Chadema wasipo kuwa makini 2015 CCM huwenda wakapeta kiulaini. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wasipo kuwa makini 2015 CCM huwenda wakapeta kiulaini.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kazuramimba, Jun 14, 2011.

 1. k

  kazuramimba Senior Member

  #1
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kiukweli mimi nimekwisha choshwa kabisa na hawa CCM yaani sina hamu nao hata kidogo.Nimekuwa nikiwaona CDM kama mkombozi wa hili jahazi ambalo linakaribia kuzama.Lakini nimeanza kupata wasiwasi kuwa huenda hadi tutakapo fika 2015 Chadema ikajikuta haina jipya kwa wananchi. Tuweni wakweli maandamano ya CHADEMA hasa kanda ya ziwa yalikuwa yakipinga malipo ya DOWANS hili ni kosa kubwa sana ambalo CDM walifanya nionavyo mimi walitakiwa wapinge kila kitu hadi mitambo ya kampuni hii ya kifisadi sasa magamba wamewapiga kanzu kwenye kuminanane wakiwa hawajui la kufanya huku Bi clinton akifunga goli kwa kisigino sasa hatutakaa tusikie jina la Dowans tena!lakini pia swala la katiba limekua kama ajenda ya CCM wamejidai wanalishuhulikia huku wakija na miswada japo kuwa imekuwa hairidhishi . Si ajabu CCM Wakaanza kuwajibishana wakati huohuo tukasikia mapacha watatu wakijiuzulu kama alivyofanya makamba! Nionavyo CCM wamesha anza kujibu hoja za chadema kimyakimya na taratibu wameanza kujitoa kwenye mashimo waliokuwa wamejitumbukiza CDM wasiposhtuka 2015 watajikuta hawana pakusimamia.sijui nyie mnasemaje.
   
 2. L

  Lua JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  We 2lia ucwe na haraka kama mko....., chadema wanaakili kuliko unavyofikili, sasa wanadeal na bajeti huku wakikusanya makombola ya dowans, siku zote mtaka mawili moja humponyoka.
   
 3. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Si rahisi kama unavyofikiri.Jamaa nao wana akili mbadala.
   
 4. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #4
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  tunakusanya dokoment kwanza huwezi kukurupuka tu. Unaweza fungwa maisha. Tunaendelea kukusanya information za symbion power. Na kazi inaendelea vizuri.
   
 5. k

  kazuramimba Senior Member

  #5
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hiyo akilimbadala ndo ipi? Hoja ya kupinga posho nayo imeshachakachulia kiaina.Nionavyo CHADEMA hawajajua la kuishinda CCM.
   
 6. suleym

  suleym JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,716
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  hata wewe unaonekna umekaa kimbadala na magamba!
   
 7. f

  fazili JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,192
  Likes Received: 404
  Trophy Points: 180
  Eee bana mwaka 2015 sio mbali lakini hata hivyo bado miaka 4 hivi tufike huko. Nchi hii kuna mambo mengi yanayojiri kila siku kwa hiyo lazima kutakuwa na mabo mengi tu ya kuhamasisha. Hayo cdm wanayoyapigania kwa sasa ni machache tu yapo mengi mengine na yataendelea kuibuka kila kukicha. Pili fahamu kuwa watanzania wa sasa sio wale wa miaka ya 90. Watu wamebadilika sana na wanaufahamu zaidi ya wakti ule kwani hata media siku hizi ni pana uelewa ni mkubwa tu. Hata CDM wakibadili uongozi wa juu bado chama hiki kipo mioyoni mwa watu. Ujue kwamba watu wengi wameshachoshwa na CCM. Pia hakuna chama kilichowahi kabaki madarakani kwa nusu karne katika historia lazima watu watataka mabadiliko tu siku moja. Cha msingi tu ni kwamba watu inapaswa waeleweshwe ili wawe na msingi imara wa kwanini wanapenda cdm, je ni ajili ya dr Slaa, Mbowe, Zitto, Mnyika, .........? kama watu wanapenda cdm kwa sababu tu ya watu hawa basi cdm yaweza kusambaratika pindi watu hawa wachache watakapo sambaratika.
   
 8. MAYOO

  MAYOO JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hizo ni ndoto za alinacha, ccm kwisha habari yake. Jk hawezi kutawala nchi hii hadi 2015 bila vimbwanga vya ajabu wewe. Utajionea subiri
   
 9. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,640
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  usiwaunderestimate cdm hata kwa nukta.. u will be suprised
   
 10. M

  MAURIN Senior Member

  #10
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CHADEMa ni chama cha ukombozi wa mtanzania,wanatumia akili nyingi kuliko effort hawakurupuki hata siku moja na wala hawabahatishi,na watanzania wenye uchungu na nchi yao wapo nyuma yao,ANGUKO LA CCM LIMETIMIA
   
 11. M

  MAURIN Senior Member

  #11
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo unafurahia dhuruma inayofanywa na CCM dhidi ya watanzania maskini?CCM haina hoja ya kushindana na CHADEMA mana wao kila kitu ndiyoo,uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana,wingi wao bugeni unafanya kila ovu kupitishwa,ila ANGUKO LAO CCM LIMETIMIA
   
 12. z

  zamlock JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  wataondoka tu
   
Loading...