Chadema Washukuru Wananchi kwa Ushindi Udiwani Kiwira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema Washukuru Wananchi kwa Ushindi Udiwani Kiwira

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lawkeys, Apr 8, 2012.

 1. Lawkeys

  Lawkeys JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 1,110
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nipo Kiwira sasa na nimepata nafasi ya kukutana na watu walionusa harufu ya mabomu ya machozi wiki iliyopita katika uchaguzi mdogo wa udiwani ulioipa CDM ushindi wa kishindo. Nimepata habari ambazo nahisi ni muhimu umma ukafahamu kuhusiana na uchaguzi huu.

  Toka nikiwa safarini kutokea Dar nimewasikia awtu wakiwa na hamasa ya hali ya juu wakizungumzia uchaguzi huu. Hamasa zaidi nimeishuhudia kwa vijana na wazee wakifurahia ushindi huu utadhani matokeo yametoka jana. Taarifa za msingi usizozijua:

  (1) Bodaboda walipewa na CCM lita Mbilimbili za Mafuta

  Vijana wamiliki wa bodaboda walijaziwa mafuta ili wahudhurie kwenye kampeni za CCM. Vija walipokea mafuta wakaenda kwenye kampeni za CDM huku wakikumbushana kwamba lita mbili zinawakilisha vidole viwili alama ya CDM na hata siku ya uchaguzi kauli mbiu iliendelea vivyo hivyo waliendelea kuonesha kidole gumba mbele (dole) kwajili ya kupokelea salio CCM lakini nyuma walificha vidole viwili kwaajili ya kupigia kura.

  (2) Ana Kilango na Wanawake wa Kiwira

  Inasimuliwa kwamba Ana Kilango aliwakusanya wanawake katika jengo la Bank Kata (Saccos) linaloendelea kujengwa ili kuwapatia kishika uchumba na CMM kwajili ya kura kesho yake. Inasimuliwa zaidi kwamba Ana na wenzake walipitia mlango wa nyuma kwa kubomoa bati fence ya mabati inayolizunguka jengo hilo.

  Wakiwa wamenza kugawana pesa, inasimuliwa kwamba kuna mtu kutoka ndani ya kikao hicho haramu alitoa taarifa kwa Kamanda wa CDM ambaye alisambaza taarifa kwa Makamanda ambao walisabisha mamia ya wananchi kuizingira nyumba hiyo wakizuia Ana na wengine kutoka ili Takukuru waje kuifanya kazi yao. Ili kuzuia aibu hii Ana na wenzake waliwasiliana na RPC ambaye alikuja na vikosi vya FFU na kuanza kupiga mabomu kiholela. Mzee mmoja amanbaye alikuwepo eneo la tukio anasema alimwambia RPC kwamba anaamini kwam ba RPC atakuwa shahidi wa ukweli wa jambo hili. Baada ya wananchi kukimbia Ana na wenzake walipata upenyo wakaondoka. Chakusikitisha ni kwamba kituo cha ITV katika taarifa ya usiku siku hiyo walitoa muda wa hewani kwa Ana ili apotoshe ukweli wa tukio hili. Makamanda waliendelea kupambana kwa kuzuia barabara mpaka Polisi walipoamua kuondoka.

  Ili kuthibitisha habari hii nimeambiwa na kada wa CCM kwamba yeye alikuwa ndani pamoja na Ana na wengine wakigawiwa pesa. Anasema kywamba walichanganyikiwa Makamanda walipowazingira. Anasema kwamba hali ilikuwa mbaya zaidi pale ambapo walikuwa wakijitahidi kudanganya kwamba kilikuwa ni kikao cha kawaida cha ndani cha chama, wakati huohuo wakinamama wengine walikuwa wanapayuka kwamba, "mimi nimepewa 10000/= ma mwingine mimi nimepewa 15000/=" kada anasema hali ilikuwa tete sana. Cha kusikitisha ni kwamba sijapata taarifa zozote za Pccb kufanya kazi yao juu ya hili.

  (3) Maboksi ya Kura ya Kamatwa

  Alfajiri ya siku ya kupiga kura,nimesimuliwa kwamba, gari ya halimashauri ya Rungwe ilikamatwa na Makamanda ikiwa na maboksi yaliyo na kura za CCM. Makamanda walitoa kichapo kwa dreva, wakanyang'anya funguo za gari na maboksi yakapelekwa kituo cha polisi. Lakini cha kusikitisha sijapata taarifa ya hatua za kisheria zilizochukuliwa.

