwa baadhi ya wanacdm kuwa wanaweza kuishinda CCM kirahisi wakati si kweli.

  Ieleweke kwamba wapenzi wengi wa cdm ni vijana walioko shuleni na wengine ndio wamehitimu elimu zao hivyo walio wengi hawana shahada za kupigia kura. Kinachotakiwa kwa cdm ni kuhakikisha kuwa wafuwasi wao wanajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura pindi mda utakapo fika hadi vijijini.

  Kuwa na wapenzi wengi kwenye chama na umati mkubwa kwenye mikutano yenu bila kuwa na wapiga kura hakutoshi kuiondoa CCM madarakani. Ambayo haiko tayari kuachia madaraka kizembe. Bila hivyo CHADEMA watajikuta wanalambishwa mchanga na CCM ambayo ina mtaji mkubwa wa wazee na kutoka vijijini kama ilivyo fanywa NCCR ya Mrema.
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Usifananishe NCCR ya Mrema na CDM au nenda Arumeru utajifunza kitu...
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wewe hauko Tanzania.

  Wazee gani na vijiji vya wapi unaposema ni mtaji wa ccm kuishinda CHADEMA?

  Hao vijana wasiokuwa na shahada za kupigia kura umewaona wapi?

  Btw, CHADEMA ni chama kilicho makini sana, siasa zake hazifanani katu na siasa za NCCR iwe ya Mrema ama ya Mbatia.
   
 4. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  We mleta thread ni Mbwiga na kilaza mkubwa! Hebu tutolee ujuha wako hapa. Ebooooo!
   
 5. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  kwa taarifa yako hata daftar la wapiga kura mwakani linaweza likajaa watu zaid ya mil 42 kwa sababu watu wanataka mabadiliko upo?
   
 6. B

  Bob G JF Bronze Member

  #6
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe wanafunzi hasa wa chuo hawapigi kura, kazi yao kubwa ni kulalamika na kunung'unika tu angalia hivi majuzi uchaguzi wa DARUSO hawapigi kura.

  Mi nashindwa kuelewa inaelekea elimu bado haijawakomboa, maneno tu, CHADEMA wachukue tahadhari sana na hawa wasomi wa vyeti na wasiojiandikisha na wasiopiga kura
   
 7. S

  SJUMAA26 JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 611
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  No, CDM wachukue tahadhari sana na Tume ya Uchaguzi yenye wasomi wa vyeti na wasiotumia maarifa na uaminifu wakati wa kuendesha zoezi la kupiga kura!
   
 8. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mkuu, naomba usiishie kwenye mitandao peke yake, cdm wanahamasisha sana watu wajiandikishe kupiga kura wakati wa kuboresha daftari ukifika. Kwa thread hii, unajionesha wazi kwamba hujawahi kwenda kwenye mikutano yao!
  Mwisho naomba nikukumbushe tu kwamba, huna haja ya kusubiri cdm kuhamasisha vijana au yeyote akajiandikishe. Kama unataka mabadiliko ya kweli kwa nchi yako, chukua jukumu hilo kwa kuhamasisha marafiki, ndugu, wake, watoto, jamaa na washkaji zako wakajiandikishe kupiga kura na kuzitunza shahada zao!
  Ni hayo tu!
   
 9. Suzie

  Suzie JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 1,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Usifananishe na 2010 ambayo kweli watu waliamini hata wakijiandikisha ccm itachukua, lakini kwasasa wameerevuka tathmini ya kwanza ni juhudi tunazozifanya kwenda kwenye mikutano ya CDM, na uhamasisho kwenye midahalo ya moja kwa moja fb na hata forum kama hii
   
 10. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  mleta hoja, kwa kadri ya uelewa wangu,kaleta angalizo la kifalsafa kwamba adhaniaye amesimama aangalie asianguke na tena CDM tusibweteke tuzidishe mapambano maana CCM wanarusha mateke kama ya mbogo au farasi aneyeelekea mautini,ni pigo la hatari hilo.
  Big up,falsafa hii ifanyiwe kazi kuelekea 2015
   
 11. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mwaka unaoutaja hakukuwa na nccr bali kulikuwa na mrema na ccm na kama si mwalimu ccm ilishakula mwereka wa mrema.
  kumbuka mwalimu aliiokoa ccm mdomoni mwa maalim seif.
  2015 wakamfufue mwalimu aje awachomoe tena katika meno ya chadema.
   
 12. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,312
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Hii kali mtu anae kupaushauri wakukuwezesha wewe kushinda anakuwa **** ukae ukielewa kuwa palipo na ushindani hata kushindwa kupo isipokukuwa hutakiwa kukiri kushindwa ilikuepuka kumpa adui yako nafasi.tz hii ni kubwa kama hayaniliyo yaeleza kwako hayapo basi niliko nimeyaona siyo vizuri kushikilia moja tu la ushindi bila kuendelea kuuongezea mbinu ushindi huo unao utafuta vinginevyo utajikuta unashindwa na adui ulie kuwa unategemea kumshinda.mtu anapotoa ushauri haina maana kuwa haitakii mema cdm la asha ninamna tu ya kujaribu kuliokoa taifa letu.kwani wengi tumepigika tunahitaji ukombozi wa kweli.
   
 13. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,312
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Hii kali mtu anae kupaushauri wakukuwezesha wewe kushinda anakuwa **** ukae ukielewa kuwa palipo na ushindani hata kushindwa kupo isipokukuwa hutakiwa kukiri kushindwa ilikuepuka kumpa adui yako nafasi.tz hii ni kubwa kama hayaniliyo yaeleza kwako hayapo basi niliko nimeyaona siyo vizuri kushikilia moja tu la ushindi bila kuendelea kuuongezea mbinu ushindi huo unao utafuta vinginevyo utajikuta unashindwa na adui ulie kuwa unategemea kumshinda.mtu anapotoa ushauri haina maana kuwa haitakii mema cdm la asha ninamna tu ya kujaribu kulikoa taifa letu.kwani wengi tumepigika tunahitaji ukombozi wa kweli.
   
 14. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  unajuaje? au umetoka kwa Sheik Yahya?
   
 15. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  usiogope, huu moto ni mkubwa.
   
Loading...