CHADEMA washinda unaibu meya jijini Arusha kwa kura 27 kati ya 34

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
UCHAGUZI NAFASI YA NAIBU MEYA

Jumla ya wajumbe 34

1.PAUL PETER MATTHYSEN - CHADEMA #27

2.PROSPER REMMY MSOFFE - CCM #7

======

Arusha. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (chadema) jijini Arusha kimeshinda nafasi ya naibu meya wa Jiji baada ya mgombea wake Paulo Matthysen kumbwaga mgombea wa CCM, Prosper Msofe.

Uchaguzi huo uliofanyika leo baada ya kuapishwa kwa madiwani wanne wa CCM, ambao awali wote walikuwa ni wanacahama wa Chadema ni pamoja na Matthysen ambaye ni diwani wa Mushono amepata kura 27 za madiwani wote wa chadema na Msofe ambaye ni diwani wa Daraja mbili amepata kura saba za madiwani wote wa CCM katika baraza hilo.

Akitangaza matokeo hayo, Mwanasheria wa jiji, Grayson Orcado amesema wapigakura halali katika uchaguzi huo walikuwa 34 na hakuna kura iliyoharibika.

Akizungumza baada ya kutangazwa kwa matokeo, Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro amesema ushindi huo umedhihirisha kuwa madiwani wa chama hicho bado wako imara jijini humo.

“Ushindi huu unaonyesha bado tupo imara, lakini pia leo tumempokea mkurugenzi mpya, Dk Maulid Madeni aliyeteuliwa na Rais John Magufuli, tunaahidi kumpa ushirikiano wa kutosha,” amesema meya huyo.

Amesema kikao hicho ambacho ni cha robo ya nne ya mwaka, kimewachaguwa pia wenyeviti wa kamati wote kutoka chadema.

Meya Lazaro amesema Diwani wa Sombetini, Ally Benanga alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya mipango miji na diwani wa Ngarenaro, Isaya Doita alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya elimu, afya na uchumi.

Wakati huo huo, kabla ya uchaguzi huo, madiwani wanne wa CCM walioshinda katika uchaguzi wa Agosti 12 wameapishwa leo. Madiwani hao ni Msofe wa Daraja mbili, Emmanuel Kessy wa Kaloleni, Obedi Meng'oriki wa Terati na Elirehema Nnko wa Kata ya Osunyai .

Chanzo: Mwananchi
 
Siamini kama hii ni kweli, kama ni kweli basi ni suala la muda tu tutasikia CCM wametimua madiwani wao waliomkataa Msofe kuwa Naibu Meya.

Pili, kwa matokeo haya, ni wazi wana CCM kindakindaki hawana imani na hao wahamiaji waliohamia kutoka upinzani, hii ni ishara mbaya kuwa CCM kuna vyama viwili ndani, CCM chotara na CCM kindakindaki.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.....
.....Mkuu kwa siriiiiii sana
 
Arusha sio jiji la Chadema, ni moja ya majiji ya Nchi ya Tanzania. Au huko Ufipa mnaitambua Chadema kama Nchi?
 
Siamini kama hii ni kweli, kama ni kweli basi ni suala la muda tu tutasikia CCM wametimua madiwani wao waliomkataa Msofe kuwa Naibu Meya.

Pili, kwa matokeo haya, ni wazi wana CCM kindakindaki hawana imani na hao wahamiaji waliohamia kutoka upinzani, hii ni ishara mbaya kuwa CCM kuna vyama viwili ndani, CCM chotara na CCM kindakindaki.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama Tanzania ingekuwa na makabila haya ya mikoa hii ya Arusha, Kagera, Kilimanjaro, Mara {Musoma}, Mbeya
Katika maswala ya utawala ingekuwa jino kwa jino

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema wana madiwani wengi Arusha , automatically lazima washinde . uchaguzi wa naibu meya kila nusu wa muhula wa miaka mitano it is just procedure matwaka ya kikatiba..huna sababu ya kusherekea ushind hapa jukwaani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siamini kama hii ni kweli, kama ni kweli basi ni suala la muda tu tutasikia CCM wametimua madiwani wao waliomkataa Msofe kuwa Naibu Meya.

Pili, kwa matokeo haya, ni wazi wana CCM kindakindaki hawana imani na hao wahamiaji waliohamia kutoka upinzani, hii ni ishara mbaya kuwa CCM kuna vyama viwili ndani, CCM chotara na CCM kindakindaki.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
Wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii. Waache wafu wazike wafu wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema wana madiwani wengi Arusha , automatically lazima washinde . uchaguzi wa naibu meya kila nusu wa muhula wa miaka mitano it is just procedure matwaka ya kikatiba..huna sababu ya kusherekea ushind hapa jukwaani

Sent using Jamii Forums mobile app
Uchaguzi wa wazi CCM hawawezi kushinda CCM itashinda kwenye chaguzi za siri wanazoweza kuiba, hata huu wangekuwa na uwezo wa kuiba wangeiba umesahau figisu za uchaguzi wa meya wa Kinondoni.
 
Back
Top Bottom