  Ushauri kwa wazalendo, sio lazima kufungua malalamiko kupitia polisi kwani unaweza ukapeleka maelezo yako moja kwa moja mahakamani. Kwahiyo mtuhumiwa na maboksi katika kesi hii yangepelekwa mahakamani. Zaidi ya hapo chukueni hata kwa simu ushahidi wa video za matukio ya uharifu wa namna hii. Mkishitaki polisi au mahakamani ikashindikana ugeukieni umma kupitia midia, kwani ni rahisi na gharama nafuu, upload hiyo video kwenye youtube, fb, twitter, jf na uwaache wananchi wachukue hatua 2015.

  (4) Piga Kura Linda Kura

  Naambiwa kwamba katika kipindi chote cha Kampeni Makamanda kutokea Tunduma na Mbeya mjini walikua wakipata taarifa ya uchakachuzi wanamwagika kama umande. Walisafiri umbali mrefu kwa gharama zao binafsi. Wengi walitokea Mbeya mjini na Tunduma. Na siku ya kupiga kura ninaambiwa Makamanda waliagiza katika vituo korofi kura zipigiwe nje ya nyumba na wanawake hawakuruhusiwa kujitanda kanga kwani inasemekana zinatumika kufichia kura. Na baada ya kupiga kura, kura zililindwa.

  (5) Mazishi ya CCM

  Ukweli ni kwamba kwa jamii za watu wa Mbeya msiba ni kitu cha heshima ya juu sana na ni chachu ya kuwaleta watu pamoja. Sasa siku moja kabla ya kabla ya uchaguzi Wapenzi wa CDM walitengeneza jeneza kisha wakaivalisha kofia ya CCM huku wakiigiza kulia wakiwa wamebeba mahindi, maharage, mikeka kama inavyokuwa katika msiba wa kawida. Walikuwa wakiimba, "nani kaua? CDM". Na baada ya mazishi walikula kande ambazo walizipika wenyewe.

  (6) Mshindi wa uchaguzi alikuwa Lawrent Mwakalibhule, mwanafunzi wa kidato cha 3 UDSM.

  (7) Mipango ya siku ya kuapishwa ni kuchinja ng'ombe mkubwa watu wale wafurahi huku wakijiandaa kwa ushindi mwingine 2015.
   
 2. m

  mandubu New Member

  #2
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu hongera kwa post nzito, imejitosheleza. hongereni sana makamanda, hakuna kulala hadi kieleweke.
   
 3. L

  Luiz JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2012
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante kwa taarifa kamanda ila nakurekibisha kidogo sio mwanafunzi wa kidatu cha 3 udsm bali ni mwanafunzi wa mwaka wa 3 udsm.
   
 4. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,569
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Engineering na sheria wanaita kitado! kwa kuwa ni miaka 4!
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeees Poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeer hiyo. Hii iendelee kuenea nchi nzima CCM ndo mwisho wao PIGA KURA LINDA KURA. Ahsante mdau kwa taarifa nzuri
   
 6. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Kunakitu mleta habali amekikisahau nacho ni Rechard Kasesela kutishia kuua kwa bastora. Alimtishia kumuua mbunge wa Vitimaalumu chadema Anna malaki pamoja na mwenyekiti wa chadema mbeya mjini Mwabigija maalufu kama Mzee wa Upako lakini tuliambiwa na polisi kuwa Kasesera atatafutwa mpaka sasa hakuna Taarifa ya kipolice juu ya hilozaidi ya Makamanda kufungua kesi zidi yake
   
 7. m

  mtengwa JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,745
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Hiyo ndo 2naitaga pipoz pawa
   
 8. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huko tunakoelekea kila mtu atalazimika kuwa na bastola yake. Hawa magamba wakishindwa kabisa kuchakachua ili wasalie madarakani wataanza kupiga watu risasi za moto.

  Wapi duka la silaha?
   
 9. M

  Molemo JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Nimefurahi tu jinsi Anne Kilango alivyoumbuka
   
 10. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Tunao watu wengi wa chadema wenye kuthubutu, wenye akili nyingi, wazalendo wa kweli na real great thinkers ni pamoja na wewe. Stay blessed.
   
