Elections 2010 Chadema wasilisheni pingamizi la kutangaza matokeo mahakamani

Joss

JF-Expert Member
May 28, 2009
765
191
Kwa mujibu wa katiba yetu,mshindi wa nafasi ya urais akitangazwa hakuna chombo chenye mamlaka ya kuhoji.Kwa namna hiyo basi nawashauri viongozi wa Chadema,kama sheria inaruhusu wawasilishe pingamizi mahakamani juu ya usitishwaji wa kutangaza matokeo halafu wafungue kesi ya uchakachuaji wa kura.Naamini kwa muda wote tangu kukamilika kwa majumuisho ya kura kwenye majimbo watakuwa wamekusanya ushahidi wa kutosha kuhusiana na uchakachuaji.

Ushahidi mwingine unaweza kuwa wazi kwa kuwa fomu zote zilizosainiwa na mawakala pamoja na wasimamizi zipo.Pia yaweza angalia idadi ya wapiga kura kutofautiana na matokeo yanayotolewa na NEC.
Chondechonde,msituangushe wapiga kura maadam mmeyakataa matokeo na mnatakwimu zote basi mwende mbele.Sisi tupo nyuma yenu.
Jumuiya za kimataifa zimekuwa na upofu katika kufanya tathimini halisi ya uchaguzi na jinsi umafia wa uchakachuaji ulivyofanyika hivyo naomba sana tusiwategemee kutoa tamko lolote.

Mungu awe pamoja nasi !!!!
 
Halafu huyu kikongwe L. makame anaulizwa swali kuhusu matokeo yanayotangazwa na tume kutofautiana na kwenye majimbo yeye anajibu wanatangaza matokeo waliyohakiki, Je kuhakiki ni pamoja kuwapigia kura upya kwa kubalidlisha haya kwenda kule na haya huko? Mimi Tanzania tuko shida kubwa sana ya demokrasia under, ndo mana hata watu hawajotokezi kupira. it is ridiculous, watanzania kupiga kura halafu mjinga mmoja au kikundi kubadilisha maamuzi yaliyofanywa na wapiga kura
 
Kwa mujibu wa katiba yetu,mshindi wa nafasi ya urais akitangazwa hakuna chombo chenye mamlaka ya kuhoji.Kwa namna hiyo basi nawashauri viongozi wa Chadema,kama sheria inaruhusu wawasilishe pingamizi mahakamani juu ya usitishwaji wa kutangaza matokeo halafu wafungue kesi ya uchakachuaji wa kura.Naamini kwa muda wote tangu kukamilika kwa majumuisho ya kura kwenye majimbo watakuwa wamekusanya ushahidi wa kutosha kuhusiana na uchakachuaji.

Ushahidi mwingine unaweza kuwa wazi kwa kuwa fumu zote zilizosainiwa na mawakala pamoja na wasimamizi zipo.Pia yaweza angalia idadi ya wapiga kura kutofautiana na matokeo yanayotolewa na NEC.
Chondechonde,msituangushe wapiga kura maadam mmeyakataa matokeo na mnatakwimu zote basi mwende mbele.Sisi tupo nyuma yenu.
Jumuiya za kimataifa zimekuwa na upofu katika kufanya tathimini halisi ya uchaguzi na jinsi umafia wa uchakachuaji ulivyofanyika hivyo naomba sana tusiwategemee kutoa tamko lolote.

Mungu awe pamoja nasi !!!!
Nakuunga mkono ikiwezekana ifanyike kesho kabla ya Ijumaa vingenevyo yakisha tangazwa itakuwa ngumu sana kupeleka mahakamani.
 
Chadema wafanye haraka sana na kuomba amri ya kupinga matokeo kutangazwa mpaka zoezi zima la kuhesabu kura litakapofanywa kwa mujibu wa sheria.
 
Back
Top Bottom