 11. Mhoja

  Mhoja JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2012
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kila la heri
   
 12. L

  LOVI MEMBE JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,121
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  PEOOOOOOOOOOOOOOOOOPLES POWEEEEEEEEEEEEEER
  HII NI KALI YA MWAKA . MIMI NAOMBA WAKULIMA ZILE VOCHA ZA MAFISADI MWAKA WA 2015 WATENGE KABISA MAHINDI NA MAHARAGE YA KANDE DEBE MOJA MOJA @ NA MASEREMALA MBAO ZA MNINGA KWA AJILI SHUGHULI HIYO NCHI NZIMA ILI TULIE KILIO CHA TAIFA CHA CCM KUONDOKA MADARAKANI BAADA YA MIAKA 50 BILA MAENDELEO YA WANANCHI. SAFARI HII LAZIMA WANANCHI WAHIMIZWE KWA NGUVU ZOTE PEOPLES POWER CHADEMA LAZIMA ICHUKUE TUFINGE TUSIFINGE? QUOTE=Lawkeys;3651813]Nipo Kiwira sasa na nimepata nafasi ya kukutana na watu walionusa harufu ya mabomu ya machozi wiki iliyopita katika uchaguzi mdogo wa udiwani ulioipa CDM ushindi wa kishindo. Nimepata habari ambazo nahisi ni muhimu umma ukafahamu kuhusiana na uchaguzi huu.

  Toka nikiwa safarini kutokea Dar nimewasikia awtu wakiwa na hamasa ya hali ya juu wakizungumzia uchaguzi huu. Hamasa zaidi nimeishuhudia kwa vijana na wazee wakifurahia ushindi huu utadhani matokeo yametoka jana. Taarifa za msingi usizozijua:

  (1) Bodaboda walipewa na CCM lita Mbilimbili za Mafuta

  Vijana wamiliki wa bodaboda walijaziwa mafuta ili wahudhurie kwenye kampeni za CCM. Vija walipokea mafuta wakaenda kwenye kampeni za CDM huku wakikumbushana kwamba lita mbili zinawakilisha vidole viwili alama ya CDM na hata siku ya uchaguzi kauli mbiu iliendelea vivyo hivyo waliendelea kuonesha kidole gumba mbele (dole) kwajili ya kupokelea salio CCM lakini nyuma walificha vidole viwili kwaajili ya kupigia kura.

  (2) Ana Kilango na Wanawake wa Kiwira

  Inasimuliwa kwamba Ana Kilango aliwakusanya wanawake katika jengo la Bank Kata (Saccos) linaloendelea kujengwa ili kuwapatia kishika uchumba na CMM kwajili ya kura kesho yake. Inasimuliwa zaidi kwamba Ana na wenzake walipitia mlango wa nyuma kwa kubomoa bati fence ya mabati inayolizunguka jengo hilo.

  Wakiwa wamenza kugawana pesa, inasimuliwa kwamba kuna mtu kutoka ndani ya kikao hicho haramu alitoa taarifa kwa Kamanda wa CDM ambaye alisambaza taarifa kwa Makamanda ambao walisabisha mamia ya wananchi kuizingira nyumba hiyo wakizuia Ana na wengine kutoka ili Takukuru waje kuifanya kazi yao. Ili kuzuia aibu hii Ana na wenzake waliwasiliana na RPC ambaye alikuja na vikosi vya FFU na kuanza kupiga mabomu kiholela. Mzee mmoja amanbaye alikuwepo eneo la tukio anasema alimwambia RPC kwamba anaamini kwam ba RPC atakuwa shahidi wa ukweli wa jambo hili. Baada ya wananchi kukimbia Ana na wenzake walipata upenyo wakaondoka. Chakusikitisha ni kwamba kituo cha ITV katika taarifa ya usiku siku hiyo walitoa muda wa hewani kwa Ana ili apotoshe ukweli wa tukio hili. Makamanda waliendelea kupambana kwa kuzuia barabara mpaka Polisi walipoamua kuondoka.

  Ili kuthibitisha habari hii nimeambiwa na kada wa CCM kwamba yeye alikuwa ndani pamoja na Ana na wengine wakigawiwa pesa. Anasema kywamba walichanganyikiwa Makamanda walipowazingira. Anasema kwamba hali ilikuwa mbaya zaidi pale ambapo walikuwa wakijitahidi kudanganya kwamba kilikuwa ni kikao cha kawaida cha ndani cha chama, wakati huohuo wakinamama wengine walikuwa wanapayuka kwamba, "mimi nimepewa 10000/= ma mwingine mimi nimepewa 15000/=" kada anasema hali ilikuwa tete sana. Cha kusikitisha ni kwamba sijapata taarifa zozote za Pccb kufanya kazi yao juu ya hili.

  (3) Maboksi ya Kura ya Kamatwa

  Alfajiri ya siku ya kupiga kura,nimesimuliwa kwamba, gari ya halimashauri ya Rungwe ilikamatwa na Makamanda ikiwa na maboksi yaliyo na kura za CCM. Makamanda walitoa kichapo kwa dreva, wakanyang'anya funguo za gari na maboksi yakapelekwa kituo cha polisi. Lakini cha kusikitisha sijapata taarifa ya hatua za kisheria zilizochukuliwa.

  Ushauri kwa wazalendo, sio lazima kufungua malalamiko kupitia polisi kwani unaweza ukapeleka maelezo yako moja kwa moja mahakamani. Kwahiyo mtuhumiwa na maboksi katika kesi hii yangepelekwa mahakamani. Zaidi ya hapo chukueni hata kwa simu ushahidi wa video za matukio ya uharifu wa namna hii. Mkishitaki polisi au mahakamani ikashindikana ugeukieni umma kupitia midia, kwani ni rahisi na gharama nafuu, upload hiyo video kwenye youtube, fb, twitter, jf na uwaache wananchi wachukue hatua 2015.

  (4) Piga Kura Linda Kura

  Naambiwa kwamba katika kipindi chote cha Kampeni Makamanda kutokea Tunduma na Mbeya mjini walikua wakipata taarifa ya uchakachuzi wanamwagika kama umande. Walisafiri umbali mrefu kwa gharama zao binafsi. Wengi walitokea Mbeya mjini na Tunduma. Na siku ya kupiga kura ninaambiwa Makamanda waliagiza katika vituo korofi kura zipigiwe nje ya nyumba na wanawake hawakuruhusiwa kujitanda kanga kwani inasemekana zinatumika kufichia kura. Na baada ya kupiga kura, kura zililindwa.

  (5) Mazishi ya CCM

  Ukweli ni kwamba kwa jamii za watu wa Mbeya msiba ni kitu cha heshima ya juu sana na ni chachu ya kuwaleta watu pamoja. Sasa siku moja kabla ya kabla ya uchaguzi Wapenzi wa CDM walitengeneza jeneza kisha wakaivalisha kofia ya CCM huku wakiigiza kulia wakiwa wamebeba mahindi, maharage, mikeka kama inavyokuwa katika msiba wa kawida. Walikuwa wakiimba, "nani kaua? CDM". Na baada ya mazishi walikula kande ambazo walizipika wenyewe.

  (6) Mshindi wa uchaguzi alikuwa Lawrent Mwakalibhule, mwanafunzi wa kidato cha 3 UDSM.

  (7) Mipango ya siku ya kuapishwa ni kuchinja ng'ombe mkubwa watu wale wafurahi huku wakijiandaa kwa ushindi mwingine 2015.[/QUOTE]
   
 13. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #13
  Apr 8, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Hongereni sana tena sana wana wa Kiwira mmenifurahisha na ( Piga kura linda kura)
   
 14. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #14
  Apr 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  da ashukuriwe sana dr. kwa kuhamasisha wananchi kulinda kura,,,,,magamba wanang'ang'ania wananchi wakipiga kura waende nyumbani hairusiwi kubaki karibu na kituo cha kupigia kura...chadema inasema sheria inaruhusu kukaa mita mia na ngapi vile.....? baada ya kupiga kura, huwa wanazodoka sana magamba kwani sheria waliiweka wenyewe
  safi sana wana-kiwira hao dawa yake kuwashushua tu wakati wanatoa rushwa halafu kuwaacha maana hata ukiwapeleka polisi hakuna lolote litakalofanywa
   
 15. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #15
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Am very proud of my homeland. Naamini 2015 tutakomboa mkoa wote. No more magamba in our sacred land.
   
 16. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #16
  Apr 8, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Big up brother.....hii kasi hakuna kulala hadi 2015....tukalala inakula kwetu...
   
 17. K

  Kidoma Member

  #17
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nzuri imetulia na imefanyiwa utafifti ulioshiba!
   
 18. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #18
  Apr 8, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hongereni kwa ushindi huu ila umesahau kutueleza idadi ya kura za kila mmoja
   
 19. m

  makaka Member

  #19
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi SAMBWEE shitambala si alijidai kuwa ataibomoa CDM mbeya?? mbona kama ameshindwa kazi halafu amesahaulika kwenye u- DC, lo jamani ccm hamna huruma kwa mwenzenu??
   
 20. F

  Froida JF-Expert Member

  #20
  Apr 9, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Mama mmoja aliyemshuhudia Kilango unaambiwa aliona siku zake,miguu yote ililowa damu ha haha chejea CDM wewe
   
Loading...